Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia

Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia

sure,
bado kuna yapo mengi yafaa kurekebishwa na kuboreshwa zaid hususan elimu ya kilimo cha kisasa.
Na wizara husika inafanya kazi kubwa sana kwenye hili.

Rais, mkuu wa nchi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan anashauriwa vizuri sana kwenye sekta ya kilimo na hata kufikia hatua ya kuanzishwa na kuipa mtaji benki ya kilimo.

Graduate wanayo fursa za ajira bwerere na ya wazi sana kwenye sekta ya kilimo iliyoboershwa sana. Zaidi sana wana fursa kwenye ufugaji, biashara, usafirishaji n.k.

lakini pia wanayo fursa ya wazi kabisa ya kiuchumi, kwani katika kila halmashauri nchini, kuna kuna fedha za mikopo kwajili ya vijana. waungane na kwenda kuchukua mikopo hiyo na kujiendeleza kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Tanzania tunaheshimu haki za binadamu mno ukilinganisha na nchi yoyote Africa Mashariki na Africa kwa ujumla. Nchi yetu haiko katika viwango vya uvunjifu wa haki za binadamu na ndiyo maana ulimwengu mzima unajua kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani na upendo.

Hata hivyo,
Ifahamike duniani kote, yeyote atakae jaribu kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wananchi Tanzania atashughikiwa kwa nguvu zote, kwani Amani ya waTanzania italindwa kwa nguvu gharama zote bila mbambamba ya nchi yoyote ya kigeni au kibaraka wao yeyote humu nchini.

Mimi ni kiongozi wa wananchi na ni raia mwema mzalendo wa Taifa hili, mchapakazi nisiestahili kupewa chochote bali furaha na amani yangu ni kuona wananchi wanapata mahitaji yao muhimu kwa kujitosheleza 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Vipi kuhusu Civil Servants nimeongelea hapo juu khasa statecraft, vipi maoni yako?

Waamini tunao CS na Statecrafters waloiva?
 
Kanuni ya kiuongozi inasema wapumbavu uchaguana wao kwa wao na wenye akili uchaguana wao kwa wao..

hivyo nchi ikiwa na rais mpumbavu basi uchagua wapumbavu wenzie kuongoza na kumshauri ...pia nchi ikiwa na rais mwenye akili uchagua wenye akili kuongoza na kumshauri .....SASA MSHAURI WA RAIS WAKO MMOJAWAPO NI MWIGURU CHEMBA YA MAVII.... UNATEGEMEA NINI ?
Na wote wamenunu PhD
 
Lazima kama taifa mna matatizo makubwa sana.

Kabisa watu wenye akili timamu mumpe Samia miaka mitano tena.

Hata mimi ambae simjui sihitaji ushawishi, ni mama mwenye uwezo mdogo sana.

Sasa sijui wale ambao wana interact nae, tuache utani kwenye shughuli ya kuongoza nchi.

Samia hana uwezo.
Kumbe shida ni wewe sqsa, unasema humjui halafu unasema hana uwezo, umemjuaje?
 
Vipi kuhusu Civil Servants nimeongelea hapo juu khasa statecraft, vipi maoni yako?

Waamini tunao CS na Statecrafters waloiva?
Actually,
watumishi wengi wa umma wana ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na kazi na majukumu yao ndani ya huduma wanazotoa kwa wananchi,

na kwakweli wako neutral na wanatekeleza wajibu wao kwa haki, usawa, weledi na bila upendeleo wa rangi, dini, ukabila au mirengo ya kisiasa, ingawa kwa nadra na uchache sana, vipo visa na mikasa ya upendeleo hususan kutoka kwa watumishi wachache wasiokua na sifa, waliojipenyeza kazini kiujanja ujanja, hao ndio wamekua wakiharibu taswira ya utumishi wa umma kwa kiasi. hata hivyo kazi zimekua zikifanyika kwa ufanisi sana kwa sehemu kubwa.

Infact,
Mwenyezi Mungu ametujaalia kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan, kiongozi mwanamke madhubuti, mwenye sifa na vigezo stahiki vya kiujuzi katika uongozi..

Na ndio maana tunaiona wazi dhamira na nia yake njema na thabiti ya kuliunganisha Taifa, na kuifungua nchini miongni mwa mataifa ya ulimwengu. Tanzania inaaminika duniani, Tanzania inakubalika duniani, Tanzania inaheshimika mno duniani na ndiyo maana mataasisi makubwa makubwa ya ulimwengu kama vile IPU, WHO, IMF n.k kanda ya Africa yanaongozwa na waTanzania, na miongni mwao waliwahi kua maCS.

kwa kuhitimisha,
tunao statesman and woman walioiva vilivyo kuongoza nchi, kuongoza wizara, mamlaka, mashirika, asasi, na taasisi za umma kwa umahiri na weledi mkubwa kulingana na taaluma zao.

Hatahivyo,
pakitokea changamoto, hurekebishwa na kusahihishwa mara moja, ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu kazi mpya ambayo kama Taifa tunayo hazina ya kutosha ya wajuzi 🐒
 
Hebu niambie mwendazake aliharibu uchumi wapi? Yule jama alikuwa Hana human rights, lakini uchumi kuharibu hapana labda nipashe
Alikimbiza wawekezaji wote ajira ikawa ni kizungumkuti kwa vijana hususani mabank na mahotel mbalimbali. Waliokuwa wanafanya kazi mahotelini wakawa wanazurula mtaani tu. Kwenye mabank vijana wakawa wako mtaani mana mabank yamefungwa. Watu kama akina manji waliajiri kama vijama 60,000 baada ya kifunga vijana wakawa jobless mtaani na serikali haiajiri kabisa labda wa kudokoa dikoa. Huu ndo uhalibifu wa uchumiana uchimi ni watu. Ndoa au familia nyingi zilijinyonga au kufa kwa mastress au njaa
 
Labda ungeweka reference
Manji aliajiri watu 60,000 nani hajui historia ya Manji?
Alikimbiza vipi watalii wakati alinunua ndege na kutofunga nchi wakati wa COVID?

Uliwahi kusikia wakati ule dollar hakuna? Chimba sana utaona kuwa yule jamaa ingawa alikuwa katili lakini alikuwa na charisma na nchi yake.

Haya ni machache tu. Samia hamfikii yule bwana hata kidogo. Kweli Samia ni mwema lakini hana vision, she is in proxy
 
Watu wamerudi kazini leo amba five years zilizopita wanarandaranda mtaani hawana kazi au wamefukuzwa kisa investment yao imefungwa au imejifinga. Mfano ngurdoto, mabank mbalimbali, siasa hasa vyama vya uponzani vimeajiri watu kibao. Korosho mtwara imepanfa bei nk. Yule jamaa alihalibu kila kitu
 
Kusema ukweli kabisa huyu bibi katuharibia Nchi iliyokuwa inamwelekeo mzuri.Umakamu aliupata ili kutimiza matakwa ya huu muungano feki lakini siyo kwamba Kwa uwezo wa kuongoza na Bahati mbaya ikatokea vile na ikawa kukubaliana na Hali.
All cards on the table and honesty as our guide, yanayoendelea a sasa ni;

1)MAKOSA YA WANANCHI WENYEWE na sio Mtu “aliepewa “ urais .
 
Kuna criteria’s za mtu ambae ni coachable kwa nafasi ya uraisi.

Samia ni un-coachable simply kwa sababu uwezo wake ni mdogo mno.

Tatizo unaliona lipo kwenye civil servants, wengi ni uwezo wao mdogo sana.

Asilimia kubwa ya senior civil servants wa TRA awaelewi hata sheria za kodi, leave alone the changes which comes with the new budget. But most don’t understand the accounting principles behind the VAT act.

Ni hivi, sasa kumuongelea huyo raisi wenu Ndio shida kabisa.

Ndio maana, sioni tatizo la Tanzania kama Samia; isipokuwa 90% ya senior civil servants hawana sifa ya nafasi walizonazo.

Na wengi hawajawahi ata kusoma vitabu vya siasa it’s obvious. I can’t waste my time to justify that kwa sababu hata kwenye hili jukwaa la siasa I can go as far as to say 99% ya wachangiaji hawajawahi kusoma kitabu cha siada at foundation level.

Ndio uhalisia
.
 
Watu wamerudi kazini leo amba five years zilizopita wanarandaranda mtaani hawana kazi au wamefukuzwa kisa investment yao imefungwa au imejifinga. Mfano ngurdoto, mabank mbalimbali, siasa hasa vyama vya uponzani vimeajiri watu kibao. Korosho mtwara imepanfa bei nk. Yule jamaa alihalibu kila kitu
Unajua maana ya investment? Labda tuanze hapo. Mwenye pesa anajenga hoteli halafu anaajiri watu (kujenga na baadaye kuendesha hoteli).

Bwawa la Nyerere limejengwa ( wanengaji wameajiriwa na waendeshaji wataajiriwa). Umeme utazalishwa utauzwa viwanda vitafunguliwa kwa wingi, majumbani watu watanunua umeme unaona. Biłan investment ya infrastructure utaaajiri vipi? Hata service sector inahitaji infrastructure.

Railway investment watu watapanda train watalipa na wataajiriwa watu na deni litalipwa.

Wewe ulitaka magu awe anaajiri watu kuwalipa mshahara kukopa hiyo siyo investment ni indirect, unayemlipa harudishi

Simple economics
 
Mkuu leo imekuwaje??? Nakuunga mkono kwa asilimia zote.

Kila mtanzania angekuwa anawaza kina namna hii Magufuli na huyu mama wasinge ruhusiwa kufika huko.

Tafakuri za namna ndizo ya kutunasua hapa tulipogota.
Magufuli huyu huyu alieongoza zoezi la kutandika mkeka wa moto karibia asilimia 80 ya nchi hii for the sole purpose of the country’s & its peoples financial freedom through sustainable infrastructures? Ndio wa kumuweka kapu moja na Rais Samia?

By the way, Rais Samia anao uwezo mkubwa sana tu katika “kile anachokifanya na Ndio maana hata the powers that be (hao state capturers) wamemfikisha hapo alipo sasa, “Kazi yake Inaendelea na inawaridhisha (if they do exist).

2025 will be so politically interesting, (Spiritually even more jaw dropping).
 
Unajua maana ya investment? Labda tuanze hapo. Mwenye pesa anajenga hoteli halafu anaajiri watu (kujenga na baadaye kuendesha hoteli).

Bwawa la Nyerere limejengwa ( wanengaji wameajiriwa na waendeshaji wataajiriwa). Umeme utazalishwa utauzwa viwanda vitafunguliwa kwa wingi, majumbani watu watanunua umeme unaona. Biłan investment ya infrastructure utaaajiri vipi? Hata service sector inahitaji infrastructure.

Railway investment watu watapanda train watalipa na wataajiriwa watu na deni litalipwa.

Wewe ulitaka magu awe anaajiri watu kuwalipa mshahara kukopa hiyo siyo investment ni indirect, unayemlipa harudishi

Simple economics
Mahotelo yote yaliyofungwa yanafanya kazi sasa hivi elewa hivyo
 
Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza raisi Samia.

Bora nikalime huko, kuliko kupokea orders kutoka kwake.

Hana uwezo hata chembe.

That says a lot ueledi wa civil services,

It’s a shitty county (ndio uhalisia).
Umeandika kitu gani wewe bumla! Kwa ulichokiandika Rais Samia hapotezi kitu chochote. "Ueledi", " county" hapa umekusudia nini? Kwanza Rudi shule! Lakini umeshacherewa.. hata huko Kwenye kilimonkwa uwezo wako utaishia kilimo cha jembe!. Au umeanzisha Uzi na wewe uonekane Tu halafu cha kushanga imeenda mpaka page 10 2/3 ukiwa umechangia wewe mwenyewe.
Hii ni aibu Kwa JF na hapa ilipofikia
 
Na hapo ndipo hoja ya yeye kukosa akili inapata nguvu Angekuwa na uwezo binafsi,angeng'amua kuwa kuna mifumo mingine inafanya mambo nje ya maelekezo yake na angetumia akili zake kurekebisha.
Kinachotufanya tuamini kwamba yeye Rais Samia hajui kwamba kuna mifumo nje ya mfumo wake nini?

Kwamba sisi wananchi tunaona mapungufu na madhambi waziwazi kwenye 18 ya Rais huku yeye Rais aliekaa mlangoni haoni kabisa?!

Kwani wale wanaotuhumiwa “kuuza mechi” huwa wanakua ni viumbe wa aina gani?!

Binafsi; natambua Rais Samia anao Uwezo mkubwa sana katika kuicheza Namba yake na wale waliopo nae kwenye team yake wanalitambua hilo na Ndio maana yupo hapo alipo sasa hivi.
 
Back
Top Bottom