Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

ngoja nikapige dufu, kwa raha zangu hayanihusu! leo ubwabwa wapi? nijuzeni ndugu zangu. najua gharama yangu ni ndizi usafiri miguu. Inshaalah!
 
Wajibu wa serikali ni kutoa ulinzi,elimu,huduma za afya n.k kwa raia wake kwa kutumia vyombo vyake. Inapokuwa haina vyombo vya kutolea
huduma serikali huingia mkataba na mtu au taasisi yoyote ili kufikia malengo hayo. Mathalani, ni wajibu wa serikali kujenga barabara hivyo huingia
mikataba makampuni au taasisi mbalimbali baada ya kubaini kitengo chake cha ujenzi wa barabara hakiwezi kufanya kazi hiyo;vivyo hivyo kwa elimu na afya.
 
Unajua watu hawajui mambo madogo sana. Utadhani hizo MoU zilikuja kutoa pesa za kujenga hospitali za Bugando, KCMC, St. Francis, Peramiho, Ilembula, Itete, mpaka nitachoka kuzitaja. Jamani hospitali za makanisa ni nyingi sana. Kiasi kwamba tunaweza tukatoa conclusion kwamba huduma za afya tanzania zinatolewa na makanisa. Hivyo serikali inabidi ichangie kwa kutoa kiasi cha pesa kwa ajili ya kutoa huduma na mishahara kwa watoa huduma wakubwa.
Wengi wetu hawajui kwamba hospitali kubwa za serikali ya Tanzania ni mbili tu, yaani Muhimbili National Hospital na Mbeya Referral Hospital. Nyingine zote ni za kikristo, ukiacha baadhi ya hospitali kama Aga Khan ambazo mtu mwenye kipato cha chini hatii mguu pale. Sasa wewe ulitaka serikali ichangie wapi?
Unajua serikali ina tabia ya kuchangia kwa watu wanaotoa huduma fulani kwa niaba yake. Kuna mkinga yupo Mafinga ana mamia ya hectares za miti ya mbao, serikali inampa zaidi ya milioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kulipa watumishi waliopo shamba lake... Sijui tutasema anapendelewa, tena jamaa mlutheri.
 
Nilitegemea kuona kifungu kipi cha katiba kilivunjwa...hamkukitoa
Rais aliyekuwepo AHM na wasasa JMK ali/anauwezo wa kuifuta kama haina manufaa..lakini hawaku/jafanya
Je, huduma zitolewazo zina ubaguzi wa aina yoyote..mmeshindwa kuthibitisha
Je, mliandaa MoU lakini ikakataliwa..????

Fanyeni kazi wenzenu wanawashangaa na muwe na mawazo ya kujenga...
 
FF na Haki! Ndugu zangu mpo wrong sana, Serikali ya Jamhur ya Tanzania haitoi pesa kwa Mashirika ya dini ya kikristo au makanisa, na hayo mashrika ya kikristo yanajiendesha yenyewe au kupata misaada toka nje ktk networks zao ambazo hazina mkono wa serikali na wala sio pia kwa mzigo wa loans. Tuache ushabiki na ulalamishi usio na maana na wenye kuleta chokochoko, tukae chini tuijenge nchi hii ndugu zangu.
 
Ukiisoma hii MOU na Kanisa hapo ndipo utakapojua kwamba hizo hela za kujenga hizo projects zinatoka wapi.
You've not answered my question, tunahitaji facts and figures. Serikali imetoa kiasi gani kwenye hii miradi?
 
Hivi hizi signing tunaangalia zitakavyo saidia watz au tuanachoangalia ni dini gani inahusika. Kimsingi madai ya kusema wakristu au waislam wanapendelewa na serikali mimi sioni kama kuna tija yoyote, ilimradi kama wamesign mkataba basi watoe huduma kwa watz wote sitaki kujua hii organisation ni ya wakristu au waislam imesainiwa na rais mwislam/mkristu. Hizi ndo fikra potofu. Sisi tunataka huduma hatutaki kujua inatolewa na mdini gani. Hoja kama hizi ndo zile eti mawaziri 50 wakristu wangapi waislam wangapi what for? Naona tutaenda mbali tuwe tunahoji shule binafsi tz ziko ngapi, ehe za wakristu ngapi za waislam ngapi? ooh wakristu/waislam wanapendelewa, na mengine kama haya hivi kwa mwendo huu tutaendelea. Mimi nadhani haya ya nani anamiliki hii mdini gani tuyatupilie mbali. Tuungane kwa pamoja kutatua matatizo ya watz.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Tatizo siyo utolewaji wa hizo huduma. Tatizo hizo huduma zinahudumiwa na fedha ya serikali, sasa kama ni za public kwa nini ziwe za upande mmoja tu?

Ni rahisi hivi: Ni suala la kuchagua tu, kama Ndanda hakuna hospitali ya serikali yenye kiwango sawa na ile ya Ndanda mission, je serikali iingie gharama kujenga hospitali ya kiwango kile au ifanye makubaliano na mmiliki kutoa huduma pale na serikali ichangie gharama hizo. Hata wewe unafanya hivyo unapohamia mji mwingine kikazi, unapohitaji nyumba kuna mawili: ujenge ya kwako au ukodi nyumba. Na wengi tunachagua kukodi, tunaingia mikataba na wenye nyumba. Kwa hiyo hiyo memorandum unayolalamikia haina tofauti na mikataba ya upangaji, hakuna kanisa linalosaidiwa kuendesha shughuli zake. Kama na wewe pia unataka kuisaidia serikali, nenda sehemu remote isiyo na hospitali, jenga hospitali halafu omba kuingia mkataba wa uendeshaji na serikali, ukikataliwa njoo hapa ulalamike tutakuelewa.
 
[h=1]News[/h] [TABLE="class: newsTable, width: 100%, align: center"]
[TR]
[TD="width: 100%"] Public Announcement on Second round of Application for 2011/2012 Admissions


The Tanzania Commission for Universities (TCU) wish to inform prospective applicants and the general public that a second round of applications through the Central Admission System will be opened starting on 1[SUP]st[/SUP] August to 22[SUP]nd[/SUP] August 2011.
The second round will be opened to those who will not be selected during the first round and applicants who did not apply during the first round of application, which was closed on 31[SUP]st[/SUP] May 2011. Names of unselected applicants will be posted on the TCU website and on the media immediately after the first round of selection is completed. Also, candidates aspiring to join higher education institutions and could not apply by the 31[SUP]st[/SUP] May 2011 are advised to apply. During the second round both unselected first round applicants and new applicants will be processed using the Central Admission System and selection results will be announced before 30[SUP]th[/SUP] September 2011. University institutions are thus advised not to admit any students outside the CAS to avoid unnecessary complications in the admission process. For further clarification please contact TCU through the following:

Executive Secretary,
P O Box 6562,
Dar es Salaam,

Tel: (255) (22) 2772657,
Fax: (255) (22) 2772891,
Hotline number: 0759 539987, 0759 537659, 0714 582742, 0783 600424 and 0773971363,

Email: es@tcu.go.tz, dad@tcu.go.tz or admission@tcu.go.tz
TCU offices along Garden, Mikocheni, Dar es Salaam.

Prof S.E. Mchome
EXECUTIVE SECRETARY
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Click here to view all news.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Hata mimi nilitaka kuuliza swali kama hili. Kwani ajabu hapo iko wapi? MoU ni makubaliano kuwa na uelewa wa pamoja kwamba Taasis fulani itatoa huduma fulani katika muktadha fulani na hapa kwa mfano, hizo taasis za "kanisa' zitatoa huduma kufuatana na makubaliano hayo. Serikali nayo imekubali kufanya mambo fulani kama namna ya mashirikiano.Hizo huduma kwani haziwasaidii wenye imani tofauti? Ni lini taasis zenu nyie mnaokereketwa na hii MoU zilikataliwa kusaini MoU na serikali?

Mbona Serikali ina saini MoU n akila taasis inayoshiriki katika kusaidia kufanya kazi au kutoa huduma? Mbona hamuulizi MOU za serikali na UN, Bilaterals kama NORAD, SIDA etc?
Au kwa vile hapa kuna "udini"? Hebu tuache mambo mepesi tujadili issues nzito.Huu udini unakuwa kama ajenda ya siri ya kuleta machafuko hasa ukizingatia wengi wa watanzania bado ni wageni sana wa modalities mbalimbali za namna serikali inavyofaya kazi kushirikiana na taasis zisizo za kiserikali.

Kama hujaona ajabu katika hilo basi hilo nalo ni tatizo.
 
Former President, Alli Hassan Mwinyi is in a better position to answer your question. Likewise, Benjamin Mkapa can tell us what really happened to the TANESCO College in Morogoro.

You amused me by your short but very clear reponse on this issue.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Tatizo ni kwanini Serikali imeingia makubaliano na Kanisa; kwa maoni ya watu inaonesha kuwa Serikali inapendelea makanisa. Kwa baadhi ya watu haijalishi kama mambo ya MoU ni ya kawaida au haijalishi kama serikali inafanya hivyo kwa taasisi nyingine hata ziwe za Kihindu au Kiislamu au mashirika mengine yasiyo ya kiserikali. Haijalishi. Tatizo ni kuwa kanisa limeingai makubaliano hayo. Na utaona kuwa watu hawataki kuangalia kabisa kuwa ilipofanyika Rais alikuwa ni Muislamu - hata hilo halijalishi.

Kuna msemo kwamba ni kujaribu kutengeneza kimbunga kwenye kikombe cha chai!
Huo ndio ukweli, kwani serikali kama ndiyo inayotoa pesa kwa hayo makanisa sasa inashindwa nini kusimamia yenyewe. na kumbuka slogan ya serikali yetu ni kuwa haina dini sasa kwanini isign mikataba na makanisa, je upande wa pili utalichukuliaje hilo?

Mwana Kijiji ni kama wiki2 sasa kulikuwa na post yako ya kuishangaa serikali kuuza UDA na watu waliochangia wengi walionesha kuishangaa serikali kwa madudu hayo. sasa leo kama kweli wewe ni mpiganaji wa dhati ambaye upiganaji wako uko based kitaifa, taifa ambalo halitakiwa kubase upande wowote wa dini unatakiwa hili ulichukie toka moyoni kwako na ukiona huwezi jua ni dalili za unafiki
 
Nimepita hapa, lakini naona tunalumbana bure tu. Tuanze kurudi nyuma na tuone chanzo cha mkataba kati ya Serikali na Wakristo. Ni jambo lisiloweza kupingika kwamba shule nyingi zilikuwa zimejengwa na wakristo. Wakati fulani ilibidi Baba wa Taifa kuzibinafsisha shule kadhaa kati ya hizo ili zisionekane kwamba ni wakristo tu wanaotakiwa kuzitumia. Zilipobinafsishwa kwa vyo vyote vile wakristo hawakujali lakini ieleweke kwamba zilijengwa kwa kutumia fedha za waumini walizokuwa wanachangia na zinaendeshwa kwa njia hiyohiyo. Kama ni hivyo basi uendeshaji wake pia unatakiwa kuchangiwa na wote wanaohusika. Serikali ndiyo ikaona waingie mkataba ili kuweza kuchangia kwa niaba ya watz. Tatizo liko wapi hapo jamani? Tunataka tusome tu bila ya kuchangia? Wengi wetu tumesoma kwenye shule hizo tena zamani zile ni bure kabisa. Sasa hivi tuchangie na hivyo ndivyo serikali inavyofanya kwa niaba yetu. Tusipende bure!
 
Tatizo siyo mou kati ya serikali na kanisa, tatizo ni nini kilichomo ndani ya hiyo mou!, je kilchomo kinavunja katiba au la?, mimi binafsi naona pamoja na vipengele vingi vizuri katika hiyo mou, lakini kuna kipengele kinavunja katiba ya nchi wazi wazi, kipengele cha serikali kulisaidia kanisa katika kutafuta misaada pindi inapofanya majadiliano na nchi rafiki hususan serikali ya ujerumani.. Serikali haipaswi kujihusisha na shughuli za kidini full stop!!!
 
Siyo muhimu sana kujua ni nani alisaini ila nini kilisainiwa na kwa nini walisaini.

Lakini pia serikali inawajibika kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake. Serikali iliposhindwa kutekeleze wajibu wake iliomba wanaoweza wafanye, kitu cha msingi hapa ni ukubwa wa mtandao wa huduma za jamii unaomilikiwa na shirika fulani. Uliza wilaya kama za Ludewa makete na nyingi za pembezoni utaonja umuhimu wa hudumu hizi za jamii zinazotolewa na makanisa. Ukiwa dar unaweza kuongelea Memorundum of Understanding kishabiki tu. Ukadhani haya makanisa yanavuna toka serikalini. Kwa kiasi kikubwa kifanyikacho ni serikali ku subsdize baadhi ya gharama kama zile za mama na mtoto. Lakini tukiongea bila kujua nini tunakiongea tutaipeleka Tanzania pasipo faa kisa tabia za udini na kufikiri baadhi ya dini zinabebwa. Ni fikira ambazo lazima ziwe backed up na knowledge ya kutosha la zivyo tutaipeleka nchi hii pabaya
 
Mbona hakuna mou serikali iliyosaid na dini za kijadi na humuulizi wala kushangaa! Au dini ni ukristu na uislam pekee?
 
Kisa cha Waislaam kuwa mstari wa mbele kudai Uhuru na kuwa Waanzilishi wa harakati za kujikomboa, kuanzia kina Tipu Tipu, MajiMaji, Mkwawa, Mirambo, Mareale, Bushiri, Sykes na wengine wengi, ilikuwa katika kupigania haki za Waislaam na kupinga elimu za kanisa zilizokuwa zinalazimisha uingie ukristo ndio upate elimu. Cha kusikitisha ni pale Nyerere alipowageuka Waislaam na kuendeleza yaleyale ya wakoloni Sheikh Suleman Takadiri akamwambia waziwazi nyerere "wewe ni mdini". Haikupita muda nyerere akadhihirisha udini wake baada ya kuivunja EAMWS na kuanzisha chombo chake cha kuua Uislaam kinachitwa Bakwata.

Alipokuja Malima na kubadili mfumo wizara ya elimu akawa adui mkubwa wa wakristo.

Leo Kikwete anabadili mfumo scientifically, hakuna kwa sasa asilimia 78 ya wakiristo kwenda sekondari kama ilivyokuwa kabla ya Kikwete, na anawekeza kwenye vyuo vikuu ili kuhakikisha mfumo kandamizi kwa Waislaam unamalizika. Kwa hilo. Kikwete ni adui mkubwa wa Wakristo kwani wabajua matunda ya Kikwete yataonekana baada ya muda si mrefu.

Mwinyi ni kipenzi cha Wakristo kwa unafik wake kama huu wa MoU na mengine na ndio maana tukaona anazabwa kibao mbele ya umma wa Kiislaam.

Wakristo leo hawana raha kabisa na Kikwete, kwanini? Kwa kuwa hafanyi mema? La hasha, ni kwa kuwa tu, anaua mfumo kristo scientifically na systematically kuanzia mashule na mpango kuchaguana mpaka misamaha ya kodi, na accessibility kwenye maeneo yenye Waislaam wengi.

Leo tunaona Kigoma, Tabora, Tanga, Kondoa, Mtwara accessibility inaongezeka kwa kuwekewa miundombinu mipya kabisa, hii ni mikoa iliyosahauka na awamu zote. Kwa hayo, tusitegemee hata siku moja "chaguo la Mungu" kuwa kipenzi cha Wakristo.

MoU tajwa ni moja tu kati ya muendelezo wa kukandamizwa Waislaam. Lakini Uislaam haufi, na hautetereki ndio kwanza inakuwa dini ya kwanza kwa kukuwa kwa kasi duniani.

Leo Waislaam ni wengi duniani kuliko wakatoliki. Kwanini? Kashfa za ngono na kuharibu watoto hususan wakiume kwa kanisa kikatoliki ni kawaida mpaka wikipedia wameweka page nzima ya hizo kashfa. Kanisa katoliki limeshahusishwa na mambo yote machafu duniani na ni ukweli usiopingika.
 
Former President, Alli Hassan Mwinyi is in a better position to answer your question. Likewise, Benjamin Mkapa can tell us what really happened to the TANESCO College in Morogoro.





jibu lako lomekwenda shule, nakuamniiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
1. MoU ilipo sainiwa raisi alikuwa Muislamu kwa hiyo aliridhia. Kama mnaona alishauriwa vibaya na yeye akakubali basi hiyo inaonyesha weakness ya Raisi Mwinyi. Pia kama mdau mmoja alivyo sema raisi anauwezo wa kuvunja hiyo MoU na hata Jakaya Kikwete nae ana uwezo huo wa kikatiba.

2. MoU kati ya kanisa na serikali si upendeleo kwa sababu taasisi za Kiislamu hazija zuiwa kuwa na MoU na serikali. Ni swala la wao tu kuongea na serijali.

3. Kama kweli Waislamu wanaona MoU kati ya kanisa na serikali ni haramu basi watangaze kwanzia leo kwamba hakuna Muislamu atakae enda kwenye shule inayoendeshwa na kanisa (kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu), hakuna Muislamu atakae enda kupata huduma ya afya kwenye hospitali yoyote inayo endeshwa na kanisa na hakuna Muislamu atakae tafuta huduma kwenye taasisi yoyote inayo endeshwa na kanisa. Kwa maana kupinga MoU na kwenda kwenye shule za kanisa na kutibiwa kwenye hospitali za kanisa ni unafiki mkubwa.

Swali: Je kwa nini kila raisi anapo kuwa Muislamu ghafla kuna ibuka baadhi ya Waislamu wanao jifanya kuwa watetezi wakubwa wa Uislamu? Raisi akiwa Muislamu basi asifanye kosa akakemewa maana akikemewa basi mtasema anasemwa kwa vile Muislamu. Kwa nini?
 
Back
Top Bottom