Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia

Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza raisi Samia.

Bora nikalime huko, kuliko kupokea orders kutoka kwake.

Hana uwezo hata chembe.

That says a lot ueledi wa civil services,

It’s a shitty county (ndio uhalisia).
Haulazimishwi kumsikiliza. Rais Samia yupo hadi 2030. Wabunge pia watafanya kitu kwenye katiba aendelee hadi 2035 kwa sababu ndo hitaji kubwa la wananchi walio wengi kwa sasa.
 
Haulazimishwi kumsikiliza. Rais Samia yupo hadi 2030. Wabunge pia watafanya kitu kwenye katiba aendelee hadi 2035 kwa sababu ndo hitaji kubwa la wananchi walio wengi kwa sasa.
Ama kweli mlamba asali huchonga mzinga.
 
Jambo la kwanza ni kuzingatia mtoa hoja ambae ameamua kuacha kumskiliza mtu na akaamua bora akalime. Mbona hakusema au kuamua kwenda kufanya kazi nyingine ispokua kilimo?

Hata hivyo,
nimefurahi mno kwa namna ulivyohoji mageuzi na mapinduzi ya kilimo ambayo kwa kiasi kikubwa yamechochewa sana katika awamu hii ya6 chini ya Rais na kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan.

Gentleman,
hakuna tena kilimo cha mkono nyakati hizi, wala hakuna ule mtindo wa kupanda kwa kumwaga mbegu, tena zisizo za kisasa.

matrekta na mashine maalumu za kupandia, mbolea, dawa na mbegu za kisasa za mazao mbalimbali ndio kwa kiasi kukubwa hutumika..

na kwa namna mambo yanavyokwenda, suala la njaa Tanzania litakua ni ndoto.

Nadhani nisitoe ushuhuda wowote but mabadliko ya kilimo nchini yamesaidia kuikimbiza njaa mbali sana na kuongeza kipato cha waTanzania kwa kiasi kikubwa mno 🐒
 
Mkuu, Tanzania ni nchi ya kistratejia zaidi katika ukanda huu wa maziwa makuu na Afrika Mashariki na kati.

Remote ipo mahala hivyo hakuna kitu kama unachofikiria kitawahi kuja kutokea.

Wafuatiliaji wenzangu wa geopolitics watanielewa.
 
Hebu washawishi watu kama hilo unaloandika ni sahihi ukitoa na sababu za kusema hivyo.

Maana nyakati za kuaminisha watu jambo bila kusema hayo mapungufu ili watu wapime wenyewe zimepita kitambo sana.
 
Sawa.

Bado yapo mambo mengi ya kuyarekebisha.

Mshaurini raisi afungue njia zaidi kwa graduate wapate ajira au mitaji ya kujiajiri.

Pia human rights records zinaharibu sifa zote unozielezea hapa.

Mie ntafanya judgement kipindi cha serikali yake halisi endapo atashinda uchaguzi ujao.

Bila shaka hata weye una nafasi yako tayari umeahidiwa.

Au?
 
Mimi nitawa laumu wote lakini wa mwisho atakuwa ni the late.. Msiniulize kivipi!
 
Weka ushahidi wa kutosha dhidi ya hizi shutuma zako. Sawa una uhuru wa maoni lakn bila ya hoja unaonekana mtovu wa nidhani.
 
Anamaanisha ilikuwaje mifumo haikubaini from the grassroots kama hakustahili kuwa hata running mate.

Hakustahili hata kuwa waziri
 
Kiongozi kwa Tanzania ndio mmiliki wa nchi kama Baba alivyomiliki wa Familia.

Nchi ni muunganiko wa familia, vijiji, mikoa , makabila, dini, kanda mbalimbali tofauti. Ili changamoto zitatuliwe zinahitaji ushirikano wa pamoja wa wote.

Ili kupata maoni sahihi ya wananchi wananchi wanahitaji kuchagua wwawakilishi wanaowaamini, sio kuchaguliwa wawakilishi na Rais.

Ni makosa makubwa kuendesha nchi kama familia yako binafsi.
 
Wawakilishi wa wananchi, wabunge, watumishi wa umma, mawaziri, Rais walitakiwa kupata hizo nafasi sababu wana vigezo, meritocracy ni wako competent. Sio sababu ni ndugu, rafiki wa kiongozi, yupo CCM au ni tajiri.
 
sure,
bado kuna yapo mengi yafaa kurekebishwa na kuboreshwa zaid hususan elimu ya kilimo cha kisasa.
Na wizara husika inafanya kazi kubwa sana kwenye hili.

Rais, mkuu wa nchi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan anashauriwa vizuri sana kwenye sekta ya kilimo na hata kufikia hatua ya kuanzishwa na kuipa mtaji benki ya kilimo.

Graduate wanayo fursa za ajira bwerere na ya wazi sana kwenye sekta ya kilimo iliyoboershwa sana. Zaidi sana wana fursa kwenye ufugaji, biashara, usafirishaji n.k.

lakini pia wanayo fursa ya wazi kabisa ya kiuchumi, kwani katika kila halmashauri nchini, kuna kuna fedha za mikopo kwajili ya vijana. waungane na kwenda kuchukua mikopo hiyo na kujiendeleza kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Tanzania tunaheshimu haki za binadamu mno ukilinganisha na nchi yoyote Africa Mashariki na Africa kwa ujumla. Nchi yetu haiko katika viwango vya uvunjifu wa haki za binadamu na ndiyo maana ulimwengu mzima unajua kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani na upendo.

Hata hivyo,
Ifahamike duniani kote, yeyote atakae jaribu kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wananchi Tanzania atashughikiwa kwa nguvu zote, kwani Amani ya waTanzania italindwa kwa nguvu gharama zote bila mbambamba ya nchi yoyote ya kigeni au kibaraka wao yeyote humu nchini.

Mimi ni kiongozi wa wananchi na ni raia mwema mzalendo wa Taifa hili, mchapakazi nisiestahili kupewa chochote bali furaha na amani yangu ni kuona wananchi wanapata mahitaji yao muhimu kwa kujitosheleza 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…