Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Kwani lazima watangaze utalii,wangeweka pichaya lissu tu
 
Hapo kwenye kutumia wanasiasa kuitishia sportpesa ndo umeongea,na si ajabu washafanya hivyo coz jamaa huwa hawashindwi kupindisha sheria alimradi lao liende.

Ila siku jakaya akienda zake jamaa watapata tabu sana,coz anawakingia kifua sana yule mzee,hususani kwenye mambo ya hovyo hovyo ambayo yeye mwenyewe ni master wa mambo hayo.
 
Haujanijibu swali langu, kwanini sportpesa aweke vipengele vya bonus kwenye mashindano mawili tu ya ndani wakati inashiriki michuano ya kimataifa pia? Je mashindano ya kimataifa haiyahusu sportpesa?
Bonus ni kitu kidogo sana kwenye biashara au mkataba

Ni kitu ambacho kinatolewa kwa mapenzi kama motisha kuku encourage ili ufanye vizuri au hufanywa hivyo kama kivutio wengine waweze kuingia deal na hiyo kampuni

Bonus sio kitu cha lazima

Kwa upande mwingine ni kwamba SportPesa waliweza kusaini deal la mkataba na Yanga bila kuweka hizo bonus na bado wangeendelea kuhesabika kama wadhamini wakuu.

Na ndio maana ukiangalia katika mkataba waliokubaliana SportPesa na Yanga ilihusisha bonus ya ligi kuu na ASF, lakini hakukuwa na makubaliano yeyote ya maswala ya bonus kwenye mapinzduzi cup and still Yanga walivaa jezi yenye nembo ya SportPesa

Hiyo ni kwasababu

portPesa kanunua jezi, haijalishi ni mashindano gani Yanga anacheza lazima logo ya SportPesa iwekwe kiifuani, vinginevyo ni mpaka SportPesa mwenyewe aridhie
 
Mapinduzi sio mashindano ni bonanza, tuzungumzia mashindano yanayotambulika. Kwanini aliweka kipengele cha bonus? Na kwanini aishie bonus kwenye mashindano mawili tu? Mapinduzi sio mashindano aisee.
 
Yanga wametoa tamko, wamesema walimuomba Sportpesa ruhusa, sportpesa hakuwajibu
Hawajasema hakuwajibu. Wamesema walikubaliana ndio maana wanashangaa kuona malalamiko mitandaoni
 
Mkuu CUF tena?? Lipumba atakutafuta
 
Sheria inawabana kuanzia makundi. Uzamini wa caf unaanzia makundi
Wewe itakuwa umebadili username. Kuna jamaa anaongeaga kama wewe ni mbishi kama shida zangu.

Kuna mnaosema Sportpesa hana mamlaka na Yanga kwenye mashindano ya CAF, mnakumbushwa mbona Yanga alikuwa wanavaa nembo yao kwenye hatua za awali, unarudi kuongelea sheria za hatua za makundi kama vile hakuna anayejua kuhusu sheria za CAF. Swali ni kama Sportpesa hausiki mashindano ya kimataifa kwenye mkataba na Yanga, mbona walivaa nembo yao hapo kabla?

Acha ubishi dogo.
 
Mapinduzi sio mashindano ni bonanza, tuzungumzia mashindano yanayotambulika. Kwanini aliweka kipengele cha bonus? Na kwanini aishie bonus kwenye mashindano mawili tu? Mapinduzi sio mashindano aisee.
Mapinduzi ni mashindano sio bonanza

Kuhusu bonus nimekuambia hiyo ni hiari ya mwekezaji na kwamba hata katika hayo mashindano unayoyatambua bado ingewezekana Yanga kusaini mkataba na SportPesa bila kuwepo kwa hizo bonus
 
Leta hapa huo mkataba tusome mbona mnaficha
 
Acha kukaa vijiweni nyie ndio wale kila kitu mjini ni cha Riziwani
 
Kama wanahusika kwanini walipendekeza timu ivae visit Tanzania? Kwanini wasingekomalia timu ivae hiyo hiyo sportpesa kifuani?
 
Kweli upo serious unajumisha mapinduzi cup kwenye mashindano? usha wahi ona mashindano mchezaji anaweza cheza bila kusajiliwa? naomba unitajie qualifications za kucheza mapinduzi, upgrade your IQ please
 
Hivi unafikiri Yanga walikuwa wajinga kupeleka ombi kwa Sportpesa kuona kama wataruhusiwa kuweka mfadhili mwingine?

Unajua ile Visit Tanzania kwenye jezi ya Simba iliwekwa kwa idhini ya Sportpesa na sio maamuzi ya Club?
Haya mambo sio rahisi kuyatolea ufafanuzi kwa sababu iyo mikataba yenyewe hatujaiona ni vyema mkataba ukawekwa hadharani ndio tujue nani yupo sahihi ila hapa yanga na SportPesa kama organizations tofauti lazima kila mmoja atatoa maelezo ya kujijitetea aonekane hana kosa ivyo ivyo kwenye suala la feisal ulilokua unaunga mkono kilichofanywa na feisal sio sawa kufanya ivyo kwa kuangalia mistari miwili ya mkataba iliyovujishwa mitandaoni wakati mkataba una kurasa zaidi ya 5. Uwekwe kwanza mkataba wote hadharani, iwekwe hadharani iyo document ya yanga kwenda sportpesa kuwajulisha wanaweka mdhamini mwingine, ziwekwe wazi taratibu za mikataba zinasemaje kwenye mashindano husika hapo ndio tutajua mbivu na mbichi. Binafdi sijasema kwamba yanga haina kosa ninachojaribu kusema tusitoe hitimisho kwa kusukumwa na hisia za kishabiki maana nina uhakika kabisa hiki jiki kilichofanywa na viongozi wa yanga na mashabiki wa simba wanapinga kingefanywa na viongozi wa simba basi mashabikihao hao wa somba wangetetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…