Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini


nakubaliana na wewe mkuu isipokuwa hapo kwenye bold. with due respect, kama kwa khiari yake Dr atapenda kufafanua sawa lakini, from my perspective, naona Huo ufafanuzi watoe wenyewe mashekhe vinginevyo wakanushe kuwa mwanzo hawakuhusika kama A Man of the People Dr Slaa alivyosema. Sisi wala A Man of the People Tusiwasemee Maulamaa. Mashkhe wafafanue kwa nini wao hawakuwa na MoU? Walikataliwa? nani aliwakatalia na aliwapa sababu gani?
 
Mama POROJO ni Mfuasi na shabiki mkubwa wa mtuhumiwa mmojawapo wa wanaotaka kuisambaratisha CHADEMA.Soma post zake za Nyuma.
 
mkuu moshdar.

sina chakuongeza umesimama kwenye mstari wa heri, amani, upendo na umoja (Tanzania na watanzania sio waislamu Vs wakristo) sisi sote ni watanzania tujivunie utanzania wetu (Umoja) sio dini zetu, ukabila wetu au siasa

Tanzania ni yetu tuitunze amani tulionayo kwa maslahi yetu na vizazi vyetu

Sumu ya Mohamed Said isipewe nafasi maana sote tutakuwa wahanga wa machafuko.

bandiko lako mkuu limetulia sana, wenye hekima watakuelewa isipokuwa kwa mshipa wa shetani mtu atashindwa kukuelewa.


 

Ukweli utabakia palepale kwamba serikali ilivyoingia kwenye memorandum ya kutokutaifisha mali za makanisa ilikuwa ni makosa. Utaifshaji ni sera ya taifa, kwa hiyo kama issue ni kulinda utaifishaji ilibidi iwe kwa dini zote na hata wasio kuwa na dini pia. Jambo jengine serkali kama guardian wa raia haikupaswa kutoa upendeleo wowote kwa kundi lolote lile katika jamii. Hizo nyingine ni porojo zako, waislamu tulishajitathmini zamani. Kilichobakia ni serikali kujiondoa kwenye hiyo MoU.
 

Common sense is not common. Niache na uelewa wangu wa kujidhalilisha lakini nawewe ni kuulize kitu kimoja:

Kwanini wakristo mnapinga Tanzania isijiunge na OIC wakati watakaonufailka ni waislamu na wasiokuwa waislamu? Hii si inapingana na hiyo logic yako yu kuuwa wanawake, au unasemaje?
 
kasome kwanza maelezo ya Dr. Slaa ni kwanini palikuwepo na hiyo MOU, halafu uje uzisome vizuri hizo clauses hapo juu...

HATA WEWE AKILI HUNA...UNASUMBULIWA NA NENO "CHURCH" EHHEEE JARIBU KUTAFSIRI SENTENSI NZIMA SIYO NENO MOJA MOJA.

Hizo clause hapo juu mimi nimezielewa kwamba

1) ‘The government shall provide vacancies in its Teachers training colleges for training qualified persons as teachers earmarked for church owned schools’. Article xi

Serikali iwatengee nafasi wakristo kwenye vyuo vya ualimu, walimu ambao baada ya kuhitimu watakwenda kufundisha kwenye shule za makanisa. Sawa sawa au ina maana nyengine?

2) ‘The government shall endeavour to include financial assistance for church run social services in its bilateral negotiations particularly with the Federal Government of Germany. Consideration shall be made during its bilateral negotiations with other donors’. Article xiii.

Serikali ifanye juhudi kuingiza kipengele cha msaada wa kifedha kwenye mapatano yake ya kimataifa, hususan kwa Ujerumani. Pia serikali itilie maanani swala hilo kwa waadhili wengine.

Hayo ya kwamba nina akili au sina namwachia mama yako akufundishe kujadiliana na watu bila matusi.
 

Tunachosema hapa ni kuwa MoU ilitengeneza upendeleo maalum kwa wakristo over and above hizo nafasi za watanzania wengine. Issue sio kufaidika waislamu watupu, kwani kwenye hizo shule za kanisa waislamu wanasoma bure.

Huu ufisadi hautofautiani na ufisadi mwingine ambao unapigwa vita. Inabidi ukomeshwe hata mkijitetea vipi.
 
na kwa vyovyote vile, mimi kama atheist, kama kuna mtu aliwakatalia waislamu kuwa na MoU, no matter ni theist wa mungu yupi, huyo mtu lazima atabeba lawama hata kama ni Mzee wetu, Baba wa Taifa Nyerere, vingenevyo kuwe na sababu-mashiko zitazoonesha kinagaubaga kuwa, thiests wa mungu wa kiislamu kuwa na MoU hiyo kusingewafaidisha wana wa Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla. ikiwa itakuwa hivyo, nitapendekeza mtu huyo tusimkate shingo wala kumtukana, bali tumtake aombe radhi kama yu angali hai na kosa hilo lisahihishwe mara moja.

Katika mambo yanayoniuma sana ni kuona kuna baadhi ya theists wapo kifukara zaidi, kifikra na kimaendeleo, kulinganisha na theists wa upande mwingine. hii ni kwa sababu najua vita vya theists ni vita mbaya, theists ni watu khatari kwa usalama wa sayari hii, ogopa mtu theist anaua theits mwenzake(na hata atheist) ili aende peponi kwa Mungu mtawala na muweza wa yote!

natoa mwito kwa vijana wa kizaz hiki cha "doti komu" tuzikatae fitna na uchochezi huu no matter anachochea nani. hata kama anachochoe mzee wa upako-tukatae, hata kama anachochoe getrude Mogella-tukatae, hata kama anachochea shkhe wa darisalamu-tukatae, hata kama anachochea Pengo-tukatae, hata kama anachochoe sjui m-budha, m-hindu nk nk wa wapi...tuzikatae. TUZIKATAE TUZIKATAE TUZIKATAE TUZIKATE. Vijana woote bila kujali itakidi zetu, dini zetu, ukabila wetu tuwaze kwa pamoja ni vipi tutakabilana na wenzetu wa afrika mashariki ndani ya hilo soko? tukizubaa tutatawaliwa tena mara ya pili tena na wana afrika mashariki wenzetu. ndoto zetu iwe ni kwenda kununua kiwanja cha changombe hukoooo mars, tuwaachie mzee Mohammed Said na Ponda(na hata kina Pengo kama nao wamo) wafitiane na kiwanja cha chang'ombe ya dar...sisi tusikubali kuchinja mama zetu kwa kuchochewa na fikra duni na mfu..HIMA HIMA vijana waafrika wenzangu, wana wa kizazi kipya, wana mapinduzi, wana wazalendo wa Mama yetu Tanzania, wana wa mama wa Afrika kamwe tusikubali kulikata ziwA la mama yetu Afrika kwa kuchochowe na Mzee Mohammed na wengine wa namna yake. tuondokane na UKOLONI, TUSONGE MBELE, Fursa tunazo. changamoto ni zetu tuzikabili pamoja. kamwe tusiwakubali wachonganishi NA wafitini. tukumbuke dini hizi hizi zilitumiwa kutoboa miguu ya babu zetu, kuwafunga kwa minyonyoro na kuwatenda kama wanyama mwitu. Tukumbuke waafrika wenzetu, kama drogba na wenzie, leo na mafanikio yake yote kimichezo na kiutajiri..bado wakoloni wale wale waliotuletea hizi dini wanawadhihaki mchana kweupe bila aibu vijana wenzetu wakiwatupia maganda ya ndizi ikiwa ni dhihaka kwao kuwa yeye drogba bado ni nyani tu na hana lolote. tukumbuke khali hiyo si tofauti uwapo Saudia Arabia.
 

Kaitka hali ya kawaida nategemea wengi wa wakristo watapinga hoja kwamba serikali ilikosea kwa kulipendelea kanisa na kuacha nyuma raia wengine. Ili haya yathibitike, tuiombe serikali izungumzie MoU na fedha ambazo serikali imeshazitoa kwa kugharimia miradi ya kanisa na itoe nafasi kwa waumini wa dini nyingine wachambue hoja za kanisa na serikali katika kuitetea MoU. Otherwise, hatutayamaza kusema kwamba serikali inavyofanya sivyo na athari zake huenda zikawa mbaya.
 
Mkuu mbona hili swala mkuu lynxeffect22 na wengine humu wamekujibu lakini hutaki kuelewa au unataka majibu yatakayo kupendeza unatatizo kubwa sana la udini

Tatizo langu laudini haliwashindi nyie wakristo mnaodhulumu taia wenzenu kwa kutumia MoU kwa kisingizio kwamba na waislamu wanatumia huduma. Lengo ni kila siku waislamu wawategemee wakristo kwenye mashule na mahospitali?
 

Ni sahihi kwa MOU kuwa kati ya Kanisa na Serikali kwa sababu serikali ndiye ilikuwa inataifisha. Na kama umesoma vizuri background ya hii MOU ni kwamba waliokuwa wanatoa msaada yaani Kanisa/serikali ya Ujerumani walitaka assurance kuwa shule au hospitali ambazo wangesaidia hazitatifishwa!

Why? Mwanzo shule, hospitali hizo zilikuwa chini ya kanisa, then zikataifishwa (tena na rais mkristu - Mwl Nyerere) baadae serikali ikashindwa kuzihudumia, na kanisa walipotaka kuziendelea tena kukawa na wasiwasi kwamba serikali inaweza kurudia mambo ya zamani ya kutaifisha. Na ili kanisa kuziendeleza shule, hospitali (nyingine ilikuwa ni kuzifufua maana zilikuwa zimechoka sana) kwa kusaidiana na Kanisa Ujerumani walitaka kuwa na written agreement kati ya serikali na hakutakuwa na mambo ya kutaisha tena, otherwise ingekuwa na mchezo wa kupiga hatua moja mbelem na hatua 2 nyuma!


Kwenye red: Kanisa Ujerumani wanapata hela (i.e ruzuku) toka serikalini. Hivyo Serikali inakuwa na sauti maana ni kodi ya wananchi wa Ujerumani ndio inatumika kusaidia baadhi ya hospitali na shule Tanzania.

Kwenye blue: Boss wa Prof Mahalu wakati anapata nafasi ya ubalozi Rome ni Kikwete - Mwislam! Lakini MOU ilisainiwa mwaka 1992 - wakati huo rais akuwa Mzee Mwinyi - naye mwislam!. Pia MOU sio tu na Kanisa Katoliki. Soma vizuri kwenye cover page utaona!

NB: Unaweza kueleza nini kilitokea kwa BAKWATA maana nao walikuwa kwenye mazungumzo ya awali na serikali ili kupata assurance ya kutotaifishiwa mali zao! What happened?
 
Wakati mwingine nikisoma mijadala kama hii najikuta kupata ushawishi wa kuegemea upande wa akina Kirangga et.al kuhusiana masuala ya dini na Imani.Huu Uislam na Ukristo ni sumu mbaya sana katika taifa hili.Kuna haja masuala haya yakatizamwa kwa upana zaidi..
 
Sasa mlitaka wakristo wa ujerumani wasaidie Bakwata pia? Basi pelekeni maombi!!! Mkikubaliwa, serikali ya Tanzania itakuwa observer hata kwa waislam pia!!!
 
Nakubaliana na Dr Slaa kuwa kabla ya kulaumu na kusemama lolote lile ni vyema kufanya utafiti kwanza ili muweza kujiridhisha na si kupiga kelele,kutukana,kulaumiana na kukejeli kwa jambo ambalo huna uhakika wowote ule.JF isonge mbele kwa nguvu ya Radi
 

Hili swala MoU tutamaliza pages hapa JF, cha msingi kama serikali iko wazi itupe maelezo na tuwaulize maswali ya msingi kuhusu MoU. Binafsi naamini ni ufisadi na matumizi ya pesa za serikali kuhudumia kundi fulani la raia wengine.

Kinachosikitisha zaidi, wakristo wanapinga serikali kujiunga na OIC kwa sababu srikali haina dini, hizi si double Standards?

JF ni platform wenye masikio wamesikia, wakiona yana maana watayafanyia kazi. Ila kama wanataka waone waislamu watafanya nini waendelee na sarakasi zao lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
Hawa Wailamu badala ya kuhangaika na mikataba mibovu ya raslimali za taifa, baadala yake wanalalamikia serikali kuridhia misaada ya ujerumani kwa makanisa ya Tanzania... Hata haiingii akilini!
 
hutajibiwa! MoU ilifungwa kiusiri na kila kinachoizunguka MoU ni usiri tu!

wacha kuseveza wewe...nyie inaonekana nia yenu ni kuchinja tu mama zenu kwa chochezi za kipu.z. mwanzoni mlikuwa kwenye mchakato wa MoU. GHAFLA MKAWA HAMPO.. SASA TUELEZENI ILIKUWAJE? Tunataka haki itendeke. kama hamkutendewa kwa khaki mtendewe sasa. ssa semen vinginevyo pelekeni kiu yenu ya damu kuleee mbali kabisa na Tanzania na Afrika.

BTW, religion is an Opinum of the people...

ntarejea. Ngoja nktabarhuku kwanza...
 
Binafsi napongeza madhehebu yote ya dini kwa kuisaidia serikali yetu kutoa huduma za kijamii hasa pale inaposhindikana kupata huduma toka serikalini. Kikawaidi zipo huduma ambazo serikali huzitoa bure kama huduma ya mama na mtoto au wazee. Pia kuna magonjwa ambayo tiba zake hugharamiwa na serikali. Sihitaji kujiuliza hapa fidia kwa watoa huduma hizo ambao si serikali itafanyika vipi. Tatizo udini ukizidi utu na ubinadamu unapotea. Ukweli huwa ni ule tu unaofundishwa na dini ya huyu mtumwa wa dini. Akili hukatazwa kufanya kazi katika mazingira hayo. Hapa mtu hutumia kanisa au msikiti kama ubongo wake. Mtu akifika katika hatua hiyo hana maana yoyote katika jamii na mara nyingi ni tishio kwa maisha ya jamii husika.

Tukiendekeza kufikiri kupitia nyumba zetu za ibada hata familia zetu zitasambaratika na taifa litaisha.

Wapo baadhi ya viongozi wetu waliopewa majukumu ya kulinda amani na utaifa wetu wameambukizwa ugonjwa wa kufikiri kwa kutumia nyumba za ibada. Hali hiyo haitatuacha hapa tulipo. Nakuhakikishi tukiwaendekeza hawa watatafuna nchi yote kwani lengo lao ni kuidinisha nchi nzima.

Wakati wenzetu wanafikiri kwa akili zao nini wafanye kuboresha maisha yao tupo buzz na MoU ambayo hata contents zake hatuzijui. Pengine hatuna uhakika wa uwepo wa hiyo MoU.

Maswali kama haya yanapoteza muda mwingi na kuibua hisia za utengano miongoni mwa wananchi. Nasikitika kuona kuna posts zaidi ya 1000 na hakuna maelezo yoyote toka chombo husika. Ni nzuri kuthamini mchango wa SOCIAL MEDIA katika ujenzi wa demokrasia na maendeleo. Nawaomba wahusika serikalini kutoa ufafanuzi kuhusu MoU inayoongelewa hapa ili angalau watu watafakari mengine.
 

Sasa tukusaidiaje wewe? Kasema tena kwa herufi kubwa matatizo ya ukarabati ya shule, uwezo mdogo waliokuwa nao serikali kukarabati na hata kuomba wasaidiwe lakini kwa ajili ya sera ya kubinfsisha ilivyokuwa imeshamiri, wafadhili wakataka waahidiwe na ndio tunaanza hapo, ilalwewe bado sio thinker!
 

Nakubaliana nawe 100% juu ya serikali kufafanua na kueleza hii MOU, tena haraka iwezekanavyo.

Baraza la Maaskofu liliitaka ifanye hivyo haijafanya, lakini ni hali ambayo ingeepukika kama Serikali ingekuwa wazi juu ya mambo kama haya.

Na pia ijielekeze zaidi kupeleka maendeleo kwa watu na sio vitu kwa raia wote nchi nzima. Hii pengine ingepunguza wigo wa malalamiko kwa sehemu; kwani kuna baadhi ya watu wamepenyeza hila na uongo ambao kwa sasa ni sumu ya amani na umoja wa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…