Nsikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.
Takribani visiku kadhaa humu ndani kuna kampeni za watu kadhaa ambao wamekuwa wakipinga suala la kuoana(Ndoa).
Nimejaribu kupitia nyuzi kadhaa nikaona wameainisha sababu zao na uenda zikawa za msingi(kwao) na kwangu zisiwe za msingi vilevile.Pengine watu hawa hadi kufikia kuona mahusiano ya mke na mume(Ndoa)kuwa kitu kisichofaa yawezekana kabisa wengi wao wamewahi kuwa kwenye Ndoa na kutoka na sintofahamu wakaamua kujiengua na ndiyo maana wamekuwa wakipiga kelele na kutoa tahadhari kana kwamba kuna bomu la nyuklia linakwenda kupigwa na kusababisha maafa muda mchache ujao.
Sidhani kama hujawahi kuingia kwenye ndoa ukawa na uhalali wa kupaza sauti na kushupalia jambo ambalo hujawahi kulifanya na hujui ubaya na wema wake,bila shaka wote wanaopinga ndoa ni majeruhi wa ndoa zenyewe.
Mimi kama
UMUGHAKA sipingani nao kwakuwa huo ndiyo mtizamo wao na mwenzio anapotoa mtizamo wake bila shaka amekaa chini akatafakari na alichowasilisha huwa kina mantiki.
My take.
Kama leo tunapinga suala la ndoa kwa nguvu zote naomba hizo nguvu pia zitumike kupinga suala la Uzinzi na Uasherati.
Suala la kupinga ndoa maana yake ni kwamba Huwezi kuishi na Mwanamke/Mwanaume kwa kifupi mwanamke/mwanaume hakupaswa kuwepo duniani,sasa nadhani hapa tuliweke hili suala vizuri,tupinge ndoa lakini pia tupinge uzinzi na uasherati.
Haiwezekani humtaki mwanamke/mwanaume kwenye jambo la ndoa halafu ukamtaka huyo huyo mwanamke/mwanaume akupe papuchi/mkuyenge mnapokutana huko vichochoroni,hili halikubariki!.
Ukiamua kukataa ndoa kataa kabisa na suala la Uzinzi na Uasherati.Siyo leo upinge suala la ndoa halafu kesho tukukute pale kitambaa cheupe unamshika Joyce matako huku ukiwa umembambia kinoma noma.
Suala la ndoa linahusu mwanaume na mwanamke,na vilevile suala la uzinzi/uasherati linahusu Mwanaume na mwanamke,hivyo hakuna sababu ya kumkataa mwanamke halafu tukuone unafanya uzinzi wa waziwazi.
UKIAMUA KUKATAA NDOA KATAA NA MAMBO YANAYOMHUSU MWANAMKE/MWANAUME.
SIYO UKATAE NDOA HALAFU UENDELEE NA UZINZI/UASHERATI.
Ni hayo tu.