Mdondoaji,
..naungana mkono. hoja kwamba Waislamu hawajasoma ni mufilisi.
..hoja kwamba Waislamu hawawezi kusoma pia ni mufilisi.
..I am one of those who believe kwamba Waislamu wakipewa access to a quality education basi wanaweza ku-achieve mambo makubwa.
..Personally nimesoma na Waislamu, and looking back, manake wakati huo tulikuwa hatuulizani dini, kuna vijana wa Kiislamu who were very smart.
..miongoni mwa wa-Tanganyika watatu wa kwanza kupata shahada ya London University ni Abdulrahman Salim Msangi. Ilibidi DC wa wilaya ya Pare wakati huo apande milima ya Usangi kwenda kumpongeza Mzee Salim Msangi kwa achievement ya mwanawe. Later on Abdulrahman Msangi alikuwa dean wa kwanza mzalendo wa kitivo cha Science UDSM.
..now,Prof.Juma Mikidadi Mtupa anafahamika sana tangu akiwa mbunge toka mkoa wa Lindi.
..baada ya kuondoka bungeni akagombea nafasi ya Mufti wa Bakwata na kushindwa. lakini nadhani huyu angewafaa Waislamu.
..tatizo ninaloliona mimi ni kwamba Waislamu wenye elimu ya ki-secular hawashiriki/hawashirikishwi ktk uongozi wa Jumuiya za Kiislamu.
..nadhani kukosekana kwa waumini wenye elimu ya ki-secular ktk taasisi za Kiislamu ndiko kunakosababisha viongozi wa taasisi hizo kutumiwa kisiasa na CCM na kupelekea kuviaibisha vyombo hivyo.
JK,
umenena vizuri sana na sio kuwa hawashiriki bali hawashirikishwi walioko katika Bakwata either ni watu wa system au mamluki. Mfano mzuri aliutoa Faiza siku za nyuma kuwa kulifanyika mabadilko kwa akina mama Bakwata wakatolewa wasomi na kuwekwa watu wanaowajua wao wenyewe wanaopendezwa na system. Why do you think system ina prefer watu hao kuliko waislamu wasomi? Jibu utalipata mwenyewe.