Nina swali hapo.
Hio kauli ulioiandika humu JF.ili kujua Bongo hamna FREEDOM OF SPEECH/ uhuru wa habari.
Mimi hili halinihusu video si inajieleza hapo alisema mwenyewe au hujatazama video.
Ukiisema hio kauli hadharani utajikuta porini katavi.
Watateka watu wangapi?
Edgar walimteka na kumtupa Katavi ila leo hii yupo na anazungumza yale yale na ukweli kuhusu utekaji.
Pia tangu wamteke Edgar je Samia ndio alipendwa na watu wote mdau??
Ngoja nikupe mifano mitatu ili ujue kuteka /kuua sio suluhu ya watu unaopishana nao mawazo.
Nakurudisha darasa la historia pengine hutopenda kuisikia .
1.Nyerere aliyeitwa baba wa demokrasia hakuwa mtu aliyependa mawazo mbadala alifanya ushawishu muswada wa nchi kuwa ya chama kimoja 1963 na hadi 1965 muswada ulipita na Tanzania ikawa rasmi taifa la chama kimoja kisheria , Nyerere akaingia katika uchaguzi mkuu wa kiini macho kama huu wa CCM matokeo kwenye karatasi ni picha [ndio ] kivuli [hapana] mwisho wa siku matokeo yalikuwa hivi.
Kura za ndio 2,410,903 sawa na asilimia 96.46
Kura za hapana ni 88,600 sawa na asilimia 3.54 .
Hapo ni funzo kuwa licha ya Nyere kutaka nchi iwe ya chama kimoja bado sio wote walimkubali kisera akaishia kupata hapa 3.54 % na pia hata huo uhalali wa 96.46 ungeweza kupungua zaidi kama asingejipa mamlaka ya kuwa na chama kimoja kihalali kisheria.
Nyerere katika awamu miaka yake yote ya utawala tangu kuzaliwa Tanzania hajawahi kupitia uchaguzi wa vyama vingi ila bado haikuzuia watu kumpinga mwishoni ndio akawa mkosoaji wa demokrasia huku akimkosoa Mwinyi hadi kumuandika katika kitabu jinsi anavyoendesha serikali huyu dakika za mwisho ndio akageuka "champion" wa kuhamasisha vyama vingi vya siasa kurudishwa.
2.Joseph Mobutu huyu alimiliki kila kitu hadi kubadilisha jina la nchi , viwanja , miji bila utaratibu maalum huyu upigaji kura ulikuwa ni wazi uchague ndio au hapana alijimilikisha kila kitu hadi kujenga kasri na uwanja wa ndege kijijini kwao .
Kwa nguvu na mauaji aliyofanya Mobutu kule kwao ni alikojenga sasa ni magofu na hakuweza hata kuzikwa kwao bali alizikwa Morocco.
3.Iddi Amin huyu alijipa vyeo vikubwa vya kijeshi na alikuwa ni mtu wa kauli moja licha ya mauaji na utekaji wake kujilimbikizia mali huyu nae hakufanikiwa kuzikwa kwake na alipofariki waligomewa asizikwe Uganda mwisho wa siku alizikwa Saudi Arabia.
Mimi sio mwandishi mzuri sana ila nimekupa mifano michache uone jibsi gani madaraka ni kitu cha kupita na kuua,kuteka,kutesa hakukufanyi upendwe na watu wote au watu wote wawe na mawazo sawa na wewe.
Je CEO wa JF ametuhakikishia ulinzi, sio polisi wakamuhitaji mwa JF alietoa kauli fulani. Akatolewa?
Wao wasihangaike na Max walimsumbua Max miaka ile sana wao wenyewe humo una uhakika wanapenda yanayoendelea au ni uniform na viapo ndio vinawabana .
Kama unabisha itisha opinion poll za wazi kuhusu Samia humu na hata moja ipo jukwaa hili kaone matokeo utabaki na mshangao.
Mimi nimetishiwa awamu ile na ID 3 hivi enzi za jiwe hawa watu leo hii wamebadili ID ila ndio vinara wa kumponda Samia , jibu silijui ni kwanini huenda walinufaika na utawala ule na sasa huu nao huyu kaja na wake.