Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

Sasa Uchunguzi wa nini hapo? Aliyemwambia atafute hela ya mafuta si yupo? Na ndiye msababishaji?

Uchunguzi wa nini?
 
Ila ujauzito ni mchakato maandalizi ya kujifungua ni muhimu sana hasa kwa wanaume tusiishie kutia mimba tu tuwajibike unakuta jitu linatia mimba tu Kila baada ya miaka miwili hospital akiambiwa achangie japo dawa na vipimo anakuambia Sina pesa inasikitisha sana.

Kuna jamaa mmoja limeoa binti wa watu akampa mimba ikalelewa hivyo hivyo kimagumashi mpaka ikatimiza miez 9 ikatakiwa 350000 ya operation na huduma nyingine bahati nzuri wale ma Dr wa Hospital ya Mwanyamala waliweka mbele ubinadamu wakamzalisha salama yule binti ila wakasema hatoki mpaka pesa ilipwe jamaa anaambiwa na baba Mkwe wake Lete pesa japo kidgo anasema Hana hata Senti yule binti alizuiliwa hospital karibu week 2 ndio baba Mkwe akaingia mfukoni kwake na kutoa 350000 kwa minajiri kwamba Mkwe atamrudushia mpaka Leo mtoto ana miez 11 na pesa jamaa hajamlipa baba Mkwe wake sasa hii sio sawa.
SHIDA waziri husema Bure mjamzito kujifungua
 
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.

Hii hakuna anaye jali kabisa.
Ila ya misafara, safari, kizimkazi, makofia, makanga, pilau, Korea, a
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.

Hii hakuna anaye jali kabisa.
Ila za misafara, safari, kizimkazi, makofia, makanga, sijuwi ujinga gani ZIPO?!
 
Ule mpango wa m-mama haupo nchi zima? Hizi habari zinahitaji kusikia taarifa kutoka pande zote mbili kabla ya kurusha lawama. Huko vijijini watu wana tabia ya kujifungulia nyumbani wakiona hali mbaya ndio wanakwenda kituo cha afya, wakati mwingine wanakuwa wamechelewa sana. Nimewahi kuona kesi ya mjamzito kujifungulia nje ya kituo ndio maana nimewaza hivyo.
Kwa hiyo unataka kusemaje mkuu, hivi hii nchi watumishi wake huwajui?
 
Lini alinunua 🚑 akalaumiwa? weka receipt hapa.

Msipende kuchekecha mijadala.
Mijadala ya ununuzi wa magari ya serikali ipo mingi tu huku do your own research binti, ila yote ya yote ambulance ni nyingi sana sahivi huyo mkuu wa wilaya naye ajieleze kwanini ambulance inakosa mafuta ?
 
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.

Hii hakuna anaye jali kabisa.
Madhara ya kuwa na viongozi wajinga wajinga ndio hayo.
 
Rip kwa aliyefariki ukiacha lawama kwa wenye ambyulensi zao natoa wito kwa wanaume ujauzito ni wa miezi tisa na siku hizi kuna changamoto nyingi wakati wa kujifungua ukilinganisha na miaka ya zamani hvyo tujitahidi kuandaa hata laki tatu iwe pa kuanzia inapofikia siku ya kujifungua tutatue changamoto ndipo tuje kulaumu mifumo vinginevyo hizi lawama baada ya kuwapoteza wapendwa wetu hazisaidii
 
We mjinga zera za CCM wajawaziti na wstoto wa chini ya miaka mitano wanatibiwa bure, hio gari kwani ni ya Private? Dereva si abaliowa kwa kodi zetu, wewe ni mjinga na hapo utakuta ndugu zako wana life gumu sana
Achana na watanzania wapumbavu mkuu, hii nchi inadai wasomi wanaongezeka ila minginga inaongezeka maradufu sijui tatizo lipo wapi? Yeye anashangaa kumlaumu Rais ila hashangai Rais kuwa na mamlaka yote ya kiutawala na kijeshi. Very stupid country
 
Rip kwa aliyefariki ukiacha lawama kwa wenye ambyulensi zao natoa wito kwa wanaume ujauzito ni wa miezi tisa na siku hizi kuna changamoto nyingi wakati wa kujifungua ukilinganisha na miaka ya zamani hvyo tujitahidi kuandaa hata laki tatu iwe pa kuanzia inapofikia siku ya kujifungua tutatue changamoto ndipo tuje kulaumu mifumo vinginevyo hizi lawama baada ya kuwapoteza wapendwa wetu hazisaidii
Nyie watanzania mnajua hali za huko kijijini lakini?
 
Sasa Uchunguzi wa nini hapo? Aliyemwambia atafute hela ya mafuta si yupo? Na ndiye msababishaji?

Uchunguzi wa nini?
Wapate kupiga pesa zingine kwenye tume na kamati zao, pia muda utakuwa umepita na wananchi kama kawaida yao watakuwa wameisha sahau na hasira zimepungua.

Halafu life as usual
 
Ule mpango wa m-mama haupo nchi zima? Hizi habari zinahitaji kusikia taarifa kutoka pande zote mbili kabla ya kurusha lawama. Huko vijijini watu wana tabia ya kujifungulia nyumbani wakiona hali mbaya ndio wanakwenda kituo cha afya, wakati mwingine wanakuwa wamechelewa sana. Nimewahi kuona kesi ya mjamzito kujifungulia nje ya kituo ndio maana nimewaza hivyo.
Pitia tena bandiko halafu uje utetee vizuri. Kaambiwa atoe hela ya mafuta sh 180,000/ uligwa?
Usitumie hisia zako mkuu tujasili hoja
 
Kuna mbunge wa huyo mama kuna mkuu wa wilaya anayotoka huyo mama, kuna mkuu wa mkoa. kuna serikali nzima kabla hujamhusisha SSH.

Wote hao wanahusika na wanawajibika kumsaidia huyo mama. Kuna zahanati zinazojengwa kwa pesa za kodi na huko Morogoro zipo nyingi tu.

Magoli yatanunuliwa tu kwani Simba na Yanga ni walipa kodi wakubwa kuliko taasisi nyingi zilizopo nchini. Wanao mchango mkubwa wa kukuza jina la Tanzania kimataifa.

Kila wanapofuzu makundi au robo fainali kuna pesa nyingi wanazoingiza kwenye akaunti za vilabu vyao na kuna kodi nyingi inayoingia serikali kuu.

Serikali haiwezi kumsaidia moja kwa moja kila mwanamke mjamzito, tupunguze hizi nongwa za kipuuzi.
Tatizo la makada wa Chama cha hovyo kifo cha mtanzania kwako si muhimu. Eti serikali haiwezi kumsaidia moja kwa moja kila mwanamke mjamzito, hoja ya kipumbavu mno ya nyie wa mama anaupiga mwingi.

Msimamizi wa katiba na serikali ni yeye, anauewateua na kuwasimamia anaowateua ni yeye, yule baba chijachinja aliyeondoka kwa ukali wake kulikuwa na upumbavu huu?

Watu wanatekwa na kuuliwa anasema ni drama, watumishi wa serikali anayoiongoza muhimu ni kuhakikisha wanabaki madarakani tu, na yeye Ndio maana anatoa hela kwenye magoli ali apate kuungwa mkono wa wapenzi wa Yanga na Simba.

Hili huwezi kumtrnganisha na uzembe huu labda uwe kiboyo kama nyie kijana wa hovyo
 
Fuata kwanza wahusika wa mkoa wake huyo mama. Samia hana uwezo wa kumfikia kila mwanamama mjamzito na kutatua matatizo yake.
Yeye ndiye tuliyempa dhamana ya uongozi wa taifa letu, yeye atajuana na hao aliwateua.

Unasikia wewe wa mama anaupiga mwingi? Umeandika jina lako lote vizuri umesahau kuweka namaba yako ya simu kama Lucas Mwanshamba unaweza ukapata twuzi
 
Mpuuzi wewe, sitafuti cheo natoa maoni inatosha.
 
Ila ujauzito ni mchakato maandalizi ya kujifungua ni muhimu sana hasa kwa wanaume tusiishie kutia mimba tu tuwajibike unakuta jitu linatia mimba tu Kila baada ya miaka miwili hospital akiambiwa achangie japo dawa na vipimo anakuambia Sina pesa inasikitisha sana.

Kuna jamaa mmoja limeoa binti wa watu akampa mimba ikalelewa hivyo hivyo kimagumashi mpaka ikatimiza miez 9 ikatakiwa 350000 ya operation na huduma nyingine bahati nzuri wale ma Dr wa Hospital ya Mwanyamala waliweka mbele ubinadamu wakamzalisha salama yule binti ila wakasema hatoki mpaka pesa ilipwe jamaa anaambiwa na baba Mkwe wake Lete pesa japo kidgo anasema Hana hata Senti yule binti alizuiliwa hospital karibu week 2 ndio baba Mkwe akaingia mfukoni kwake na kutoa 350000 kwa minajiri kwamba Mkwe atamrudushia mpaka Leo mtoto ana miez 11 na pesa jamaa hajamlipa baba Mkwe wake sasa hii sio sawa.
Walishaambiwa wafyatue tu, huduma ziko bwerere na mapori bado yako makubwa hayana watu na wanyama.
Poor Tanzanians.
 
Kuna magari ya wagonjwa yanasambazwa nchi nzima, mbunge wa eneo hilo alilofariki huyo mama alihangaika kuhakikisha yanakuwepo kwenye wilaya za mkoa wake?.

Kuna mkuu wa wilaya mpaka mkuu wa mkoa wote hao wanahudumiwa na kodi inayolipwa na mwananchi wa kawaida ikiwemo huyo mama aliyeaga dunia, wana wajibu wa kushughulika na shida za wananchi.

Rais Samia ni mamlaka ya juu sana, hana uwezo wa kwenda kila anapokuwa mama mjazito na kumpeleka zahanati akatibiwe, hizi ni akili za kipumbavu sana za kutoelewa mamlaka ya rais yanaanzia wapi na yanaishia wapi.

Michezo ina haki ya kupewa hamasa ili timu zetu zishinde kimataifa, zinaposhinda jina la Tanzania linaendelea kuwa juu siku zote.
 
Back
Top Bottom