Kwanza mtu yeyote anayepinga ndoa awe mwanamke au mwanaume basi huyo ni wakala wa shetani hilo halina mjadala.
Mtu yeyote akikwambia eti usioe au usiolewe hata kama ni rafiki yako au ndugu yako basi kuanzia siku hiyo mhesabu kama shetani na adui wa maisha yako kwa sababu mtu anaye kushauri kuwa usioe au usiolewe ina maana ana kushauri kuwa mzinzi na ukisha kuwa mzinzi tiyari ww ni adui wa Mungu.
Ukitaka kuishi maisha yanayo mpendeza mungu ndoa haiepukiki maana mbadala wa ndoa ni uzinzi kwa sababu binadamu hauwezi kuishi bila kufanya ngono.
Kuoa ni dhihirisho la mamlaka ya mwanaume hapa duniani sasa ww mwanaume unaanzaje kukataa kuowa?
Watu wana sema eti ndoa za siku hizi ni pasua kichwa lakini ukichunguza ni zimekuwa pasua kichwa kwasabau jamii imeendekeza uzinzi ,matatizo mengi ndani ya ndoa kwa sasa haya sababishwi na kingine zaidi ya wanandoa kuendekeza uzinzi hata wawapo ndani ya ndoa, ni mara chache kukuta ndoa ina mgogoro inayo husiana na Mambo mengine nje ya wanandoa kutuhumiana juu ya usariti ndani ya ndoa.
Halafu kingine matatizo hayapo kwenye mahusiano ya kindoa tu hata huko kwenye mahusiano yenu ya kinzinzi yamejaa tele. Kwani mara ngapi hapa tumesikia vijana wanajiuwa kisa kuachwa na mademu zao? au mbona kuna vijana kibao wanauwa mademu zao kisa amegundua ana mwanaume mwingine? ina maana pia hata kwenye mahusiano yasiyo ya kindoa bado uzinzi ni tatizo? Kiufupi uzinzi ni sumu kwenye mahusiano yeyote yale.
Kwa maelezo yangu utagundua kuwa uzinzi ndo saratani ndani ya jamii yetu na si ndoa, ina maana jamii yetu ikiamuwa kudhibiti na kuacha kuhusudu uzinzi wa kiholela basi kwa kiasi kikubwa migogoro ndani ya ndoa itapungua sana.
Haya ni baadhi ya madhara ya jamii kuendekeza uzinzi.
(1)Kumeleta rundo la watoto wasio na baba.
(2)Umeshabisha rundo la single mother mitaani.
(3)Umeshababisha rundo la magonjwa ya ajabu ajabu.
(4)Umeshababisha kiwango cha kuheshimiana ndani ya jamii kimeshuka.
(4)Umeshabisha migogoro kwenye ndoa na kusababisha watoto kuteseka hasa baada ya wanandoa kuachana kwa sababu ya uzinzi.
Usikatae ndoa bali kataa uzinzi.
Kataa uzinzi, kataa uzinzi, kataa uzinzi.