Mimi baba wa watoto watatu ratiba yangu ya asubuhi na jioni

watoto wangu wakirudi shule huwa nawauliza maswali haya:
1. siku yako ilikuwaje
2. kitu gani kipya umejifunza leo?
3. kitu gani hujakipenda siku ya leo?
4. hapo shuleni kwenu kuna sheri ipi ambayo unaona haiko sawa?
5. kuna mtu amekukorifisha leo?
6. ulipocheka shule kwa saut kubwa nini kilikufurahisha?
7. kuna swali umemuuliza mwalim darasani ? na ulielewa kila somo ulilofundishwa?
8. njian wakat unaenda au wakati unarudi umeona kitu gani kipya ambacho hujawahi kukiona?..ulikipenda?
9. ratibaya chakula cha mbwa leo ikoje na umecheza mchezo gani leo?..
10. mmefanya homework? na ratiba ya kujisema lweo ni somo gani
11. niulize swali lolote

hayo huwa ndo maswali yangu wa wanangu na huwa tunainjoy sana mazungumzo hayo na wanaipenda session hiyo kinoma.. niwepo home au nisiwepo ntapiga simu tutaongea...
 
Safi sana, hii pia inawahimarishia confidence yao
 

Best Dad Ever.
 
Hiyo ratiba uzeeni itakuja kutesa, watoto nao watakuwa busy na mama yao, wewe watakuacha peke yako coz huna chemistry nao. Hiyo mifugo muda huo hutakuwa na uwezo wa kuihudumia.
Hahaaaaa, kimsingi hata ufanyaje watoto watakuacha tu nami nimeshajiandaa kwa hilo. Watoto hawatakaa.na Baba milele.
 
Mzee Maisha yangu yenyewe ni mazoezi tosha. Mazoezi mnafanya nyie kula kulala ila sisi tunaoshinda mashambani maisha tu ni mazoezi.
Acha kupanic kirahisi hivyo kama mtoto mdogo. Naamka sa 12 nafanya mazoezi kwa nusu saa mpaka dakika 45 naenda kuwaandalia kuku vyakula na maji kwakua kila kitu kipo settled hainichukui muda sana. Nikitoka hapo najiandaa naingia ofisini sa 2.

Ungeweza kunijibu vyovyote ila kuniita kula kulala umenikosea sana mdogo wangu. Kufanya mazoezi siyo lazima usiwe na majukumu. Pangilia muda wako vizuri acha excuses za kimama.
 
Kuna upweke wa uzeeni mzee..mke yupo busy na watoto wewe ata simu hupigiwi
 
Kuogesha watoto!
Hell NO!!

Ratiba za kurudi nyumbani mchana ni za kitoto sana, wewe ni mtoto mwenzao kama sio benteni.

Huyo mkeo anarudi sangapi?

Watoto mzae wawili. Kuhangaika ahangaike mmoja! Kuna tatizo gani ukiogesha mwanao wa kuzaa?? Akili finyu za wanaume wa kiafrica!!!
 
. Mimi huwa nawaogesha but mara moja moja. Wakati mwingine watoto huwa wanagoma kuogeshwa na mama wanamtaka baba. So nachip in. Mke huwa anarudi mapema zaidi. Saa tisa au kumi huwa yupo home.

Asikuzingue huyo, there is nothing wrong kwa wewe kuogesha wanao hata kama kila siku! Achana na hao matasa wa kiume wewe wanao utaona matunda yake uzeeni
 
Kidume unarudije jioni saa 11.unazidiwa mpaka na watoto ambazo wengine hurudi mida ya dinner aisee.

By the way mm saa kumi na moja kasoro nishasepaa narudi saa 2 kasoro nabana chemba namkula vyombooo mpaka saa 6 au Saba ndo narudi home. Kiufupi hata wanangu Huwa wananisahau Mimi Kama ni baba yao maana hata siku ya off Huwa simalizi masaa 4 nkiwa home
 
Namna hii, unashindwa kuweka bond na watoto... bond na familia yako inapotea.
 
Nakuunga mkono kwa asilimia zote. Endelea hivyo hivyo...
Unawekeza kwa watoto, utakuja kuona Faida yake baadaye....
 
Naendelea kajifunza kwenu wazazi

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ratiba uzeeni itakuja kutesa, watoto nao watakuwa busy na mama yao, wewe watakuacha peke yako coz huna chemistry nao. Hiyo mifugo muda huo hutakuwa na uwezo wa kuihudumia.
Haya maisha hakuna namna baba utaweza kubondi na watoto hadi uzeeni, labda uwe na mali na utapendewa mali..... ukiwa na maisha ya kuunga watoto ni rafiki wa mama yao tu.
Ushahidi na uzoefu unaonesha hivyo, hata wewe ni shahidi.
 
Wamama watakusifu sana humu -
Unaratiba nzuri..ingawa wanaume tunamaisha magumu kidogo - sio kama unavyoyaelezea hap😵therwise utakuwa na shida mahali au una- advantage kuliko wanaume wa kawaida wanaojitafuta - au umetengenezewa maisha tayari..
Kuna dereva malori, daladala, bodaboda, kuna wafanyabiashara wanatembea mikoani huko kutafuta fursa, kuna wafanyabiashara jioni ni kutafuta watu wa kuwapa connection , kuangalia kama mambo yataenda, kuna wanajeshi wapo mbali huko kutimiza majukumu yao..n.k wengi wa hizo kazi ni wanaume..

Ratiba yako ni nzuri na wanaume tunaitamani LAKINI ni nadra sana kwa mwanaume kuwa na ratiba CALM kiasi hicho- maisha sio mepesi haya...
 
Ukipata pesa ambazo za maana hiyo ratiba itabadirika, mwanaume huwezi rudi nyumbani saa 11.

Mwanaume akitoka kazini ananipia kwa amina mchepuko kwa waifu anaenda saa 2 usiku.

Sipendi hii comment yangu initokee ila huu ndo ukweli na vile hatupendagi ukweli nasi nitatukanwa.

Sisi wanawake tunajua ratiba ya mwanaume mwenye maokoto na mwanaume unga unga.
 
Wewe ni mkufunzi bila shaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…