kaka nakuskia sana unachokisema. Tatizo ni kuwa waabudi Mungu wa kikoloni, bila kujali ni wa Mungu yupi, bila kujali kuwa Mungu huyo anatangaza wema ama mauaji,....hakuna atakayekubali kuwa Mungu wa upande wake ndiye Mungu asiyetakiwa na kuwa Mungu wa upandewa pili ndiye Mungu anayetakiwa. Kila mmoja atashkilia kwa nguvu zake zoooooooooooooooooooote kuwa Mungu wake ndo Mungu sahihi, na atakusomea kwenye vitabu nyao kukudhibitishia hilo!!
ukijaribu kufikiri kidogo nje ya boksi utaona kuwa ukweli ni kuwa hawa wote hawana Mungu(if there is one by the way) wao, ila ni wafuasi wa Mungu wa watu wengine kutoka huko uarabuni. Ni Mungu anayezunguka duniani kunyang'anyana wafuasi, ni Mungu wa wafuasi. waafrika wamemwacha Mungu wao, ambaye hana haja ya kupigania wafuasi na wala hana makundi, wamemfuata Mungu Mpigania wafuasi. Waafrika wamemwasi Mungu na sasa Mungu anawaadhibu - mtoto anamchinja mama yake, mama anamchinja mumewe nk nk. Mtu ukishapoteza asili yako ni kama vile haupo tena, you becabe a nonsensical.
Lakini si kuwa dawa haipo, dawa ipo nayo ni waafrika kujitambua wao ni kina nani. KUtambua kuwa, kaMa wewe ni mmatumbi ni mmatumbi tu huwezi kugeuka kuwa mwarabu kwa kujifunga kilemba, huwezi kugeuka kuwa mzungu kwa kuvaa tai, mmatumbi ni mmatumbi tu hadi kufa.