Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu(breakfast, lunch na dinner) ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.
Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.
Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.