KUMBUKUMBU YA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU BUKOBA
Mwaka 1966 Bukoba kulikuwa na timu iliitwa "Bulwark" ilianzishwa na Sheikh Fadhil na mmoja wa wachezaji wake mahiri ni Alhaj Profesa Issa Kaboko Musoke! Makao Makuu ya timu hiyo ni mkabala name TTCL kwa Al almarhum Juma Mwanandege.
Timu nyingine maarufu ilikua ni Balimi miaka ya 1970. Timu hii ilifanya vizuri, iliweza kuunganisha vijana wengi na baadhi ya wachezaji waliweza kushika nyazifa mbali mbali za kiutawala baadae
Picha inayofuata[emoji116] ilikua ni mechi kati ya Balimi na Simba. Wageni wa heshima walikua ni Marehemu Mzee Juma Suedi na Marehemu Meya wa mji Mzee Rugusha. Marehemu Juma Suedi alikua Mwenyekiti wa FAT Kagera.
Katika mechi hiyo Simba walilazwa goli moja kwa sifuri uwanja wa Kaitaba kwa shuti kali kutoka mguuni mwa Adallah.
Baadhi ya wachezaji wa Balimi ni Kayumbe, Burchard, Adallah, Goalkeeper na 11, Mar. Abubakar Kulewa, Juma Mhina, Mkuya, Juma Kikwemu, Abdulgaddy, Alhaj Sheikh Haruna Kichwabuta (Sheikh wa Mkoa-Kiongozi), Ishebo, Coach Catanasio,
Ramadhani Kingi, Alhaj Dr. Abdallah Mporokosh, Morris Mapalala, Leopold "Tasso" Mukebezi Saleh Jordan Moyo, Elias Robert, Mar.Kasabo na Salum Mawingo.
Wengine ni Mar. Nurdin, Mikidadi, Masoud Said el-Khusaiby, Mutimba, Boniphace, Lubega ama Kato, Godfrey, Mar. Juma Manyara, Ruhinda, Hussein Kingi, simkumbuki jina, linesman Mar. Mzee Sudi Brandes Badru Nsubuga, Alhaj Juma Suedi Kagasheki, Nuru Suedi Kagasheki, kyebijuna, George Kyangenyenka, Paul Tosi, Tadeo, cyprian, Shariff na Libenti Oyogya.
Source: Mzee Ramadhan Kingi