TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Utoto ni nini na ukubwa ni nini ndugu?
Kutoa kwa ajili ya kizazi kijacho.
Hii tabia tulitakiwa tuwe nayo tangu utoto na tungeenda nayo hadi ukubwani.
Ila tabia ambayo tunayo ni ile utoe ili unufaike. Na hiki ndicho kimesababisha hadi leo bukoba ipo nyuma.
Akili nyingi huondoa maalifa. Mmejenga mashule mengi Dar kwa easy payback.
Je mngejenga Bukoba mjini ingekuwaje?no easy payback
 
Tuanze sasa, inawezekana[emoji4]
 
Sisi tuna nyumba pale mtaa wa uswahilini.
Ni ya late bibi.nimejaribu kuwashauli Mama zetu ambao ni warithi watuachie sisi watoto wao. Tuijenge iwe ya kisasa na vizazi vyetu baadae nao kila likizo wawe na sehemu nzuri ya kufikia. Nimegonga mwamba.
Wamepiga hesabu zao nani kabaki bk na kuna ambaye anahitaji kurudi bk kati yao.wameamua kuiuza. Kwa kuwa wao wapo Dar na majumba mazuri they dont care.
Imagine utajili tuliouweka nje ungekuwa pale town Bk ingekuwaje?
Elimu imetuharibu.
Ndio maana mchaga ambae hana elimu ya mzungu akibahatisha town anainvest kwao.
Now Moshi pana heshima sio only ya mashule bali pia uwekezaji ukilinganisha na sisi ambao tunaongoza kuwa na civilized elimu ya mzungu.
Ningeshauli ipite kwanza elimu ya kujua uthamini wa nyumbani kwanza
 
Tuna akili sana. Hicho ndicho kitakacho tukwamisha.
 
NAPAZA SAUTI!!

Naomba sauti hii iwafikie wajeolojia waliokuja mkoani kufatilia tetemeko la ardhi lakini pia Wakala wa Jeolojia TZ.

Ziwa victoria kwa muda mrefu sasa limekua likisogea nchi kavu taratibu na kufikia kumega sehemu kubwa ya nchi kavu. Hali hii si salama kwa maana kuna majengo yamekwisha ondoshwa na maji na mengine si salama kwa kuishi hasa yaliyoko pembezoni mwa ziwa.

Hali hii inashuhudiwa katika picha zifuatazo zilizopigwa eneo la Spice Beach na eneo la wazi kati ya Spice Beach na Bukoba Cooperative Hotel zamani Yasira.

Tungependa kujua inakadiriwa maji yatafikia sehemu gani ya mji, kwa muda gani na tahadhari zinazoweza kuchukuliwa kabla ya hali ya hatari kujitokeza. Kwasababu kuna uwekezaji na miradi mbali mbali inaendelea ndani ya mji ni vyema taarifa na elimu juu ya hiki kinachotokea kutolewa mapema na kuhakikisha zinawafikia watu wengi zaidi kama si wote


 
UTATU ULIOBARIKIWA!!



Ndugu Alex ambaye ni katibu wa mbunge, Bi Rahel ambaye ni mchumi wa BMC na afisa habari wa JF-Tushirikishane (mpiga picha) katika kikao kidogo cha kupitia mpango-kazi wa Tushirikishane Bukoba. Kikao hiki kilifanyika juzi tar 14-10-2016

Utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane unahusisha taasisi tatu ambazo ni Jamiiforums, Mbunge na Bukoba Manispaa.

Vipaumbele vyetu ni;

1. Ujenzi wa Soko Kuu, Soko la Kashai na Stand kuu ya Mabasi

2. Urasimishaji Makazi

3. Mikopo kwa Vijana na kina Mama, na

4. Bima ya Afya

Vipaumbele hivi ndivyo tutakua tukijadili zaidi na kutoa ripoti ya hatua zinazofikiwa kila wiki na ripoti ya jumla kwa kila mwezi na hatimaye ripoti ya mwisho ya mradi.

Usiache kufatilia


Bwana atuwezeshe[emoji120]
 
RASILIMALI MFU KATIKATI YA MJI WA BUKOBA (CBD)



Haya ni majengo ya kihistoria (monuments) yanayoelezea historia ya mji wa Bukoba. Majengo haya yana hadhi sana na mejengo mengine ya kihistoria kama yaliyoko Stone Town, Bagamoyo, Kilwa na kwingineko. Pamoja na kuwa majengo haya ni muhimu kihistoria lakini pia ni vivutio vya kitalii na kitafiti. Majengo haya yanapaswa kuwa chini ya idara ya Antiquity-Wizara ya Maliasili na utalii, yanapaswa kutunzwa, kurekebishwa bila kupoteza asili yake na pia kutangazwa ili wazawa wafahamu na pia kuvutia watalii.

Majengo haya yamepakana na ofisi ya mkuu wa mkoa na mbunge. Yapo majengo mengine ya yenye hadhi sawa na haya katika Bukoba manispaa




Jengo hili ambalo linamilikiwa na CCM pia ni rasilimali mfu. Jengo hili linatumika kama tuition center[emoji85] kama shughuli yake maalum. Nalo limepakana na ofisi ya mkuu wa mkoa
 
UKARABATI



Ukarabati wa barabara ya Kastamu, eneo la Kasarani ukiendelea. Barabara hii iliathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 September. Ukarabati huu ni moja kati ya jitihada za serikali kuhakikisha miundombinu na taasisi za umma zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi zinarejea katika matumizi yake ya awali
 
HISTORIA

Hili ndilo jengo lililopata umaarufu sana kuliko majengo yote ya mkoa wa Kagera. Jengo hili linafahamika kwa jina na "Duka kubwa". Duka kubwa ni jengo la kwanza la kisasa katika mkoa wa Kagera ambalo lilijengwa na wajerumani. Jengo hili lilikua likitumika kama supermarket.

Kanisa la Bunena ndilo lilikua la kwanza kujengwa huku Duka Kubwa likifuata. Duka Kubwa lilikamilika ujenzi wake kabla ya kanisa la Bunena hivyo kuwa jengo la kwanza la kisasa mkoani Kagera.

 
HISTORIA

Anaandika mzee Ramadhan Kingi

Baada ya Mwalimi J.K. Nyerere kufika Bukoba 1957, Watawala waingereza walihakikisha hakuna nyumba yoyote ya Wageni kumpokea ama kumpa nafasi ya kulala. Wenyeji wake walikwishaijua hii harakati.
Mzee Sued Kagasheki aliamua Mwalimu afikie kwake mjini mtaa wa Uhuru. Wazungu wakalifahamu hilo. Mzee Sued alikwishapanga plan b Mzee Sued aliiweka siri hiyo moyoni. Ilipofika saa Sued alimhamishia nyumba yake ya Rwamishenye na Mwalimu akaweza kupumzika raha mustarehe



Maoni;
Nyumba hii inapaswa kutunzwa na kuwèkwa kwenye kumbukumbu ya kihistoria kama zilivyo nyumba nyingine ambazo alifiki/aliishi Baba wa Taifa kwaajili ya vizazi vijavyo
 
Tumuombe mbunge wetu awasiliane na Twaha Taslima kuhusu uhuwishaji wa bandari ya Kemondo katika kusafirisha mizigo kuanzia Kemondo
Reli ya Kati( standard gauge iwe mpaka Mwanza halafu meli ya MV. Umoja isafirishe hadi Kemondo!
Reli kwenda Kigali na Burundi na mizigo kwenda kwa Barbara hadi ya Uganda.Haya ndio mapendekezo ya EAC ya 1977
 
Isaka ni ghali kwani uwezo wa meli ya mizigo ni konteina za futi 40 Umoja ilikuwa ni kontena 40. Semi trela moja hubeba kontena moja. Pia kwa maji bukoba hadi port bell Uganda ni karibu ukitokea kemondo.Pia Kisumu ni karibu ukitokea bukoba kuliko kutokea Mz. Isaka ni bandari ya nchi kavu ambayo iko pale kwa maslahi ya watu binafsi.
 
KUMBUKUMBU YA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU BUKOBA

Mwaka 1966 Bukoba kulikuwa na timu iliitwa "Bulwark" ilianzishwa na Sheikh Fadhil na mmoja wa wachezaji wake mahiri ni Alhaj Profesa Issa Kaboko Musoke! Makao Makuu ya timu hiyo ni mkabala name TTCL kwa Al almarhum Juma Mwanandege.

Timu nyingine maarufu ilikua ni Balimi miaka ya 1970. Timu hii ilifanya vizuri, iliweza kuunganisha vijana wengi na baadhi ya wachezaji waliweza kushika nyazifa mbali mbali za kiutawala baadae



Picha inayofuata[emoji116] ilikua ni mechi kati ya Balimi na Simba. Wageni wa heshima walikua ni Marehemu Mzee Juma Suedi na Marehemu Meya wa mji Mzee Rugusha. Marehemu Juma Suedi alikua Mwenyekiti wa FAT Kagera.
Katika mechi hiyo Simba walilazwa goli moja kwa sifuri uwanja wa Kaitaba kwa shuti kali kutoka mguuni mwa Adallah.



Baadhi ya wachezaji wa Balimi ni Kayumbe, Burchard, Adallah, Goalkeeper na 11, Mar. Abubakar Kulewa, Juma Mhina, Mkuya, Juma Kikwemu, Abdulgaddy, Alhaj Sheikh Haruna Kichwabuta (Sheikh wa Mkoa-Kiongozi), Ishebo, Coach Catanasio,
Ramadhani Kingi, Alhaj Dr. Abdallah Mporokosh, Morris Mapalala, Leopold "Tasso" Mukebezi Saleh Jordan Moyo, Elias Robert, Mar.Kasabo na Salum Mawingo.

Wengine ni Mar. Nurdin, Mikidadi, Masoud Said el-Khusaiby, Mutimba, Boniphace, Lubega ama Kato, Godfrey, Mar. Juma Manyara, Ruhinda, Hussein Kingi, simkumbuki jina, linesman Mar. Mzee Sudi Brandes Badru Nsubuga, Alhaj Juma Suedi Kagasheki, Nuru Suedi Kagasheki, kyebijuna, George Kyangenyenka, Paul Tosi, Tadeo, cyprian, Shariff na Libenti Oyogya.

Source: Mzee Ramadhan Kingi
 
Hivi ndivyo jinsi majengo ya Soko Kuu yatakavyofanana juu ya ardhi



Ujenzi wa Soko Kuu ni kipaumbele namba moja katika mradi wa Tushirikishane. Hii inatikana na ukweli kwamba katika vitu ambavyo wanaBukoba wanahamu sana ya kuona vikifanyika ni ujenzi wa Soko
 


Huo[emoji115] ni mwonekano wa ndani wa stand mpya ya mabasi itakayojengwa eneo la Kyakailabwa.



[emoji115] Mwonekano wa nje wa stand mpya ya mabasi ya kyakailabwa
 
Reactions: MC7
Ujenzi wa stend ukikamilika itakuwa vizuri sana kwa kukuza utalii maana sasa watalii wengi wanaokuja kwa bus wakifika stend ya Bukoba wanashangaa ilivyo na mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya.
Mkoa WA Kagera umejaliwa kuwa na vivutio vingi sana vya utalii tembelea website ya www.kageratourism.com kujionea.

KAGERA TOURISM | Home
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…