Wanaume hawaoi kwa ajili ya kufanyiwa hizo kazi.
Wanaoa kwasababu wanataka familia.
Na hizo kazi sio kitu cha kumsumbua mwanaume kwa miaka hii ambayo digital imetawala.
Kama kufua alikuwa anaweza kuwapa nguo madobi wamfulie akawalipa, akawa ameokoa gharama za sabuni na maji.
Angeweza kununua washing machine akawa anafua bila tabu yeyote.
Angeweza kununua hata dish washer akawa anaosha vyombo bila usumbufu wowote.
Angeshindwa kabisa angeweza kumuajiri dada wa kazi ambaye angekuwa anafanya hizo kazi tena kwa malipo nafuu kabisa.
Wewe sasa naona unaleta nadharia kwenye uhalisia hawa wanaume tunaowaona kila siku wanasema wanaoa ili wake zao wawafanyie kazi za nyumbani ni wa wapi, hao wanaume unaosema wananunua hizo mashine za kusimplify kazi au wanawalipa watu wafanye hizo kazi ni wangapi kulinganisha na hawa ambao hadi leo wanaona hayo mambo ni anasa na wengine wanadai hawawezi kuafford, kuna mwanaume hadi leo anawaza kupelekewa maji ya kuoga bafuni na akiambiwa aweke bomba anakuambia sasa nimeoa mke wa kazi gani au labda nikuulize wewe unaweza kukubali kulipa watu wafanye hizo kazi ilihali una mke nyumbani
Shukurani hiyo mbona wewe hujaitoa kwa wazazi wangu?
Kwamba wazazi wangu hawastahili shukurani au ni kudharau walicho kizaa kuwa hakistahili kupewa shukurani?
Ndio maana ya mfumo dume, ukitaka mahari itolewe basi kubali 50/50, hiyo ni shukurani ya familia ya mke kumtoa mtoto wao kwa familia ya mume
Sio kweli kuwa familia ya mwanamke inakuwa ime lose.
Mwanaume ndio anaye lose
Kwasababu mwanaume akioa anakuwa amebeba majukumu yanayohusu familia yake, majukumu ya wazazi wake hadi familia ya wazazi wa mke wake.
Kutumia jina la ukoo hakuna maana kumetokana na malipo ya mali.
Kutumia jina la mume la ukoo ni kutokana na kuweka usawa katika umiliki wa mtoto.
Mama ndio mtu pekee ambaye akizaa mtoto anakuwa wake kwa 100%. Lakini kwa mume hilo kuna walakini inawezekana akawa amesingiziwa
So ili ku balance ndio ikawekwa hiyo principle
Hapana familia ya mke ndio inakuwa imelose kwa sababu kwa kawaida kwenye tamaduni nyingi, mwanamke akishaondoka kwao huwa hatakiwi kuwatembelea wazazi au ndugu zake mara kwa mara, lakini kwa mwanaume ni tofauti yeye wazazi na ndugu zake hata wakitaka kuja kuishi hapo kwake inaonekana sawa tu
Na mwanamke mara nyingi huwa anashiriki kwenye shughuli za upande wa mume kuliko anavyoshiriki kwenye shughuli za kwao, na wakati mwingine mume anaweza hata kumuambia mke akamuuguze mama yake mzazi akiumwa, hivyo ni haki kabisa familia ya mume kuhudumia familia ya mke yani hapo inakuwa ni kama exchange ya huduma
Kuhusu majina ya ukoo sidhani kama baba kutokuwa na uhakika na umiliki wa watoto inahusiana na watoto kutokutumia jina la ukoo la mke, kwa sababu kwa tamaduni za afrika mtoto kutumia jina la ukoo ni heshima kwa upande wa mwanaume kwamba watoto wanaendeleza jina linakuwa halifi hivyo kwa familia ya mke hiyo ni loss, na ndio maana kwenye makabila mengi wababa walikuwa wanachukia kuwa na watoto wa kike wengi kuliko wa kiume sababu kubwa ni hiyo
Kama kufua anafua msaidizi, kupika anapika yeye, usafi wote ni yeye.
Hiyo sehemu ambayo unataka huyo mfanyakazi afanye usafi unataka aingie chumbani kwako?
Yani malalamiko yako sio tena wingi wa kazi bali hutaki kazi yeyote bila kujali udogo wake?
Kazi ya kufagia chumbani kwako ndio hiyo ambayo inakufanya udai 50/50 mkiachana?
Sasa kama wewe na mke wako wote mnafanya kazi na wote mnawahi kuondoka na mnachelewa kurudi ni kipi kinachofanya mwanamke aweze kufanya usafi wa chumbani kwenu ambacho wewe kinakufanya ushindwe, na ndio maana nikasema mnaposema kazi ni rahisi mnatakiwa mjiulize kwanini ninyi mnashindwa kuzifanya na kutegemea mke ndio azifanye kila wakati, halafu siyo usafi wa chumbani tu wanaume wengi hata hizo kazi za kupika na kufua bado hawataki mahousegirl wafanye wanataka wake zao ndio wafanye wanadai hawawezi kula chakula cha housegirl wakati mke yupo
Kwenye theory ndio, ila uhalisia hilo jambo halipo kabisa
Halipo kwa sababu hata hao wanaume uliowatolea mfano kwamba wanafanya kazi za nyumbani kisa wake zao wanatafuta pesa hawapo, wanaume hawawezi kukubali kufanya kazi za nyumbani eti kisa tu wake zao wanatafuta pesa watawaambia watafute wadada wa kazi, na pia wanaume bado huwa wanataka kupewa heshima na utii hata katika scenario kama hiyo ambayo mke ndio anatafuta pesa na kuhudumia nyumba
Na nyie kwenye sera ya 50/50 mbona focus yenu mmeiwekea mambo ya kimaslahi lakini hamjawahi kudai haki za kupambana na majambazi kama hizi??
Sisi tunawaona nyinyi kama wanyonyaji mnaotumia sera ya 50/50 kama fursa ya kutuibia mali zetu, kwasababu tunaona kwenye mambo magumu hiyo sera hamuiongei
Ndio maana nikakuambia mnataka tuongelee kwenye mambo magumu ambayo they are not likely to happen in daily life hizo ni uncertainties tu, 50/50 siyo sera ya kuwaibia mali ndio maana nikasema mgawanyo wa mali mara nyingi huzingatia kwamba ni either mmechuma wote au mwanamke ndiye anayelea watoto, sidhani kama mwanamke anaweza akagawiwa mali za mwanaume nusu ikiwa siyo katika mazingira kama hayo
Ukomandoo wa mwanamke hauwezi kuwa sawa na komandoo wa kiume.
Yapo mazoezi ambayo wanashare kama ABT ambayo yanatolewa kwenye level ya chini ya regular army.
Mwanaume aliyeshindwa kufuzu kwenye ukomandoo ni kutokana na intensity ya hayo mafunzo yalivyokuwa magumu.
Na mwanamke aliyefuzu mafunzo ya ukomandoo haina maana amefuzu hayo mafunzo ambayo huyo mwanaume amefeli.
Ni tofauti kabisa.
Mimi sijui unaongelea jeshi gani mkuu lakini ninachojua ni kwamba mafunzo yote huwa ni sawa hayatenganishwi, halafu kitendo cha wanawake kujaribu tu tayari wameonesha uthubutu suala la kufuzu au kutokufuzu hayo ni matokeo tu kama ambavyo wapo wanaume wanaoshindwa kufuzu, ingekuwa ni suala kama wanawake wangekuwa hawajaribu kabisa ila wapo wengi sana wanaojaribu ila ndio hivyo kufuzu ni matokeo tu
Tofautisha kuyaona magumu kwasababu ni magumu na kuyaona magumu kwasababu ni mvivu.
Oohh kwahiyo wanaume wanapokataa kufanya kazi za nyumbani na kulea watoto maana yake ni wavivu siyo