Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia

Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia

Kama kweli Nchi hii kuna wazalendo wa kweli na wana uchungu wa Nchi hii na wanataka kukumbukwa katika historia ya Nchi hii, hata kama ni CCM wenyewe, watuletee mgombea mwingine wa Urais mwaka 2025.
Mama apumzike na apewe heshima yake yote kama Rais mstaafu.
Hapo wewe ukiwa Ndio Mwananchi (mwenye nchi) unafanya kazi gani kuhakikisha hilo linafanyika?!
 
sure,
bado kuna yapo mengi yafaa kurekebishwa na kuboreshwa zaid hususan elimu ya kilimo cha kisasa.
Na wizara husika inafanya kazi kubwa sana kwenye hili.

Rais, mkuu wa nchi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan anashauriwa vizuri sana kwenye sekta ya kilimo na hata kufikia hatua ya kuanzishwa na kuipa mtaji benki ya kilimo.

Graduate wanayo fursa za ajira bwerere na ya wazi sana kwenye sekta ya kilimo iliyoboershwa sana. Zaidi sana wana fursa kwenye ufugaji, biashara, usafirishaji n.k.

lakini pia wanayo fursa ya wazi kabisa ya kiuchumi, kwani katika kila halmashauri nchini, kuna kuna fedha za mikopo kwajili ya vijana. waungane na kwenda kuchukua mikopo hiyo na kujiendeleza kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Tanzania tunaheshimu haki za binadamu mno ukilinganisha na nchi yoyote Africa Mashariki na Africa kwa ujumla. Nchi yetu haiko katika viwango vya uvunjifu wa haki za binadamu na ndiyo maana ulimwengu mzima unajua kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani na upendo.

Hata hivyo,
Ifahamike duniani kote, yeyote atakae jaribu kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wananchi Tanzania atashughikiwa kwa nguvu zote, kwani Amani ya waTanzania italindwa kwa nguvu gharama zote bila mbambamba ya nchi yoyote ya kigeni au kibaraka wao yeyote humu nchini.

Mimi ni kiongozi wa wananchi na ni raia mwema mzalendo wa Taifa hili, mchapakazi nisiestahili kupewa chochote bali furaha na amani yangu ni kuona wananchi wanapata mahitaji yao muhimu kwa kujitosheleza 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Kama Tanzania inaheshimu haki za binadamu sana ongea shiti kuhusu samia. Ongelea madhaifu yake kwenye mitandao yote ya kijamii just for one month kisha urudi kutuambia namna ambavyo haki za binadamu zinaheshimiwa humu nchini kwetu.
 
Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza raisi Samia.

Bora nikalime huko, kuliko kupokea orders kutoka kwake.

Hana uwezo hata chembe.

That says a lot ueledi wa civil services,

It’s a shitty county (ndio uhalisia).
Upo sahihi kabisa na mimi nasimama na wewe una hoja kabisa
Ngoja mpiga kinubi Lucas muoshambwa aje
 
Siwezi kusema Rais hana akili wala uwezo. Akili anayo lakini siyo ya kutosheleza mahitaji ya nafasi anayoishikilia.

Nafasi anayoishikilia inahitaji akili kubwa, uwezo mkubwa, maarifa ya kutosha. Kwa ufupi ni kwamba tumebebesha tani 50 za mzigo kwenye bajaji. Japo siyo kweli kuwa bajaji haiwezi kubeba mzigo.

Kama Rais atakuwa na uwezo wa kuifikia hekima, ni vema sana amalizie tu kipindi hiki alicholazimika kuchukua madaraka kwa mujibu wa katiba yetu hii mbovu, kisha apumzike; na Taifa limshukuru kwa hicho alichokikamilisha. Akikosa hekima, akadanganyika na hawa punguani machawa njaa wanaompa sifa za uwongo, kipindi cha miaka 5 itakayofuata, kitakuwa kigumu sana kwake, kwasababu uvumilivu wa watu wenye akili dhidi yake utazidi kupungua siku baada ya siku, na atakuja kuwakumbuka wote waliomshauri apumzike. Anaweza kuishia kupata stress za ajabu, zitakazodhoogisha sana hata afya yake.
 
Bado hujaeleweka, kwa mfano ameshindwa kuongoza nini?

Mbona Uchumi unakuwa, Mikopo kwa Wanafunzi wa level zote Diploma & Degree ipo, Mikopo kwa Wakulima inapatikana, Miradi mikubwa inaendelea kutekelezwa

Umeona kuna Mkwamo wapi?
Pamoja na kuwa sikubaliani na wewe juu ya hayo uliyo yataja ndicho kiwe kipimo cha uongozi, nakubaliana na wewe kwamba mleta mada hajaeleza popote kwa ufasaha wa kueleweka ubovu wa uongozi wa Samia ni upi hasa.

Natamani mjadala ungejikita huko zaidi kuliko ulalamishi wa kiujumla jumla tu kama unao fanyika hapa.

Ukweli kwamba Samia hana uwezo wa kuwa kiongozi wa nchi unaonekana katika mambo mengi tu; lakini hasa kimsingi zaidi ni kuwa Samia hana uwezo wa kujuwa nchi inako elekea (Dira); lakini hata kama angekuwa anajuwa hana uwezo wa kuielezea na kuisimamia hiyo dira.
Chukulia ule mfano wa uigizaji wa zile "4R", alizo tengenezewa na wanao mzunguka ili aonekane ana maono fulani. Hata waliozitengeneza hawaku jishughulisha na kumfundisha maana yake ni nini ili aweze kuwasilisha maono hayo kwa wananchi; ambao ndio walengwa wa maono yenyewe!

Tatizo langu kubwa dhidi ya uongozi wa Samia, ni kuua moyo wa nchi hii; wananchi kujuwa nafasi yao katika kulijenga taifa lao. Ni wajibu wa waTanzania kuleta maendeleo yao, si wajibu wa mtu mwingine yeyote toka nje. WaTanzania sasa wanabaki kuandaliwa tu watumike kama watwana wa hao anao watengenezea mazingira toka huko nje. Kamwe hatuwezi kuwa na taifa la namna hiyo na kujisifu kwamba sisi ni taifa linalo endelea.

Kwenye hili, ni dhahiri kabisa kuwa Samia anajipambanua kuwa adui mkubwa wa nchi hii, na siyo kiongozi wake.
 

Attachments

  • Screenshot_2024-10-26-18-00-36-109_com.linkedin.android.jpg
    Screenshot_2024-10-26-18-00-36-109_com.linkedin.android.jpg
    410.5 KB · Views: 2
Siwezi kusema Rais hana akili wala uwezo. Akili anayo lakini siyo ya kutosheleza mahitaji ya nafasi anayoishikilia.

Nafasi anayoishikilia inahitaji akili kubwa, uwezo mkubwa, maarifa ya kutosha. Kwa ufupi ni kwamba tumebebesha tani 50 za mzigo kwenye bajaji. Japo siyo kweli kuwa bajaji haiwezi kubeba mzigo.

Kama Rais atakuwa na uwezo wa kuifikia hekima, ni vema sana amalizie tu kipindi hiki alicholazimika kuchukua madaraka kwa mujibu wa katiba yetu hii mbovu, kisha apumzike; na Taifa limshukuru kwa hicho alichokikamilisha. Akikosa hekima, akadanganyika na hawa punguani machawa njaa wanaompa sifa za uwongo, kipindi cha miaka 5 itakayofuata, kitakuwa kigumu sana kwake, kwasababu uvumilivu wa watu wenye akili dhidi yake utazidi kupungua siku baada ya siku, na atakuja kuwakumbuka wote waliomshauri apumzike. Anaweza kuishia kupata stress za ajabu, zitakazodhoogisha sana hata afya yake.
Hiyo "hekima" unayo mtaka yeye awe nayo/aionyeshe, hilo ni tamanio asiloliona yeye kuwa na maana yoyote, na kusema kweli sijui kama unaliwasilisha hapa ukiwa na matumaini ya yeye kufanya hivyo!

Kama kulikuwepo na kundi lilillo ona toka mwanzo kuwa nafasi hiyo haimtoshi wakati ule, hata kabla ya kushuhudia uwezo wake kama sote tulivyo shuhudia sasa; kwa nini kundi hilo na wengine ndani ya CCM wasijitokeze sasa, ndani ya chama chao au hata nje, kupaza sauti za kukataa mtu huyu kuendelea kuwepo kwenye nafasi hiyo?
Tanzania itaumia sana endapo huyu mama atashikilia tena nafasi hiyo kwa miaka mitano.
 
Ofcourse kama unachota billions za madili bila kelele lazma awe best president ever happened to you.
Hakuna Raisi amewahi pita akaongelewa vizuri,anaongelewaga vizuri akisha kuwa nje ya system,Kwa hiyo hata huyu tutaona wema wake akisha sepà! Siku Mjomba Magu ana Rest in peace,wapo walio chinja Hadi mbuzi kusherehekea kifo wapo ambao nawajua hata huku mtaani ila Leo wanasema Dah kuna vitu mwamba angekuwepo mara hivi mara vile,Kikwete Hadi aliitwa Mzee WA kuchekacheka,ana kichwa kibovu hata Nazi ina thamani! Hakuna Raisi hajatukanwa Ila alionekana ukubwa wake baada ya madaraka sasa Kwa nini nisiseme hata Mama ni Moja ya maraisi wazuri hawajawahi tokea nchi yetu!
Tupambane wazee hakuna atakaye kuletea ugali mbuzi mezani zaidi ya wewe!
 
Majibu ya namna hii yanaashiria kuishiwa hoja. Jibu hoja ya mleta mada kuwa Rais ana uwezo mdogo sana kulinganisha na nafasi anayoishikilia.
je ametoa ushahidi kuwa ana uwezo mdogo,wakati kuna ushahidi ulio waziwazi wa maendeleo makubwa chini ya usimamizi chini ya samia
 
Kama Tanzania inaheshimu haki za binadamu sana ongea shiti kuhusu samia. Ongelea madhaifu yake kwenye mitandao yote ya kijamii just for one month kisha urudi kutuambia namna ambavyo haki za binadamu zinaheshimiwa humu nchini kwetu.
gentleman,
unless mtu hafahamu kuhusu haki za binadamu. Na by the way haki ina ambatana na wajibu.

haki za binadamu sio makelele au kulalamikia kudhulumiwa tu. Na by the way umedhulumiwa nini na wewe umewajibikaje kwenye dhuluma hiyo?

we cheki,
kuna vibaraka vimbelembele mara kadhaa wameenda kubweka bweka hadi kwa mabwenyenye wanaowafadhili huko ng'ambo, ati Tanzania kuna uvunjifu na dhuluma kwa haki za binadamu. Kitu ambacho ni uongo wa mchana kweupe kabisa.

matokeo yake hao vibaraka mabwenyenye wenyewe hususani wa magharibi walipokuja kushuhudia hizo dhuluma, hawakuona kitu. Infact wakabaini kwamba huko kwao ndiko hasa kuna matatizo makubwa, watu wa huko wangelalamika na kuandamana kudhulumiwa haki zao kuliko Tanzania ambapo Tanzania ni kisiwa cha amani hakuna mambo kama hayo.

Rais na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, ameendelea kua lulu ya amani Tanzania na ndie champion wa kulinda na kutetea haki za binadamu Tanzania, Africa Mashariki, Africa na duniani kote, na ndio maana Majeshi yetu yametapakaa maeneo mbalimbali duniani kulinda haki za binadamu na Amani 🐒
 
Mh! Makusudi tu wanafanya kwani unadhani hawajui kuongoza? Nchi hii achilia mbali elimu, ukiwa mpenda haki tu unaiongoza vizuri kabisa na kwenye msiba wako tunatandika vitenge upite.
 
Hii Serikali ya kijinga Sana. Kuna jambo nimeligindua ndio maa nasema hivyo.
Gentleman,
mwerevu anaejiamini, mwenye mawazo mapya na fikra mbadala juu ya jambo Fulani, anaeleza jambo hilo kinagaubaga kwa weledi, umahiri na ungwana wa kiwango cha juu sana, na sio kuibuka na mihemko ama ghadhabu ambazo kimsingi hazina maana yoyote kwa wadau 🐒
 
Civil services ambao ni ulinzi wa nchi na wa sio wa mzaha kabisa kwenye ascendency. Na sina shika wa succession planning yao.
Tuwe wakweli mkuu, civil service ya Tanzania ilishakuwa compromised mno. Ndiyo hao hutumika kuiba kura ili kuweka madarakani watawala kwa ushindi batili.

Kutarajia uadilifu wowote kutoka kwa watu wa hivyo ni kujidanganya.
This is not accident (hii inaonyesha pia ni kwamba civil ni weak) kukubali kuachia raisi ateuwe watu anavyojisikia.
Watafanya nini? Wanaweza kuzuia au kukosoa?
Kama mkuu wa mhimili Ndugai alifanya kazi yake halali ya kukosoa akafurushwa upesi, kuna mwingine anaweza?

Kwa mfumo uliopo sasa, hakuna chochote wanachoweza kufanya ila uchawa tu.

Ndiyo maana wenye hekima wanadai mabadiliko ya Katiba
 
Huko wala usijali waziri wa mambo ya nje kwa sasa, ni mtaalamu.

Lakini Samia akili hana, lazima tukubaliane kwenye hilo watanzania.

Kafikaje hapo halipo MaCCM yanajua yenyewe succession planning. Mimi binafsi siwezi kukaa kikao ata cha mtaa kitachoongozwa na Samia.

Huyu mtu Kafikaje hapo na Generał Mabeyo kabisa aliwapinga watu apewe nchi is beyond me.

Samia akili hana, huo ni ukweli usiopingika.
Daah,
Chawa Lucas Mwashambwa na msaidizi wake Tlaatlaah wachukue notes hapa
 
Back
Top Bottom