Kuna Afisa mtendaji wa kata aliua mtu kijijini kwetu tena dogo wa miaka 10 alikuwa mchunga, sasa yule afisa kwakuwa shamba lake liliwahi kutiwa mifugo akawa na hasira na wachunga akawa akiwaona anawafukuza ili awashike wakawa wanamkimbia sasa siku ya siku ndipo akamshika huyo dogo akamgeuza kichwa chini miguu juu akawa anamtikisa baadae akamuacha ila wakati huo wenzie waliokimbia wakaja kusimulia kijijini kuwa fulani kashikwa baada ya muda dogo karudi hata kuongea hawezi wakamkimbiza hospital akafariki,,kesi ikaenda mahakamani afisa akashinda kwasababu hakukuwa na ushahidi wa kumtia hatiani...ndugu wakakaa pamoja wakaja kwenye mahakama ya jadi yule jamaa aliumwa sana akaja kuomba radhi kwasababu hospital hauonekani ugonjwa mpaka akaja kufariki kwa mateso sana