Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Nafikiri watu wengi wanapotosha hiyo maana ya 50/50 ndio maana kunakuwa na huu mkanganyiko wote, 50/50 haina maana kwamba mwanamke amtawale mwanaume, bali maana yake ni kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na wa kumtawala mwenzake yani
 

Sasa kama majukumu ya nyumbani hayana mchango wowote katika maendeleo yenu kwanini wanaume wengi huwa wanaoa ili wafanyiwe hayo majukumu, yani kuna wanaume wake zao wasipofanya hayo majukumu huwa wanachukia seriously kabisa na wanaweza hata kuwarudisha makwao, utasikia mtu anasema kabisa "acha nioe nimechoka kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba nk, na vipi kuhusu suala la kulea watoto nalo mbona hujaliongelea ilihali mgawanyo wa mali kwa asilimia kubwa huzingatia kwamba mwanamke ndiye mlezi wa watoto tangu wakiwa wadogo


Kama ulimaanisha mahari basi kaa ukijua mahari haihusiani kabisa na majukumu anayoenda kufanya mwanamke kwenye ndoa labda nikurekebishe hapo mahari ni kama shukurani na fidia kwa wazazi wa mke, kwa sababu mwanamke anapoolewa familia yake inahesabika imelose while ya mwanaume imegain kwa maana kwamba mke ataenda kuendeleza ukoo wa mume na watoto watatumia majina ya ukoo wa mume, na ndio maana kwenye jamii nyingi wanaopokea hiyo mahari ni wazazi na ndugu wa mwanamke na si mwanamke mwenyewe kwa sababu ni familia yake ndio inahesabika imepoteza hapo

Lakini

3.

Vipi kama nilikuwa mtu wa huruma nisiyependa kukuona ukihangaika na hivyo kuamua kutafuta mfanyakazi wa kukusaidia?

Bado utaendelea kudai 50/50 ya mali kwenye kazi ambazo hufanyi wewe??

Ni wanaume wangapi wanaoweka wafanyakazi bila kutaka wake zao nao wafanye hizo kazi, ningekuelewa kama ungesema ukiweka huyo mfanyakazi basi yeye ndio anatakiwa afanye kazi zote na siyo tena uanze kumuuliza mkeo kwanini hamsaidii mfanyakazi, lakini wanaume wengi wakiona hivyo wanaanza tena malalamiko kwamba mke kajisahau kamuachia kila kitu mfanyakazi na matokeo yake wanaanza kutembea na hao wadada wa kazi kwa hiko kisingizio


Yeah 100% katika scenario kama hiyo basi mwanaume ana haki zote za kudai 50/50 katika mali zote za mke wake


Hapana wanawake wanasitasita kwa sababu mnataka kwenye hiyo 50/50 wakubali majukumu tu ila haki wasipewe au wapewe kidogo, mwanamke kutafuta pesa na mali zake siyo shida shida ni pale ambapo mwanaume bado anataka heshima na utii na kutimiziwa majukumu ya nyumbani kutoka kwa huyo huyo mwanamke anayejitafutia vya kwake, na huo ndio utapeli wenyewe ninaousema


Aliyekuambia kwamba course za ukomandoo zinatofautiana mafunzo baina ya wanaume na wanawake ni nani na ni jeshi gani linalofanya hivyo, suala la kuvunja mawe kwa kichwa hilo wanajua viongozi kwanini hawawapangi wanawake nao wafanye hilo zoezi lakini si kwamba duniani hakuna wanawake wanaoweza kuvunja mawe kwa kichwa, huko kwenye course za ukomando hata wanaume wapo wengi wanaoshindwa kufuzu sasa kwanini ionekane kama vile mwanamke kushindwa kufuzu ni kwa sababu ya jinsia yake tu na si kwa sababu nyinginezo ambazo zinafanya na baadhi ya wanaume nao wasifuzu


Mkuu unatofautishaje na unatafsiri vipi jukumu gumu na jukumu rahisi kwa sababu mimi ninavyojua ugumu au urahisi wa jukumu unategemea na mtu binafsi maana naona umekomaa kuyaita hayo majukumu "vitu simple", hayo majukumu unayoona wewe marahisi kuna watu wanaona ni magumu na hawataki kuyafanya na unayoona wewe ni magumu kuna watu wanaona ni marahisi na wanapenda kuyafanya, hayo majukumu ya nyumbani unayoona rahisi wanaume wengi wanayaona magumu na wako radhi hata washinde shambani wanalima siku nzima kuliko kuyafanya hayo kwa mfano shughuli ya kulea mtoto mchanga kuna mwanaume atakayekubali kuifanya
 
Ushoga ulikuwepo toka enzi za Sodoma na Gomora kipindi cha mfumo dume mkuu
 
Nafikiri watu wengi wanapotosha hiyo maana ya 50/50 ndio maana kunakuwa na huu mkanganyiko wote, 50/50 haina maana kwamba mwanamke amtawale mwanaume, bali maana yake ni kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na wa kumtawala mwenzake yani
Ukifuata nadharia za nchi za magharibi wanataka kuwe na mambo ambayo ni kinyume na maelekezo ya Mungu kupitia 50/50. Inatakiwa kuwa makini sana. Kiuhalisia 50/50 imevuka mipaka na imetumika vibaya kupitisha mambo yasiyo ya kawaida ikiwemo ushoga.
 
Hata akikuzidi kimo ,utajuta.
 
Wanaume hawaoi kwa ajili ya kufanyiwa hizo kazi.

Wanaoa kwasababu wanataka familia.

Na hizo kazi sio kitu cha kumsumbua mwanaume kwa miaka hii ambayo digital imetawala.

Kama kufua alikuwa anaweza kuwapa nguo madobi wamfulie akawalipa, akawa ameokoa gharama za sabuni na maji.

Angeweza kununua washing machine akawa anafua bila tabu yeyote.

Angeweza kununua hata dish washer akawa anaosha vyombo bila usumbufu wowote.

Angeshindwa kabisa angeweza kumuajiri dada wa kazi ambaye angekuwa anafanya hizo kazi tena kwa malipo nafuu kabisa.
 
Kama ulimaanisha mahari basi kaa ukijua mahari haihusiani kabisa na majukumu anayoenda kufanya mwanamke kwenye ndoa labda nikurekebishe hapo mahari ni kama shukurani na fidia kwa wazazi wa mke
Shukurani hiyo mbona wewe hujaitoa kwa wazazi wangu?

Kwamba wazazi wangu hawastahili shukurani au ni kudharau walicho kizaa kuwa hakistahili kupewa shukurani?
 
Sio kweli kuwa familia ya mwanamke inakuwa ime lose.

Mwanaume ndio anaye lose

Kwasababu mwanaume akioa anakuwa amebeba majukumu yanayohusu familia yake, majukumu ya wazazi wake hadi familia ya wazazi wa mke wake.

Kutumia jina la ukoo hakuna maana kumetokana na malipo ya mali.

Kutumia jina la mume la ukoo ni kutokana na kuweka usawa katika umiliki wa mtoto.

Mama ndio mtu pekee ambaye akizaa mtoto anakuwa wake kwa 100%. Lakini kwa mume hilo kuna walakini inawezekana akawa amesingiziwa

So ili ku balance ndio ikawekwa hiyo principle
 
Kama kufua anafua msaidizi, kupika anapika yeye, usafi wote ni yeye.

Hiyo sehemu ambayo unataka huyo mfanyakazi afanye usafi unataka aingie chumbani kwako?

Yani malalamiko yako sio tena wingi wa kazi bali hutaki kazi yeyote bila kujali udogo wake?

Kazi ya kufagia chumbani kwako ndio hiyo ambayo inakufanya udai 50/50 mkiachana?
 
Na nyie kwenye sera ya 50/50 mbona focus yenu mmeiwekea mambo ya kimaslahi lakini hamjawahi kudai haki za kupambana na majambazi kama hizi??

Sisi tunawaona nyinyi kama wanyonyaji mnaotumia sera ya 50/50 kama fursa ya kutuibia mali zetu, kwasababu tunaona kwenye mambo magumu hiyo sera hamuiongei
 
Dunia inahitaji Equity sio Equality ,mkilitambua hili basi mtaondoa huu upumbavu wenu kichwani.

Yule superpower ,the father of democracy nchi yake na purukushani za kidunia hajawahi kumpa mwanamke aongoze.

Ni mjinga anaweza kukubali usawa wakati hata vikojoleo vipo tofauti
 
Ukomandoo wa mwanamke hauwezi kuwa sawa na komandoo wa kiume.

Yapo mazoezi ambayo wanashare kama ABT ambayo yanatolewa kwenye level ya chini ya regular army.

Mwanaume aliyeshindwa kufuzu kwenye ukomandoo ni kutokana na intensity ya hayo mafunzo yalivyokuwa magumu.

Na mwanamke aliyefuzu mafunzo ya ukomandoo haina maana amefuzu hayo mafunzo ambayo huyo mwanaume amefeli.

Ni tofauti kabisa.
 
Tofautisha kuyaona magumu kwasababu ni magumu na kuyaona magumu kwasababu ni mvivu.
 
Ukifuata nadharia za nchi za magharibi wanataka kuwe na mambo ambayo ni kinyume na maelekezo ya Mungu kupitia 50/50. Inatakiwa kuwa makini sana. Kiuhalisia 50/50 imevuka mipaka na imetumika vibaya kupitisha mambo yasiyo ya kawaida ikiwemo ushoga.
Mkuu sijui kwanini unakazania hili suala la ushoga kama vile ni jambo geni duniani, ushoga ulikuwepo toka enzi za Sodoma na Gomora ambako kulikuwa na mfumo dume, maovu yote haya tunayoyaona yalikuwepo toka enzi za mfumo dume huo mfumo ulifanya nini kuzuia maovu hayo
 

Wewe sasa naona unaleta nadharia kwenye uhalisia hawa wanaume tunaowaona kila siku wanasema wanaoa ili wake zao wawafanyie kazi za nyumbani ni wa wapi, hao wanaume unaosema wananunua hizo mashine za kusimplify kazi au wanawalipa watu wafanye hizo kazi ni wangapi kulinganisha na hawa ambao hadi leo wanaona hayo mambo ni anasa na wengine wanadai hawawezi kuafford, kuna mwanaume hadi leo anawaza kupelekewa maji ya kuoga bafuni na akiambiwa aweke bomba anakuambia sasa nimeoa mke wa kazi gani au labda nikuulize wewe unaweza kukubali kulipa watu wafanye hizo kazi ilihali una mke nyumbani

Shukurani hiyo mbona wewe hujaitoa kwa wazazi wangu?

Kwamba wazazi wangu hawastahili shukurani au ni kudharau walicho kizaa kuwa hakistahili kupewa shukurani?

Ndio maana ya mfumo dume, ukitaka mahari itolewe basi kubali 50/50, hiyo ni shukurani ya familia ya mke kumtoa mtoto wao kwa familia ya mume


Hapana familia ya mke ndio inakuwa imelose kwa sababu kwa kawaida kwenye tamaduni nyingi, mwanamke akishaondoka kwao huwa hatakiwi kuwatembelea wazazi au ndugu zake mara kwa mara, lakini kwa mwanaume ni tofauti yeye wazazi na ndugu zake hata wakitaka kuja kuishi hapo kwake inaonekana sawa tu

Na mwanamke mara nyingi huwa anashiriki kwenye shughuli za upande wa mume kuliko anavyoshiriki kwenye shughuli za kwao, na wakati mwingine mume anaweza hata kumuambia mke akamuuguze mama yake mzazi akiumwa, hivyo ni haki kabisa familia ya mume kuhudumia familia ya mke yani hapo inakuwa ni kama exchange ya huduma

Kuhusu majina ya ukoo sidhani kama baba kutokuwa na uhakika na umiliki wa watoto inahusiana na watoto kutokutumia jina la ukoo la mke, kwa sababu kwa tamaduni za afrika mtoto kutumia jina la ukoo ni heshima kwa upande wa mwanaume kwamba watoto wanaendeleza jina linakuwa halifi hivyo kwa familia ya mke hiyo ni loss, na ndio maana kwenye makabila mengi wababa walikuwa wanachukia kuwa na watoto wa kike wengi kuliko wa kiume sababu kubwa ni hiyo


Sasa kama wewe na mke wako wote mnafanya kazi na wote mnawahi kuondoka na mnachelewa kurudi ni kipi kinachofanya mwanamke aweze kufanya usafi wa chumbani kwenu ambacho wewe kinakufanya ushindwe, na ndio maana nikasema mnaposema kazi ni rahisi mnatakiwa mjiulize kwanini ninyi mnashindwa kuzifanya na kutegemea mke ndio azifanye kila wakati, halafu siyo usafi wa chumbani tu wanaume wengi hata hizo kazi za kupika na kufua bado hawataki mahousegirl wafanye wanataka wake zao ndio wafanye wanadai hawawezi kula chakula cha housegirl wakati mke yupo

Kwenye theory ndio, ila uhalisia hilo jambo halipo kabisa

Halipo kwa sababu hata hao wanaume uliowatolea mfano kwamba wanafanya kazi za nyumbani kisa wake zao wanatafuta pesa hawapo, wanaume hawawezi kukubali kufanya kazi za nyumbani eti kisa tu wake zao wanatafuta pesa watawaambia watafute wadada wa kazi, na pia wanaume bado huwa wanataka kupewa heshima na utii hata katika scenario kama hiyo ambayo mke ndio anatafuta pesa na kuhudumia nyumba


Ndio maana nikakuambia mnataka tuongelee kwenye mambo magumu ambayo they are not likely to happen in daily life hizo ni uncertainties tu, 50/50 siyo sera ya kuwaibia mali ndio maana nikasema mgawanyo wa mali mara nyingi huzingatia kwamba ni either mmechuma wote au mwanamke ndiye anayelea watoto, sidhani kama mwanamke anaweza akagawiwa mali za mwanaume nusu ikiwa siyo katika mazingira kama hayo


Mimi sijui unaongelea jeshi gani mkuu lakini ninachojua ni kwamba mafunzo yote huwa ni sawa hayatenganishwi, halafu kitendo cha wanawake kujaribu tu tayari wameonesha uthubutu suala la kufuzu au kutokufuzu hayo ni matokeo tu kama ambavyo wapo wanaume wanaoshindwa kufuzu, ingekuwa ni suala kama wanawake wangekuwa hawajaribu kabisa ila wapo wengi sana wanaojaribu ila ndio hivyo kufuzu ni matokeo tu

Tofautisha kuyaona magumu kwasababu ni magumu na kuyaona magumu kwasababu ni mvivu.
Oohh kwahiyo wanaume wanapokataa kufanya kazi za nyumbani na kulea watoto maana yake ni wavivu siyo
 
Km mnahusiana, bas jua mnaoana, na sio kuoa wala kuolewa.

Hisia za sex kwa mumewe, sio mchumba, km ambavyo wee utampa huduma na mahitaji mkeo.

Hukimbiiii hapa.
 
Nakupendea hapo tyuuh dada angu, [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…