Naomba nijibu kipengele cha pili:
The government shall provide vacancies in its Teachers training colleges for training qualified persons as teachers earmarked for church owned schools. Article xi
Hapo nilipopigia mstari ni walimu makhsusi kwa ajili ya shule za kanisa.
Mkataba huo kwa sasa una miaka takriban 22, ni upi ukomo wake? Kama hivyo ndivyo kuna ajabu gani kwamba shule za serikali hazifanyi vizuri bali ni shule za kanisa? Huu ni ufisadi ambao hauwezi kumalizwa JF bali viongozi wa dini ya kiislamu, kanisa na serikali kukaa na kujadiliana. Kinyume chake ni maafa twendako.
Fresh,
Ukifuatilia majibu ya Mnyamahodzo na wengine utaona maswali yako 2 yamejibiwa kwa kina ila inaonekana sio majibu uliyoyataka.
Naomba nikufahamishe hivi ya kuwa ktk mikataba kuna vitu vingi vya msingi mbali na maandishi na saini ambavyo kwa pamoja huusababisha mkatana kutekelezeka na kueleweka. Moja ya kanuni za kutafsiri sheria na mikataba zinalazimisha kuheshimiwa kwa kanuni ya "Rule of Context". Huwezi kuchagua/kuchomoa sentensi fulani kisha ukaitoa nje ya muktadha na kuipa tafsiri au kutaka ipewe tafsiri kinyume na mwili wa mkataba.
Nijibu swali lako la pili, kama ulivyosisitiza hapo juu kwa kupigia mstari. Nitaenda kwa urefu kidogo.
Kanisa lilikuwa linakubaliana na serikali ya Tanzania kuhusu namna ya kutoa huduma zilizotajwa na kujadiliwa kwa kina huko juu/nyuma. Kanisa kwa vile lina utaratibu wa kutoa huduma bora likasisitiza kuwa ubora walimu watakofundisha shule (zitakazoendeshwa na kanisa) lazima uheshimiwe na kutambuliwa. Hivyo wakaleta hoja mezani kuwa serikali itoe nafasi (wewe unasoma upendeleo) kwa walimu wenye sifa kupata mafunzo.
Wewe ulitaka kuwe na kitu kama hiki'
....earmarked for state (or) muslim owned schools' ndipo hisia zako zingetulia kidogo, sio?
Well, sasa kama Kanisa lingesema hiyo sentensi (nadhani ambayo wewe ulitaka iwe) je hiyo MOU ingekuwa ni baina/kati ya Serikali vs nani? i.e. offer and receivership. Kuwepo kwa hicho kipengele ktk MOU kunalazimisha kutambulika kuwa wakishahitimu wataenda wapi.
Kwa mfano Kanisa lingesema Serikali itoe mafunzo halafu lisiseme wakifuzu wataenda wapi, Serikali huenda ingekataa maana haikuwa na fedha za kutoa huduma mama husika sembuse kufikiria kutoa ajira mpya, kwani haikuwa na uwezo wa kifedha wakati. Kanisa liliweka bayana kuwa litateua watu wenye sifa na kisha litawapokea na kuwapangia kazi (ajira). Kanisa halikusema litapeleka watu wa dhehebu fulani tu, bali wenye sifa/uwezo ndio kigezo! Na hao wahitimu hawekuwa wanakwenda kufanya kazi kanisani bali mashuleni, hivyo dhana ya Kanisa kufaidika kama Kanisa ni dhaifu mno
Na kama hoja hiyo inakuumiza na kukuchefua hebu jiulize ni vipi leo inakuwa maelfu ya walimu wanahitimu kila mwaka ..... je ni % wanaopata ajira, hasa serikalini? Nadhani unaona bayana kuwa hoja yako inaelea hewani na kupotelea huko!
Kwa hivyo in context, ni kuwa Kanisa liliitaka Serikali iheshimu na kuwajibika kimkataba juu hoja muhimu ya ubora wa walimu kama sehemu ya utekelezaji wa MOU nzima. Jitahidi usisome zaidi ya kilichoandikwa.