Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli


Buduma za afya kwenye emergency inabidi ziwe bure kwa Watanzania,wote.
 
Sijapinga mengine uliyosema kwenye post yako. Ila naangalia uhalali wa wewe kumlaumu dereva kwa gari kukosa mafuta. Tuseme ambulance ni ya serikali, unafikiri dereva akiamua tu kuinunulia mafuta, ambayo kawaida anayapatia GPSA hiyo pesa yake nani atamrudishia? Najaribu tu kumtoa dereva kwenye lawama.
 
Tutatoa za rambi tambi kufidia kifoo chake na hayo mafuta
 
Ni wakati wa sisi wananchi kuambiana ukweli afya, elimu na chakula na mengineyo ni jukumu letu kila mmoja binafsi cha bure hewa tu. Haiwezekani mimba tangu ina mwezi mmoja hadi tisa hauweki akiba ya fedha hata kidogo ukitegemea upewe kila kitu bure! Vituo vya afya vijijini bado vinachangamoto nyingi, ambazo serikali imeweza kufanya pakubwa.
Wanasiasa nao wawaambie ukweli wananchi wao! sisi ni dunia ya tatu' kiuchumi bado tunajitafuta, watu wafanye kazi kwa bidii na wapange uzazi kuweza kumudu gharama za maisha wasije kuishia kulaumu magoli ya mama ambayo yanatengeneza morali ya kujituma zaidi kwa wachezaji wetu itakayokuja kupelekea ajira nyingi zaidi kwa vijana ikiwa mpira wetu utauzika nje ya nchi.
 
du ipo shida mahali na nahisi kabisa watu wanakula kwasababu ya shida za watu
 
mh!
 
labda sielewi utaratibu wa serikali kwani mtu hawezi kudaiwa baada ya huduma..??
 
Sidhani kama mfano wako unaendana na hali halisi, sera ya serikali kwa wamama wanaojifungua inasemaje? Wanalipia gharama ?

Pili wako ni uselfish wa ajabu, kumbuka yuko kijijini na kuna zahanati pale na je tunatakiwa kuweka hela ya mafuta ya gari kwenye taasisi za serikali ambayo inakusanya kodi?

Ni rahisi mwananchi wa kijijini kuwa na sh 180,000/ ? Acheni roho za kichawi kama wewe ni rahisi kuwa na pesa wahurumie wasiokuwa nazo usiwalaumu wala kuwaona hawana akili kwa kukosa hela huo ni ulimbukeni na ushamba
 
Mama akinunua magari shida asiponunua ndo hayaa sasa
 
Sijui kiungo gani unatumia kufikiria, bila aibu mwananchi wa kijijini unadai achangie sh 189k, tena unasema kirahisi tu Δ·wa sababu wewe unazo.
Je sera ya serikali inasemaje kwa wanaojifungua wachangie mafuta huko vijijini? Wala rushwa na mafisadi utawajua tu kwa kauli useless kabisa.
 
Baba yako angetumia condom tu, mwananchi wa kijijini anaweza kulipa sh 180,000? Umeona posho wanazolipana maofisa wa serikali?
Umeona magari ya thamani yanayonunuliwa serikali kila mwaka?
Unajua kuna halmashauri huwa zinarudisha pesa serikalini kwa kukosa matumizi?
Unajua wastani wa kipato cha mwananchi wa kijijini?

Ubinafsi wa kichawi huu kushindwa kuwaonea wengine wasio na kipato. Hebu tuambie serikali imefanya juhudi gani za kimkakati ili kuinua maisha ya watanzania vijijini?
 
Inasikitisha sn, kwani hizo ofc zao hazina petty cash? Wanashindwa kuwa hata wazalendo? Naimani alivyofariki hao wafanyakazi wa afya walishiriki msiba wake kwa kuyoa fedha za pole, stupid kabisaaa. Ukishajiona unakinga mkono kila mwisho wa mwezi kutoka serikalini usijione ndio umefika na wenzako ni takataka. Sasa walishindwa hata kuchanga fedha za mafuta hao wafanyakz wa afya?

Lakini kuna maana gani ya kuwa na gari la wagonjwa ambalo halina mafuta? Si bora lisiwepo jamani.

Huyu Raisi anasafiri sana na mambo kibao yasiyonamsingi yanafanyika lakini wananchi wanaopaswa kula keki ya taifa wanakufa kwa sababu hata hiyo keki yenyewe wanatakiwa walipie. Nimesikitika sana kupotrza watu wawili kwa uzembe na ubinafsi.

Hapo kuna watoto either kawaacha wanatunzwa na mwanamke gani wa kuwapenda kama mama aloyewazaa? Nina masikitiko sana jaman kwa kweli, ni huzuni sanaa kwa familia hiyo. Mtafanya uchunguzi lakini hamuwezi kufuta alama ya hiyo familia, na chuki mliyoitengeneza ni kubwa sanaaa.


Kuna haja gani ya kuwa na gari lisilo na mafuta? Machungu mliyotengeneza kwa hiyo familia ni makubwa sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…