Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo na uchaguzi mkuu wa 2025 unashauri tusifanye uchaguzi wa Rais kwa kua matokeo tayari unayajua!!??Chama chako ccm huwa kinavuruga uchaguzi ili kishinde.Wewe jiandikishe,nenda kapige kura.
With all due respect Mh waziri,hii hoja yako ni yenye faida kwa mwanaccm tu.Kwa makusudi wenye mamlaka walivuruga uchaguzi wa 2019,na ule wa 2020.Labda mtu ajiandikishe kwa lengo la kupata ktambulisho tu,ila si lengo la kupiga kura.Unapigaje kura huku mamlaka zimeshapanga matokeo?.Ni ujinga na kupoteza muda.
Katiba ya Tanzania inakuruhusu kua huru!!Mimi na familia yangu nakuunga mkono kwa mengi ila kwa hili hapana Dr.
Anafanya Jambo zuri Sana Sanaa jamii forums Kuna material mengi Sanaa.Waziri pekee aliye karibu na wananchi kupitia JF.
Hv wale mawaziri wengine wanapatikana wapi
tupeni mitandao yao tusafate huko
Naungq mkono hojq nq hii ianzie kwenye vyama wakati wa kura za maoniHongereni ila washauri viongozi wenzako wenye dhamana ya kusimamia uchaguzi watende haki ,nchi inatumia fedha nyingi sana kwenye uchaguzi kuanzia uandikishaji hadi upigaji kura ,matendo ya kuiba kura au kuaanda kura za maruhani mapema ni bora kusifanyike uchaguzi muwe mnajichagua wenyewe ili hizo fedha ziende kutumika kwenye huduma za jamii.
Mwenyewe nataka kwenda kujiandikisha,nawaza hilo foleni, kama Mama Samia tu kapanga foleni huko Dodoma,mimi ni nani nisipange foleni!![emoji113]Ngoja na mimi nikajiandikishe hivyohivyo
Wwe nenda kokote mwisho wa siku utarudi na utatukuta!!Hongera, mimi siwezi kujiandikisha wala kupoteza muda wangu kupiga kura. Nampango wa kuzamia Australia bongo bahati mbaya.
Usiongee maneno matupu,lete data na achaa blaablaa!!Mh Waziri najua huna namna ila ukweli unaujua.
Nikiri wazi mwaka 2015 nilisimama sana na JPM naomba niseme sana..na ni mtu ambae niliamini at least anaweza kupush baadhi ya vitu kwenye huu mfumo mbovu tulionao..nashukuru kafanya mambo mengi mazuri ila mambo mawili ambayo nilimdharau ni issue ya Covid-19 ambayo wewe binafsi pamoja na elimu yako ulifanya vituko sana huku ukiona watu wakiteketea ule ulikuwa ni Unyama sijui kama unajua.....la pili kuvuruga Uchaguzi wa 2020 hili liliathiri na litaathiri Taifa kwa kipindi kirefu sana...nikuhakikishie it is very Tough to fix it penda usipende...Muda utaongea.
Ni hayo tu.
Kama kujiandikisha mpaka ufuatwe kupiga kura itakuaje?Samaleko mheshimiwa sana
tunaomba muwe na utaratibu wa kuandikisha watu kwa kuwafuata katika maeneo yao ya kazi kama mnavofanya kwenye sensa vinginevyo % kubwa ya watu hawatojiandikisha nikiwemo mimi
Nawasilisha
Kwani ww na familia yako mkijuandikisha ndio sisi tunahamasika? Hatuwezi kuendelea kushiriki chaguzi za kihuni zinazowafanya ccm mkae madarakani kwa shuruti.Leo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.
Hatua hii ni kufuatia uzinduzi rasmi kitaifa wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa uliofanywa tarehe 11 Oktoba , 2024 huko Chamwino, Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
PONGEZI kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo Ndugu Robert Ally Massawe kwa maandalizi mazuri ya utaratibu wa kujiandikisha na wepesi na umahiri wa maafisa waandikishaji kwenye kutoa huduma husika.
Mimi na familia yangu tunawahamasisha watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye serikali za mitaa yao zoezi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba, 2024.
Viongozi wenye sifa za kutumikia jamii ni matokeo ya kura yako mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura hivyo, jitokeze jiandikishe. Mimi na familia yangu, tayari tumetimiza wajibu wetu.
Tunawatakia uandikishaji na uboreshaji mwema wa taarifa zenu kwenye daftari husika.
MWISHO.
View attachment 3121584View attachment 3121585View attachment 3121586View attachment 3121587View attachment 3121588View attachment 3121589
View attachment 3121590
Na wwe pika chai,achana na ready-made!!Muda huu napiga ghahawa kitu cha kapuchinoo....huku nayajenga
Mipango yangu,siyo ukaniweke foleni kama wanataka waje nyumbani kwangu waniandikishe
[emoji1]
Ova
Wote wako humu na mafake ID, wanajua wakiingia na ID zao, watakutana na hasira ya umma.Waziri pekee aliye karibu na wananchi kupitia JF.
Hv wale mawaziri wengine wanapatikana wapi
tupeni mitandao yao tusafate huko
Hata wakija kama sensa tutawaambia kabisa hatuko tayari kushiriki chaguzi za kuhuni.Wangetufuata kama sensa. Ila sawa tutaenda weekend.
Yaani kwa kifupi anamaanisha.kila kitu kifanyike online, kama vile unavyo fanya miamala ukiwa uko home kwako! Sasa ila ukitaka cash [emoji389] lazima uifute kwa wakala au Bank!!Kama kujiandikisha mpaka ufuatwe kupiga kura itakuaje?
Boksi la kura liwekwe kwenye junctions zote Tanzania?
Huku kwetu vijijini hakuna foleniMwenyewe nataka kwenda kujiandikisha,nawaza hilo foleni, kama Mama Samia tu kapanga foleni huko Dodoma,mimi ni nani nisipange foleni!![emoji113]
Dr Doroth nasmini umekuwa sasa umeacha kumnyanyasa mumeo .......maana kajamaa kamevumilia aseee khaaaaLeo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.