Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

nimeona matamko kadhaa yanayosemwa kuwa ni misimamo ya kanisa katoliki bila Serikali kuongea....sasa mimi kama mwananchi ninayeipenda Serikali hii najaribu kurejea mijadala iliyokwama au kusitishwa kwa namna yoyote ile.
 
Kwanini haukusapoti hiyo hoja wakati ilipoletwa na waislam? Au imegusa maslahi yenu ndo maana?

Na siyo kanisa tu, hata mjinga kuliko wewe anaweza kuona wazi kabisa kwamba katiba iliyopo haifai. Na siyo hivyo tu, bali hata iliyopo ambayo mumeapa kwa kutumia misahafu kutoka kwa hao unaowalaumu, bado hamuifuati!

Katiba inaruhusu vyama vingi, nyie mnafanya matendo ya kudidimiza haki ya vyama vingi, demokrasia yake, pamoja uhuru unaoambatana na demokrasia hiyo ya vyama vingi.
 
nimeona matamko kadhaa yanayosemwa kuwa ni misimamo ya kanisa katoliki bila Serikali kuongea....sasa mimi kama mwananchi ninayeipenda Serikali hii najaribu kurejea mijadala iliyokwama au kusitishwa kwa namna yoyote ile.
forget it...anaweza kuwananga wastaafu lakini sio hawa na ndo maana kapiga kimya
na uvimbe upasuke,utajijua mwenyewe😀
 
That is very right...kwamba kipindi cha nyerere alifanya yale kwa kuwa Serikali ilishindwa kutoa huduma kwa wananchi kwa ajili ya uchanga wake.Sasa hivi kuna afadhali kubwa je kuna umuhimu wa kuendelea na MoU?
By the way haya makanisa na taasisi za dini yaliwahi kuwa sehemu ya uhujumu wa jamii ya kitanzania haswa haswa enzi zile za ukoloni lakini wananchi na serikali kwa ujumla ilisamehe yote na kuamua kuingia kwenye makubaliano ...leo hii tuko kwenye zama mpya kabisa je hakuna haja ya kureview?
Kama kanisa limeamua kuisogelea na kuhandle mambo kisiasa basi hakuna budi turejee hiyo siasa.
 
Ref: NB yako. Na wewe binafsi uko kwenye upande upi? Mpagani, muislamu au mkristo mkatoliki?
 
kutokupost wakati huo sio hoja na hata kupost wakati huu sio hoja.
Hoja ni je turejee mchakato wa MoU au Katiba mpya?
Tufanye hivyo kwa maslahi ya nani na kuachieve nini?
Je kama mwanachi kwa nini unishinikize kufanya marejeo ya jambo moja na sio yote kwa maslahi ya Taifa?

yaani wewe unafurahia kurejea majadiliano ya katiba mpya lakini hufurahii marejeo ya mjadala wa MoU ...!huo ni unafiki mkubwa.
 
Naunga mkono hoja. MoU ya Kanisa na serikali ujadiliwe na kiwekwa hadharani. Navyofahamu hospital nyingi za kanisa hazitaki hata kuwa chini ya serikali. Mfano ni KCMC na Bugando. Hospital hizo nashauri zirudishwe kwenye udhibiti wa kanisa na serikali ijenge hospitali zake.

MoU ivunjwe sasa
 
Ifike mahali hawa maaskofu na mashehe watambue kuwa jukumu lao ni kwenye maswala ya imani tu na sio kuingilia kwa namna yoyote ile mambo ya kisiasa...
Uchafu wanaoufanya unajulikana na wasichukulie ukaaji kimya wa Serikali ndio kama vile wanaogopewa....
 
Kudadadeki! Ukiona hawa wachumia tumbo wanaanza kulia lia kuhusu shinikizo la mchakato wa katiba mpya, ujue CCM imeshikwa pabaya. Swala la mabadiliko ya katiba haliepukiki kwa sasa. Hayo ya MoU, watanzania hawayajui wala hawaoni hasara zake.
 
ha ha ha...wachumia tumbo ni wale wanaotoa matamko kila kukicha!
 
Kwahiyo maaskofu kuzungumzia madhila ya waumini wao mnaleta habari za MoU. Kwenye hiyo MoU kwani kuna nini. Endeleeni kukimbizana na mijusi, ikigeuka Swira, usikimbie usimame hapo hapo.
 
mkuu hizi hospitali ukienda kama mtoto chini ya miaka mitano,mjamzito au mzee zaidi ya miaka 60 huwezi pata huduma kama kwenye hospitali za Serikali despite MoU ...hayo ni baadhi ya maudhi ya MoU.

Shule za makanisa au misikiti zinacharge ada za ajabu sana na sio katika mategemeo ya MoU!

Halafu askofu anasimama kuongelea katiba mpya as if itasolve upuuzi wa namba hii.
 
Kwahiyo maaskofu kuzungumzia madhila ya waumini wao mnaleta habari za MoU. Kwenye hiyo MoU kwani kuna nini. Endeleeni kukimbizana na mijusi, ikigeuka Swira, usikimbie usimame hapo hapo.
madhila ya waumini kwa kiasi kikubwa ni kwenye huduma za jamii yaani elimu na afya...na haya yamo kwenye MoU.
Sitegemei katiba mpya badala ya sasa ndio itashinikiza makanisa au misikiti itoe huduma za wazee,watoto chini ya miaka mitano na wazazi bure ...kulingana na sera ya Taifa...kitu ambacho kipo kwenye MoU.

Good thing nomewahi kudeal na hizi taasisi za kidini katika hili.
 
Wewe utakuwa apostoliko, Katoliki ni dini ya siasa ndio maana tunaye balozi wa Vatican hapa nchini. Na ndio sababu nchi yetu inaongozwa na watu waliosomeshwa na wakatoliki hata kama wao ni waislamu. Na pili huna bunge la kuijadili MoU!
 
soma N.B yangu hapo juu
 
mada imejibiwa hapa na mjadala umefungwa

Mimi nadhani kwa hoja hizi mjadala umekwisha. Tusepeni tu.
 
Kama nia yenu ni ku-polarise basi reaction yetu ni polarsation!!
Kwa wana sayansi watanielewa zaidi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…