Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkuu moshdar tupo pamoja ingawa kwa mtazamo tofauti,
MoU ni nini na nini kilisababisha iwepo ni jambo ambalo hakuna anayelilalamikia mkuu, na ndio maana hata kwenye maelezo ya ''tamko'' la Dr Slaa ameeleza kwamba utaifishaji ulihusu dini zote na kwenye mchakato mzima wa mwazo Dr ametaja BAKWATA iliwakilishwa na Waislam ingawa sijaelewa vizuri mwishoni wakaja kuwa makanisa pekee.
Sasa kwenye Red ndipo ninaposema labda Dr Slaa arudi kutoa ufafanuzi kukamilisha tamko lake.
hapo kwenye red ndipo kwenye contents za MoU yenyewe kunakoleta malalamiko yote maana sababu zilikuwa zile zile kwa waislam na wakristo na dini zingine

nakubaliana na wewe mkuu isipokuwa hapo kwenye bold. with due respect, kama kwa khiari yake Dr atapenda kufafanua sawa lakini, from my perspective, naona Huo ufafanuzi watoe wenyewe mashekhe vinginevyo wakanushe kuwa mwanzo hawakuhusika kama A Man of the People Dr Slaa alivyosema. Sisi wala A Man of the People Tusiwasemee Maulamaa. Mashkhe wafafanue kwa nini wao hawakuwa na MoU? Walikataliwa? nani aliwakatalia na aliwapa sababu gani?
 
At last mmenza kukiponda chama chenu kwa hoja zenu za Udini! Tunashukuru Mungu sumu yenu imeanza kuwatafuna wenyewe! Malipo ni hapa hapa! Mlijua mnaibomoa CDM kumba mnajibomoa na wenyewe!

Nakala: Matola, Crashwise, Precise Pangolin, Mungi, Kimbunga, Yericko Nyerere, Isango, Ben Saanane, MAMA POROJO, Dr.W.Slaa, etc.

TUMBIRI (PhD, HULL City - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Mama POROJO ni Mfuasi na shabiki mkubwa wa mtuhumiwa mmojawapo wa wanaotaka kuisambaratisha CHADEMA.Soma post zake za Nyuma.
 
mkuu moshdar.

sina chakuongeza umesimama kwenye mstari wa heri, amani, upendo na umoja (Tanzania na watanzania sio waislamu Vs wakristo) sisi sote ni watanzania tujivunie utanzania wetu (Umoja) sio dini zetu, ukabila wetu au siasa

Tanzania ni yetu tuitunze amani tulionayo kwa maslahi yetu na vizazi vyetu

Sumu ya Mohamed Said isipewe nafasi maana sote tutakuwa wahanga wa machafuko.

bandiko lako mkuu limetulia sana, wenye hekima watakuelewa isipokuwa kwa mshipa wa shetani mtu atashindwa kukuelewa.


ReLIGION IS AN (a notorious) opium of the people...tizama. mtu wa kiwango cha usomi wa Mzee Mohammed Said, potelea mbali hata kama usomi wenyewe ni ule wa juu ya nadharia juu ya uwepo wa kitu kiitwacho mungu, sadeeq, rits na wengineo....usomi wao wooooooooooooooooooooooooooote makhali ulipoishia ni hapa kuja kuchochoe chuki, fitna na magomvi kati ya wana wa afrika ili siye watukuze, wajukuze na wanawe mzee huyu Mohammed tuyainue majambia yetu huko yalikolala tuyatumie majambia hayo kuchinja tumbo za mama zetu ambao ni wakeze huyo mzee mOHAMED, tena tufanye hivyo KWA JINA LA mUNGU MWEMA MUNGU WA UPENDO. Hii ndiyo elimu/ilmu aitafutayo mwafrika, haimsaidii kuchambua na kutakari juu ya changamoto za ulimwengu huu kabla hajauacha siku chache zijazo, bali kukenua meno, kufurahia na kujiona mshindi maadamu tu ameitwa na wazungu(soma wakoloni) oxford university kuzungumza chuki na fitna dhidi ya waafrika wenzake, tena watanzania wenzake. muulize ametumiaje hiyo ilmu yake kubadilsha kizazi chake duni kutoka uduni kwenda ubora? jibu hana...ni mavyeti tu atakuchomolea kutoka kabatini lakini mchango kwa jamii ziro. utaskia mimi ni profesa bana, mimi nina masterz bana, mimi nina degree bana, muulize umeitumiaje hiyo degree kuiballi dunia for the better? utakuta hamna kitu sana sana wizi na ufisadi na uchochezi ili ndugu tuuane.

ningekuwa nimekuwa brainwashed kama huyu mzee Mohammed Said, kias cha kuaminishwa kuna kitu kinaitwa mungu, basi ningesema "Mungu amlaani sana huyu mzee". lakini kwa kuwa sijawa brainwashed basi nasema "ulaaniwe sana mzee Mohammed Said( na wenzako woooooooote wenye ubazaz kama wako, no matter of what religion) na chochote kile kiwezacho kukulaani.

halafu watu mnashangaa kwa nini wazungu wanatutupia maganda ya ndizi tule kama manyani kwa sababu hiyo ndo hasa stahiki yetu!! wenzetu wameshatua mars, sasa wanalitafuta jua, sisi tumekalia ----- wa uchochezi, kugombana kati yetu, kufitiniana, kuchukiana na hata kuuana kwa sababu ya tofauti ya fikra za kikoloni tulizopandikiziwa na mkoloni ambaye ni mkolon huyo huyo ambaye, baada ya mwezini, sasa keshatua mars akitafuta uwezekano wa kwenda kuwekeza huko ikiwa ni pamoja na kupeleka tena hizi hizi fikra za ki-atheist. sisi tumebaki tunachinjana tukigombea kiwanja cha chang'ombe alichogawa nyerere (wote someni baba wa Taifa la Tanzania, Mwana wa Afrika, Mwanamapinduzi, mwanazouni, kisima cha fikra sahihi na endelevu na Nabii wa Karne ya Ishirini, Mzee Muheshimiwa sana Julius Kambarage Nyeere-RIP Mzee Wetu) miaka ya sitini...

uuuuuuuuuuuuwi, apaa mmawomi, miafirika kweli ndivyo tulivyo chambeche nguGu yangu mmoja humo JF.
 
Hebu waislamu tujitathmini kwanza badala ya kuhamishia makosa kwa wengine.
Kwanza tujiulize tulikuwa na shule ngapi na za viwango gani?Ukichunguza sana utaona shule zilikuwa za madhehebu ya Ismailia na zaidi kwa watoto wa kihindi.
Jambo la pili ni kuwa ni nani alikuwa msimamiziwa mali za East africam muslim welfare,huyu ndiye angeweza kuungana na wakiristo katika kudai shule na hospitali (kama ziliikuwepo).
Mapungufu makubwa ni yetu na tusilalamike tulishindwa na tunazidi kushindwa kutumia fursa,mfano mzuri ni kuwa serikali kupitia bodi ya mikopo inatoa mikopo kwa wanfunzi wa vyeo vya juu na ukianzisha chuo kikuu na ukaweka hata faculty moja tu ya education tayari pesa unayo lakini hata hicho tulichpewa cha morogoro bado/

Ukweli utabakia palepale kwamba serikali ilivyoingia kwenye memorandum ya kutokutaifisha mali za makanisa ilikuwa ni makosa. Utaifshaji ni sera ya taifa, kwa hiyo kama issue ni kulinda utaifishaji ilibidi iwe kwa dini zote na hata wasio kuwa na dini pia. Jambo jengine serkali kama guardian wa raia haikupaswa kutoa upendeleo wowote kwa kundi lolote lile katika jamii. Hizo nyingine ni porojo zako, waislamu tulishajitathmini zamani. Kilichobakia ni serikali kujiondoa kwenye hiyo MoU.
 
Niruhusu nikuulize swali rahisi lakini litakalokupa ufahamu rafiki, swali lenyewe ni hili: Kwa mfano Tanzania wanawake wanaishi takriban miaka 54 na wanaume kwenye 50, kwa hiyo kwa kuwa tumeshindwa kuhakikisha life expectancy ya wanaume inalingana na ya wanawake, basi tuwaue wanawake wote mara wafikishapo umri wa miaka 50 for the sake of equality?.

Common sense is not common. Niache na uelewa wangu wa kujidhalilisha lakini nawewe ni kuulize kitu kimoja:

Kwanini wakristo mnapinga Tanzania isijiunge na OIC wakati watakaonufailka ni waislamu na wasiokuwa waislamu? Hii si inapingana na hiyo logic yako yu kuuwa wanawake, au unasemaje?
 
kasome kwanza maelezo ya Dr. Slaa ni kwanini palikuwepo na hiyo MOU, halafu uje uzisome vizuri hizo clauses hapo juu...

HATA WEWE AKILI HUNA...UNASUMBULIWA NA NENO "CHURCH" EHHEEE JARIBU KUTAFSIRI SENTENSI NZIMA SIYO NENO MOJA MOJA.

Hizo clause hapo juu mimi nimezielewa kwamba

1) ‘The government shall provide vacancies in its Teachers training colleges for training qualified persons as teachers earmarked for church owned schools’. Article xi

Serikali iwatengee nafasi wakristo kwenye vyuo vya ualimu, walimu ambao baada ya kuhitimu watakwenda kufundisha kwenye shule za makanisa. Sawa sawa au ina maana nyengine?

2) ‘The government shall endeavour to include financial assistance for church run social services in its bilateral negotiations particularly with the Federal Government of Germany. Consideration shall be made during its bilateral negotiations with other donors’. Article xiii.

Serikali ifanye juhudi kuingiza kipengele cha msaada wa kifedha kwenye mapatano yake ya kimataifa, hususan kwa Ujerumani. Pia serikali itilie maanani swala hilo kwa waadhili wengine.

Hayo ya kwamba nina akili au sina namwachia mama yako akufundishe kujadiliana na watu bila matusi.
 
1.Serikali haikusomesha Wakristo wakristo walijisomesha wenyewe kwenye shule zao walizojenga wakati nyie mpo busy kujenga Madrasa Serikali iliwasomesha nyie baada ya kuzipora shule za kikristo ili mpate nafasi ya kusoma lakini bado mnazichukia hizo shule

2. Kanisa halikutaka watu waende kusomea ualimu kwasababu tu ni Wakristo bali vigezo vilizingatiwa na walitaka kuziendeleza hizo shule ambazo hata nyie mlisoma

3. Hapo ndo kuna shida tu eti wafaidike waislamu tu? Tunataka program ambazo kila mtu bila kujali dini yake atafaidika

Tunachosema hapa ni kuwa MoU ilitengeneza upendeleo maalum kwa wakristo over and above hizo nafasi za watanzania wengine. Issue sio kufaidika waislamu watupu, kwani kwenye hizo shule za kanisa waislamu wanasoma bure.

Huu ufisadi hautofautiani na ufisadi mwingine ambao unapigwa vita. Inabidi ukomeshwe hata mkijitetea vipi.
 
na kwa vyovyote vile, mimi kama atheist, kama kuna mtu aliwakatalia waislamu kuwa na MoU, no matter ni theist wa mungu yupi, huyo mtu lazima atabeba lawama hata kama ni Mzee wetu, Baba wa Taifa Nyerere, vingenevyo kuwe na sababu-mashiko zitazoonesha kinagaubaga kuwa, thiests wa mungu wa kiislamu kuwa na MoU hiyo kusingewafaidisha wana wa Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla. ikiwa itakuwa hivyo, nitapendekeza mtu huyo tusimkate shingo wala kumtukana, bali tumtake aombe radhi kama yu angali hai na kosa hilo lisahihishwe mara moja.

Katika mambo yanayoniuma sana ni kuona kuna baadhi ya theists wapo kifukara zaidi, kifikra na kimaendeleo, kulinganisha na theists wa upande mwingine. hii ni kwa sababu najua vita vya theists ni vita mbaya, theists ni watu khatari kwa usalama wa sayari hii, ogopa mtu theist anaua theits mwenzake(na hata atheist) ili aende peponi kwa Mungu mtawala na muweza wa yote!

natoa mwito kwa vijana wa kizaz hiki cha "doti komu" tuzikatae fitna na uchochezi huu no matter anachochea nani. hata kama anachochoe mzee wa upako-tukatae, hata kama anachochoe getrude Mogella-tukatae, hata kama anachochea shkhe wa darisalamu-tukatae, hata kama anachochea Pengo-tukatae, hata kama anachochoe sjui m-budha, m-hindu nk nk wa wapi...tuzikatae. TUZIKATAE TUZIKATAE TUZIKATAE TUZIKATE. Vijana woote bila kujali itakidi zetu, dini zetu, ukabila wetu tuwaze kwa pamoja ni vipi tutakabilana na wenzetu wa afrika mashariki ndani ya hilo soko? tukizubaa tutatawaliwa tena mara ya pili tena na wana afrika mashariki wenzetu. ndoto zetu iwe ni kwenda kununua kiwanja cha changombe hukoooo mars, tuwaachie mzee Mohammed Said na Ponda(na hata kina Pengo kama nao wamo) wafitiane na kiwanja cha chang'ombe ya dar...sisi tusikubali kuchinja mama zetu kwa kuchochewa na fikra duni na mfu..HIMA HIMA vijana waafrika wenzangu, wana wa kizazi kipya, wana mapinduzi, wana wazalendo wa Mama yetu Tanzania, wana wa mama wa Afrika kamwe tusikubali kulikata ziwA la mama yetu Afrika kwa kuchochowe na Mzee Mohammed na wengine wa namna yake. tuondokane na UKOLONI, TUSONGE MBELE, Fursa tunazo. changamoto ni zetu tuzikabili pamoja. kamwe tusiwakubali wachonganishi NA wafitini. tukumbuke dini hizi hizi zilitumiwa kutoboa miguu ya babu zetu, kuwafunga kwa minyonyoro na kuwatenda kama wanyama mwitu. Tukumbuke waafrika wenzetu, kama drogba na wenzie, leo na mafanikio yake yote kimichezo na kiutajiri..bado wakoloni wale wale waliotuletea hizi dini wanawadhihaki mchana kweupe bila aibu vijana wenzetu wakiwatupia maganda ya ndizi ikiwa ni dhihaka kwao kuwa yeye drogba bado ni nyani tu na hana lolote. tukumbuke khali hiyo si tofauti uwapo Saudia Arabia.
 
Fresh,
Ukifuatilia majibu ya Mnyamahodzo na wengine utaona maswali yako 2 yamejibiwa kwa kina ila inaonekana sio majibu uliyoyataka.

Kwa hivyo in context, ni kuwa Kanisa liliitaka Serikali iheshimu na kuwajibika kimkataba juu hoja muhimu ya ubora wa walimu kama sehemu ya utekelezaji wa MOU nzima. Jitahidi usisome zaidi ya kilichoandikwa.

Kaitka hali ya kawaida nategemea wengi wa wakristo watapinga hoja kwamba serikali ilikosea kwa kulipendelea kanisa na kuacha nyuma raia wengine. Ili haya yathibitike, tuiombe serikali izungumzie MoU na fedha ambazo serikali imeshazitoa kwa kugharimia miradi ya kanisa na itoe nafasi kwa waumini wa dini nyingine wachambue hoja za kanisa na serikali katika kuitetea MoU. Otherwise, hatutayamaza kusema kwamba serikali inavyofanya sivyo na athari zake huenda zikawa mbaya.
 
Mkuu mbona hili swala mkuu lynxeffect22 na wengine humu wamekujibu lakini hutaki kuelewa au unataka majibu yatakayo kupendeza unatatizo kubwa sana la udini

Tatizo langu laudini haliwashindi nyie wakristo mnaodhulumu taia wenzenu kwa kutumia MoU kwa kisingizio kwamba na waislamu wanatumia huduma. Lengo ni kila siku waislamu wawategemee wakristo kwenye mashule na mahospitali?
 
Ukurasa wa nje wa MoU una maneno yafuatayo:
MEMORANDUM OF UNDERSTANDING
BETWEEN
CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA AND TANZANIA EPISCOL CONFERENCE
AND
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA(sio Serikali ya Ujerumani).

Drawn by Prof.C R Mahalu.
Kilichozisimamisha nywele za kichwani mwangu ni Mahalu huyohuyo ambaye alikuja kuwa balozi wa Tanzania Rome (kitovu cha ukatoliki)
na kukumbwa na kesi ya ufisadi!...ufisadi juu ya ufisadi.

Vilevile hotuba ya Rais Dodoma anaelezea kuwa Serikali ilitiliana saini na Kanisa (si Ujerumani), nikinuuu:

"baada ya Serikali kutiliana saini Itifaki ya Makubaliano (MoU) na TEC na CCT mwaka 1992, kasi ya kurejesha shule ilikuwa ndogo sana na baadae ikasimama kabisa".

Ni sahihi kwa MOU kuwa kati ya Kanisa na Serikali kwa sababu serikali ndiye ilikuwa inataifisha. Na kama umesoma vizuri background ya hii MOU ni kwamba waliokuwa wanatoa msaada yaani Kanisa/serikali ya Ujerumani walitaka assurance kuwa shule au hospitali ambazo wangesaidia hazitatifishwa!

Why? Mwanzo shule, hospitali hizo zilikuwa chini ya kanisa, then zikataifishwa (tena na rais mkristu - Mwl Nyerere) baadae serikali ikashindwa kuzihudumia, na kanisa walipotaka kuziendelea tena kukawa na wasiwasi kwamba serikali inaweza kurudia mambo ya zamani ya kutaifisha. Na ili kanisa kuziendeleza shule, hospitali (nyingine ilikuwa ni kuzifufua maana zilikuwa zimechoka sana) kwa kusaidiana na Kanisa Ujerumani walitaka kuwa na written agreement kati ya serikali na hakutakuwa na mambo ya kutaisha tena, otherwise ingekuwa na mchezo wa kupiga hatua moja mbelem na hatua 2 nyuma!


Kwenye red: Kanisa Ujerumani wanapata hela (i.e ruzuku) toka serikalini. Hivyo Serikali inakuwa na sauti maana ni kodi ya wananchi wa Ujerumani ndio inatumika kusaidia baadhi ya hospitali na shule Tanzania.

Kwenye blue: Boss wa Prof Mahalu wakati anapata nafasi ya ubalozi Rome ni Kikwete - Mwislam! Lakini MOU ilisainiwa mwaka 1992 - wakati huo rais akuwa Mzee Mwinyi - naye mwislam!. Pia MOU sio tu na Kanisa Katoliki. Soma vizuri kwenye cover page utaona!

NB: Unaweza kueleza nini kilitokea kwa BAKWATA maana nao walikuwa kwenye mazungumzo ya awali na serikali ili kupata assurance ya kutotaifishiwa mali zao! What happened?
 
Wakati mwingine nikisoma mijadala kama hii najikuta kupata ushawishi wa kuegemea upande wa akina Kirangga et.al kuhusiana masuala ya dini na Imani.Huu Uislam na Ukristo ni sumu mbaya sana katika taifa hili.Kuna haja masuala haya yakatizamwa kwa upana zaidi..
 
Mkuu moshdar tupo pamoja ingawa kwa mtazamo tofauti,
MoU ni nini na nini kilisababisha iwepo ni jambo ambalo hakuna anayelilalamikia mkuu, na ndio maana hata kwenye maelezo ya ''tamko'' la Dr Slaa ameeleza kwamba utaifishaji ulihusu dini zote na kwenye mchakato mzima wa mwazo Dr ametaja BAKWATA iliwakilishwa na Waislam ingawa sijaelewa vizuri mwishoni wakaja kuwa makanisa pekee.
Sasa kwenye Red ndipo ninaposema labda Dr Slaa arudi kutoa ufafanuzi kukamilisha tamko lake.
hapo kwenye red ndipo kwenye contents za MoU yenyewe kunakoleta malalamiko yote maana sababu zilikuwa zile zile kwa waislam na wakristo na dini zingine
Sasa mlitaka wakristo wa ujerumani wasaidie Bakwata pia? Basi pelekeni maombi!!! Mkikubaliwa, serikali ya Tanzania itakuwa observer hata kwa waislam pia!!!
 
Nakubaliana na Dr Slaa kuwa kabla ya kulaumu na kusemama lolote lile ni vyema kufanya utafiti kwanza ili muweza kujiridhisha na si kupiga kelele,kutukana,kulaumiana na kukejeli kwa jambo ambalo huna uhakika wowote ule.JF isonge mbele kwa nguvu ya Radi
 
Freshthinking naomba tuwekana sawa katika hili
1. Hizo nafasi za upendeleo unazozirudia rudia sana ni zipi? - Kutoa nafasi za kufundisha walimu watakaohudumu katika taasisi zinazoendeshwa na makanisa ndicho kinachozungumzwa kwenye MoU. Wakati huo hakukuwa na vyuo vya binafsi vya kufundisha walimu isipokuwa TTC za serikali. Kipengele hiki kinasema serikali itoe nafasi kwa watu watakaofundisha katika taasisi za makanisa. Sioni tatizo hapo, tafuta kipengele chengine.
2. Maombi ya misaada - Kumbuka hapa serikali ndo ilikuwa inayataka makanisa yaisaidie kuziendesha shule na hospitali ambazo walizitaifisha halafu wakashindwa kuziendesha. Makanisa yalikuwa na uwezo wa kupata misaada kutoka kwa taasisi za kutoa misaada za makanisa kutoka nchi zilizoendelea. Lakini na wao wakaishauri na serikali kwa upande wake nayo itafute misaada. Kosa lipo wapi?
.

Hili swala MoU tutamaliza pages hapa JF, cha msingi kama serikali iko wazi itupe maelezo na tuwaulize maswali ya msingi kuhusu MoU. Binafsi naamini ni ufisadi na matumizi ya pesa za serikali kuhudumia kundi fulani la raia wengine.

Kinachosikitisha zaidi, wakristo wanapinga serikali kujiunga na OIC kwa sababu srikali haina dini, hizi si double Standards?

JF ni platform wenye masikio wamesikia, wakiona yana maana watayafanyia kazi. Ila kama wanataka waone waislamu watafanya nini waendelee na sarakasi zao lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
Hawa Wailamu badala ya kuhangaika na mikataba mibovu ya raslimali za taifa, baadala yake wanalalamikia serikali kuridhia misaada ya ujerumani kwa makanisa ya Tanzania... Hata haiingii akilini!
 
hutajibiwa! MoU ilifungwa kiusiri na kila kinachoizunguka MoU ni usiri tu!

wacha kuseveza wewe...nyie inaonekana nia yenu ni kuchinja tu mama zenu kwa chochezi za kipu.z. mwanzoni mlikuwa kwenye mchakato wa MoU. GHAFLA MKAWA HAMPO.. SASA TUELEZENI ILIKUWAJE? Tunataka haki itendeke. kama hamkutendewa kwa khaki mtendewe sasa. ssa semen vinginevyo pelekeni kiu yenu ya damu kuleee mbali kabisa na Tanzania na Afrika.

BTW, religion is an Opinum of the people...

ntarejea. Ngoja nktabarhuku kwanza...
 
Binafsi napongeza madhehebu yote ya dini kwa kuisaidia serikali yetu kutoa huduma za kijamii hasa pale inaposhindikana kupata huduma toka serikalini. Kikawaidi zipo huduma ambazo serikali huzitoa bure kama huduma ya mama na mtoto au wazee. Pia kuna magonjwa ambayo tiba zake hugharamiwa na serikali. Sihitaji kujiuliza hapa fidia kwa watoa huduma hizo ambao si serikali itafanyika vipi. Tatizo udini ukizidi utu na ubinadamu unapotea. Ukweli huwa ni ule tu unaofundishwa na dini ya huyu mtumwa wa dini. Akili hukatazwa kufanya kazi katika mazingira hayo. Hapa mtu hutumia kanisa au msikiti kama ubongo wake. Mtu akifika katika hatua hiyo hana maana yoyote katika jamii na mara nyingi ni tishio kwa maisha ya jamii husika.

Tukiendekeza kufikiri kupitia nyumba zetu za ibada hata familia zetu zitasambaratika na taifa litaisha.

Wapo baadhi ya viongozi wetu waliopewa majukumu ya kulinda amani na utaifa wetu wameambukizwa ugonjwa wa kufikiri kwa kutumia nyumba za ibada. Hali hiyo haitatuacha hapa tulipo. Nakuhakikishi tukiwaendekeza hawa watatafuna nchi yote kwani lengo lao ni kuidinisha nchi nzima.

Wakati wenzetu wanafikiri kwa akili zao nini wafanye kuboresha maisha yao tupo buzz na MoU ambayo hata contents zake hatuzijui. Pengine hatuna uhakika wa uwepo wa hiyo MoU.

Maswali kama haya yanapoteza muda mwingi na kuibua hisia za utengano miongoni mwa wananchi. Nasikitika kuona kuna posts zaidi ya 1000 na hakuna maelezo yoyote toka chombo husika. Ni nzuri kuthamini mchango wa SOCIAL MEDIA katika ujenzi wa demokrasia na maendeleo. Nawaomba wahusika serikalini kutoa ufafanuzi kuhusu MoU inayoongelewa hapa ili angalau watu watafakari mengine.
 
Du!!! Kumbe MOU maana yake ni makubaliano ya kimaendeleo baina ya Wakristo wa Tanzania na Ujerumani!!??? Kumbe serikali ya Tanzania iliridhia tu kama observer!!! Kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza! Sasa maskini kelele nyingi kuhusu MOU ni za nini???

Sasa tukusaidiaje wewe? Kasema tena kwa herufi kubwa matatizo ya ukarabati ya shule, uwezo mdogo waliokuwa nao serikali kukarabati na hata kuomba wasaidiwe lakini kwa ajili ya sera ya kubinfsisha ilivyokuwa imeshamiri, wafadhili wakataka waahidiwe na ndio tunaanza hapo, ilalwewe bado sio thinker!
 
Kaitka hali ya kawaida nategemea wengi wa wakristo watapinga hoja kwamba serikali ilikosea kwa kulipendelea kanisa na kuacha nyuma raia wengine. Ili haya yathibitike, tuiombe serikali izungumzie MoU na fedha ambazo serikali imeshazitoa kwa kugharimia miradi ya kanisa na itoe nafasi kwa waumini wa dini nyingine wachambue hoja za kanisa na serikali katika kuitetea MoU. Otherwise, hatutayamaza kusema kwamba serikali inavyofanya sivyo na athari zake huenda zikawa mbaya.

Nakubaliana nawe 100% juu ya serikali kufafanua na kueleza hii MOU, tena haraka iwezekanavyo.

Baraza la Maaskofu liliitaka ifanye hivyo haijafanya, lakini ni hali ambayo ingeepukika kama Serikali ingekuwa wazi juu ya mambo kama haya.

Na pia ijielekeze zaidi kupeleka maendeleo kwa watu na sio vitu kwa raia wote nchi nzima. Hii pengine ingepunguza wigo wa malalamiko kwa sehemu; kwani kuna baadhi ya watu wamepenyeza hila na uongo ambao kwa sasa ni sumu ya amani na umoja wa Taifa.
 
Back
Top Bottom