Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
🙋♂️✍️🎯🤝🙏Ukisema akili hana nadhani si kauli sahihi kwani yeye ndie first citizen, hivyo heshima ni ya kulazimika nadhani labda useme mawazo yake yametekwa.
Kuna jamaa humu alileta mada inohusu state capture kaongelea namna state inavyoweza kuwa chini ya watu fulani ambao ndo wenye maamuzi.
Kisha mie pia kuna mada humu niliongelea kuhusu madhara ya nchi kuruhusu mfumo wa Kleptokrasia ambao pia ni mfumo unokuwa chini ya watu wachache na viongozi ambao huiba na kujilimbikizia mali za taifa.
Hivyo hata kama hyupoo kiongozi ambae amefumbwa na mifumo kama hiyo si kwamba hana akili ila huwaza namna ya kuchomoka lakini bado ana kuwa limited ni maamuzi yepi yatatimizwa au kuzimwa na mifumo hiyo.
Kwa bahati mbaya yaonekana nchi yetu imekumbwa na mifumo yote miwili yaani "double knock factors".