Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Acha porojo kaka, pitia hotuba ya rais Kikwete kwenye baraza la idd kule Dodoma ndiyo utajua serikali inatoa kiasi gani cha pesa kwa kanisa kila mwaka. Utasutwa wewe.
I know what I am talking about. Serikali imetoa ahadi nyingi lakini fedha nduhu. Fedha nyingi zinazoendesha hospitali za makanisa zinatolewa na walipa kodi wa nchi za nje kama vile Ujerumani, na makundi ya kibinafsi kama vile Marekani. Serikali ya Tanzania imetoa ahadi tu lakini utekelezaji nduhu! Kanisute kaka! Na correction: serikali haitoi fedha kwa kanisa. Imeahidi kutoa msaada kwa taasisi za makanisa zinazotoa matibabu kwa raia wote wa Tanzania.
 
I know what I am talking about. Serikali imetoa ahadi nyingi lakini fedha nduhu. Fedha nyingi zinazoendesha hospitali za makanisa zinatolewa na walipa kodi wa nchi za nje kama vile Ujerumani, na makundi ya kibinafsi kama vile Marekani. Serikali ya Tanzania imetoa ahadi tu lakini utekelezaji nduhu! Kanisute kaka! Na correction: serikali haitoi fedha kwa kanisa. Imeahidi kutoa msaada kwa taasisi za makanisa zinazotoa matibabu kwa raia wote wa Tanzania.

Kaka kumbe umeamua kuanzisha ligi.
 
Acha porojo kaka, pitia hotuba ya rais Kikwete kwenye baraza la idd kule Dodoma ndiyo utajua serikali inatoa kiasi gani cha pesa kwa kanisa kila mwaka. Utasutwa wewe.


Tatizo lako unakuwa na majibu kabla hujaulizwa swali. Matokeo yake unajibu usichoulizwa. Suala si Serikali imetoa kiasi gani, bali serikali imetoa fedha kwa ajili ya nini? Hivi madhehebu yako yana hospitali gani ambayo inatoa huduma kwa wananchi na serikali imekataa kuingia nayo MOU? Au unataka serikali ikujengee nyumba ya ibada?

Hivi umesoma vizuri maelezo ya Dr. Slaa? Bugando Medical Centre na KCMC zilikuwepo hata kabla ya MOU. Ukiona akili yako ni nzuri mshauri JK, ambaye ni MUislam, asipeleke fedha kwenye hospitali hizo. Kwa taarifa yako JK atakuona umechanganyikiwa. Soma MOU acha kukurupuka.
 
Tatizo lako unakuwa na majibu kabla hujaulizwa swali. Matokeo yake unajibu usichoulizwa. Suala si Serikali imetoa kiasi gani, bali serikali imetoa fedha kwa ajili ya nini? Hivi madhehebu yako yana hospitali gani ambayo inatoa huduma kwa wananchi na serikali imekataa kuingia nayo MOU? Au unataka serikali ikujengee nyumba ya ibada?

Hivi umesoma vizuri maelezo ya Dr. Slaa? Bugando Medical Centre na KCMC zilikuwepo hata kabla ya MOU. Ukiona akili yako ni nzuri mshauri JK, ambaye ni MUislam, asipeleke fedha kwenye hospitali hizo. Kwa taarifa yako JK atakuona umechanganyikiwa. Soma MOU acha kukurupuka.

Wewe hujui lolote bora ukae kimya.
 
Mimi labda sijaelewa Slaa anatolea ufafanuzi kama msemaji wa kanisa au kiongozi wa chadema.Babu mbona unatuchanganya uko upande upi

Jaribu kutumia akili yako wewe babu alishiriki kwenye hiyo akiwa kama katibu wa kanisa embu soma kwa umakini usipende kulalamika kam mwanamke.
 
Acha porojo kaka, pitia hotuba ya rais Kikwete kwenye baraza la idd kule Dodoma ndiyo utajua serikali inatoa kiasi gani cha pesa kwa kanisa kila mwaka. Utasutwa wewe.

Sio KANISA mbulula wewe, serikali haina uwezo wa kulisaidia kanisa, ni kanisa ndio linaisaidia Serikali. Fedha zinatolewa kwa taasisi za kanisa na sio kanisa. Zile Hospitali zinaendeshwa na serikali na ndio maana umeona wakati wa mgomo hata wao waligoma, wameajiriwa na serikali na sio kanisa.

Hivi mtapata hasara gani kutumia akili angalau mara moja kwa mwaka? Mbona hamuendi kutibiwa Aga khan mnakimbilia KCMC?

Yaani wewe kwa akili zako unataka kutuambia kuwa muasisi wa kupinga MoU, shehe Bassalleh ana akili kuliko bunge lote? Akili zako zinafanana na hiyo avatar yako
 
Heshima yako mkuu. Naona umechambua vyema juu ya hii MoU. Mimi nimekuwa nikiisikia tu lakini nilikuwa sijaelewa undani wake. Mimi ni msikilizaji mzuri sana wa Radio Imani. Hii Redio imekuwa ikiiipigia kelele sana MoU. Sasa naona naielewa baada ya huu ufafanuzi.

Lakini umeanza kwa kuonyesha kwamba BAKWATA, TEC na CCT zilikuwa zishirikishwe kwenye mazungumzo. Baafaye hapo mbele tunaona BAKWATA imeenguliwa na zinabaki TEC na CCT. Nini kilitokea hapa?

BAKWATA haijaenguliwa, bali imeenguka automatically kwa kukosa hisa. Kama kikao cha kwanza cha wananchi kuzungumzia kuanzisha duka la mtaa kitahusisha wanakijiji wote zingatia kuwa cha bodi ya wakurugenzi kitahusisha wanahisa tu.

Ama ipo taasisi ya huduma ya jamii inayomilikiwa na BAKWATA?
 
La kuuliza ni je shule za kiislam hazikutaifishwa? Au hazikuwepo? Waarabu walichukua watumwa na pembe za ndovu wakasahau kuwekeza hapa nchini? Sasa wao walipeleka MOU ya kuomba mahakama ya kadhi au vipi? Maisha yetu tumeyaweka rehani kwenye dini?
 
cover.jpg


quote_icon.png
By Dr.W.Slaa


"Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo "
PENGINE WENGINE KUTOJUA KINGEREDHA KUNACHANGIA KUTUFANYA TUSIELEWE VIZURI.HEBU WENZANGU NISAIDIENI HICHO KICHWA CHA HABARI HAPO KWENYE MoU KINAMAANISHA NI MAKUBALIANO KATI YA NANI NA NANI KABLA YA UFANUZI WENYE BOLD NYEKUNDU.WASWAHILI HUSEMA ZA KUAMBIWA UNACHANGANYA NA ZAKO.
 
cover.jpg


quote_icon.png
By Dr.W.Slaa


Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.

Very good.
 
PENGINE WENGINE KUTOJUA KINGEREDHA KUNACHANGIA KUTUFANYA TUSIELEWE VIZURI.HEBU WENZANGU NISAIDIENI HICHO KICHWA CHA HABARI HAPO KWENYE MoU KINAMAANISHA NI MAKUBALIANO KATI YA NANI NA NANI KABLA YA UFANUZI WENYE BOLD NYEKUNDU.WASWAHILI HUSEMA ZA KUAMBIWA UNACHANGANYA NA ZAKO.

Watu nyie mna shida kweli. Soma maelezo yote ya Dr. Slaa halafu utajua ni kwanini makubaliano hayo ni kati ya kanisa na observer(Serikali) . Hivi ni nani aliyewaloga wenzetu vichwa vyenu?
 
Watu nyie mna shida kweli. Soma maelezo yote ya Dr. Slaa halafu utajua ni kwanini makubaliano hayo ni kati ya kanisa na observer(Serikali) . Hivi ni nani aliyewaloga wenzetu vichwa vyenu?
MoU nimeisoma yote Na Maelezo ya Slaa nimeyasoma yote na makubaliano kwa mujibu wa MoU Inaonekana ni kati ya makanisa ya upande mmoja na serikali kwa upande mwengine.ndo maana simply tu nikaamua kurejea kichwa cha habari cha MoU.labda kama alie andika hii MoU Kakosea na silaa aliyeshiriki ndo yuko sahihi.zaidi ya hapo nashauri ni bora kwenye hoja kama hii tukawa wakweli na wawazi zaidi kuliko kufanya ushabiki na kuegemea kulinda kundi moja ama jengine.tujadili mada;tusijadili watu.
 
Mudi follower wana akili hawana porojo kama wewe. Hivo hiyo ni aibu kubwa kuliko kiongozi kama DR Slaa kuthubutu kuja kutetea ufisadi huu wa MoU?



Ufisadi wa MoU uko hapa ambapo DR Slaa nasikitika hakuweza kutuelezea kwa undani:

The government shall provide vacancies in its Teachers training colleges for training qualified persons as teachers earmarked for church owned schools. Article xi

The government shall endeavour to include financial assistance for church run social services in its bilateral negotiations particularly with the Federal Government of Germany. Consideration shall be made during its bilateral negotiations with other donors. Article xiii.

Tatizo lako hapa ni lugha iliyotumika kwasababu sio tu ni ya kiengereza bali ni ya kisheria ambayo kama wewe si mwanasheria na ukijifanya unaelewa basi utakuwa mbishi tu maana nijuavyo mimi wanasheria hufundushwa tafsiri ya sheria.



 
PENGINE WENGINE KUTOJUA KINGEREDHA KUNACHANGIA KUTUFANYA TUSIELEWE VIZURI.HEBU WENZANGU NISAIDIENI HICHO KICHWA CHA HABARI HAPO KWENYE MoU KINAMAANISHA NI MAKUBALIANO KATI YA NANI NA NANI KABLA YA UFANUZI WENYE BOLD NYEKUNDU.WASWAHILI HUSEMA ZA KUAMBIWA UNACHANGANYA NA ZAKO.
Ni full magumashi
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti

Angalia huduma zitolewazo na hizo taasisi sio utafikiri mtu asiyekuwa na akili timamu,sasa hiyo bakwata inaisaidia nini jamii hadi ipate hiyo ruzuku?
 
Hapa unazungumzia "Tanzania isijiunge na OIC", jibu mbona unalo tayari? Tanzania haina dini, hamna aliyepinga hiyo OIC kuwajengea mashule na mahospitali, kwa nini mnataka Nchi kama nchi ijiunge na taasisi ya kiislamu? Ndiyo yale yale ya kutaka mahakama ya kadhi itambuliwe na katiba huku mmesharuhusiwa ninyi kama ninyi mzianzishe wala hamna aliyewazuia. Mbona mnangangania Tanzania! kuna siri gani hapa? Nchi kama nchi haina dini, period.

Sasa kama Tanzania haiwezi kujiunga na OIC kwa kuwa haina dini, mbona Tanzania hiyo hiyo inaomba misaada nchi za nje kwa ajili ya kanisa? Au dini ya Tanzania ni Katoliki?
 
Back
Top Bottom