Mwalimu Kambarage Nyerere, alipokuwa anazungumza kuhusu Ujamaa, kiuono na ufikirifu mifumo, alikuwa akijinasibu na kitu tunachokwenda kukifahamu kama
'Jeometria ya Utendekavyo Maamuzi' ambavyo ni kadiri pia kusema: ikiwa 'fahamu za watu/wanajamii' hazitanuki kupita miktadha ya ELIMU 1.0, tabia, mienendo na vitendo vyao huzaa 'Matriksi' ilivyo ni >
'MCHE MRABA--KUBU'< ya 'UDHALIMU'. Lakini ikiwa fahamu za watu/wanajamii zinatanuka kufaa ELIMU 2.0 hili huleta >
'TETRAHEDRONI'< ya >
'NYOTA ya UKOMBOZI'<...
Basi Mwalimu alikuwa na Mwangaza wa haya, na kwa wakati alizungumza ya kufaa kwa umma; kuna yanayofaa kufahamika wakati unapokuwa sahihi -- yakifahamika kabla ya wakati sahihi, badala ya kuleta matunda thabiti, yataleta matunda legevu katika muktadha wa maendeleo na ustawi wa umma. Hapa tulipo, kama wanajamii, tunao ufunguo wa kukadirisha ikiwa tunda letu la kujinasibu na 'kujua ilivyobora' linakwenda kuwa ni thabiti ama legevu... Hapa tulipo, ni kama vile tunakaribia kujitazama katika kioo-->
ili kuachana na 'utoto'<...
Kwa hivyo Mwalimu Kambarage Julius Nyerere alikuwa anajua fika mapelekeo ya kusema:
Ujamaa pia ni tabia na vitendo, ujamaa ni uhusiano wa mtu na mtu na mtu na umma, ni usawa na utu, ni kuheshimu na kuheshimiana, ni haki na ni wajibu na mambo haya hayapatikani kwa amri wala kwa sheria... Huu ni 'Uono na Ufikirifu Mifumo'; Mtu wa uono na ufikirifu mifumo huona mambo kwa 'mahusiano na vitendo' na wala si 'miundo' na 'udhibiti'. Ushawishi wa mambo huwa na sura mbili kwa wakati mmoja, kutoka juu kuja chini na hapo hapo kutoka chini kuelekea juu... Ndivyo basi kwa nini 'kuheshimiana', kiujamaa, ni 'udugu'--si 'ubwana mkubwa na ubwana mdogo'... Ni 'haki' na 'wajibu' ambavyo mambo haya hayapatikani kwa 'amri' wala 'sheria'...
Kwa muktadha huu, ni vema kutambua: kule kufikiria kwetu Katiba kama 'Sheria mama' inaweza kuleta 'haki' na 'wajibu' kuna namna ni ufikirifu mushkeli wa kielimu, ELIMU 1.0... Ukosefu wa maadili na kutothamini mipaka ya mambo kwa 'jicho la staha' na 'nidhamu' haya ni mapungufu ya 'kitabia' katika 'Utu' wa mtu... Mtu wa daraja la chini la akili, husukumwa utendaji wake na 'vina vya tafsri' ya mambo vilivyo ni vya juu juu--hata kwa taratibu za maisha yake. Mtu wa namna hii ni rahisi kudhibitiwa kiakili kwa >
'mifumo ya usadikifu'< na 'mienendo ya kipambe'-->
maisha ya mkumbo<... Hili lafanya kwanini 'Sheria na Amri' ni vitu vya kufaa watu wa ufahamu wa chini kiakili, lakini 'uwajibikaji' na 'kujituma' ni nasibu ya 'ufahamu wenye kuinuka/kuchachuka'... Yesu amepata kuzungumza busara ya jambo hili hili katika muktadha wa 'Utaasisi na Mapokeo': Musa aliwapa watu >
'Sheria za Taratibu za Maisha'< kwa shauri ya 'Mioyo' yao ilikuwa ni migumu...