Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemkuta hana hatia Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, bilionea Erasto Msuya hivyo ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.
Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wakidaiwa kumuua kwa kumchinja Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.
Miriam na mwenzake Muyella walidaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, imetolewa leo Februari 23, 2024 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Pia soma: