Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Wapinzani walishatoboa siku nyingi sana, tatizo CCM mnaiba kura sana, bila kuiba hata wabunge wawili hampati
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi"

Chanzo: Darmpya
Yaani Simba na Yanga wakae kupanga waamuzi wa mechi yao? UJINGA GANI HUU!
Inaelekea hatujui tunataka nini?
Nikiwasikiliza naona kama tunataka TUME SHIRIKISHI na huo ndio utakao kuwa mwisho wa TUME HURU.
 
Wapinzani walishatoboa siku nyingi sana, tatizo CCM mnaiba kura sana, bila kuiba hata wabunge wawili hampati
Mkuu wapiga kura wengi wapo vijijini, na huko vijijini huwaambii kitu kuhusu CCM na kura nyingi huwa wanazoa huko. Huku mijini wazee wa hoya hoya nyingi na kuchangamsha mikutano
 
Ingependeza zaidi kama haya mazungumzo vingeshiriki vyama vyote
 
Nimemsikia MZEE PINDA akisema Tuanze Mchakato wa TUME HURU YA UCHAGUZI
Binafsi NAPINGA kwa NGUVU ZOTE
WATANZANIA Tunataka Tukamilishe RASIMU ya KATIBA ya WARIOBA KWANZA kisha ndio Itafuata TUME HURU ya UCHAGUZI.
RASIMU ya WARIOBA imekwisha tumia MABILIONI ya KODI za WANANCHI bila KUKAMILISHWA Mchakato.
Tuanze na KATIBA MPYA kisha TUME HURU ya UCHAGUZI

JamiiForums1376280645.jpg
 
Narudia kutamka Tena

Naipenda sana CCM!
CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu Sana!
CCM inao Makada werevu Sana!

KaziIendelee
Endeleeni kujadili!
 
Hivi huyu pinda,yale mashamba yake ya zabibu huwa analipa kodi stahiki kweli?tuanzie hapo
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa

Wakati mwingine mnajiweka kwenye mazingira ya mivutano isiyo na tija kwa kuondekeza mambo yasiyo na maana. Inatakiwa katiba mpya ambayo ni full package na tume huru ya uchaguzi humo humo. Lakini mnakalia ukiritimba usio na tija, kisha mkiambiwa mnajivuta mnasema tunabeza. Kwa hiyo umekaa unasubiri mpaka kiongozi aseme ndio uone kafanya la maana, hivyo aungwe mkono. Tukikuuliza sababu ya kujivuta ni nini huna, ila unataka siku hao viongozi wakijisikia basi waungwe mkono hata kama wanazingua.
 
Endeleeni kushupaza shingo, hamjifunzi, huku kushupaza shingo kwenu ndiyo kulisababisha tukose katiba mpya 2014
Usilie wala kulaumu kwa kunyimwa pombe!
Inawezekana ungekunywa sumu ukafa!
Tumeagizwa Tushukuru kwa Yooote!!!
 
Huwezi kujadili swala la tume huru kabla hatujazungumzia mamlaka ya uteuzi aliyonayo raisi.

Sababu raisi ndio amepewa mamlaka ya kuteuwa nani awepo katika katiba mpya plush raisi ndie anaamua huyo raia afanye nini na nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh!! Hata shetani akizeeka anakuwa Malaika......

Halafu Pinda ukimrudisha madarakani leo, hayo maneno atayakana mchana kweupe.

Hata Mama Samia siku akitoka madarakani utasikia tumechelewa sana kupata katiba mpya.
Kwa umri huo au malezi yalumumba
 
Mh!! Hata shetani akizeeka anakuwa Malaika......

Halafu Pinda ukimrudisha madarakani leo, hayo maneno atayakana mchana kweupe.

Hata Mama Samia siku akitoka madarakani utasikia tumechelewa sana kupata katiba mpya.
Kunja mtumishi wa ikulu enzi za Mchonga ....[emoji854]
 
Tukipata Tume HURU hata tunaweza kuifanyia marekebisho Katiba hihii hii halafu tukaingia kwenye Uchaguzi mkuu.

Huko mbele ndio tutaibadilisha Katiba.
 
Endeleeni kushupaza shingo, hamjifunzi, huku kushupaza shingo kwenu ndiyo kulisababisha tukose katiba mpya 2014

Wala haikukosekana kwa sababu ya kushupaza shingo kwani katiba pendekezwa iliyochakachuliwa na wahuni ipo, na inangoja kura ya maoni. Ila kwakuwa wewe ni bendera fuata upepo ukisikia Ukawa ndio waliokwamisha katiba unarukia humo humo.
 
Back
Top Bottom