Mkataba wa Yanga na Sport Pesa waingia mdudu baada ya Yanga kutambulisha mdhamini mpya

Mi kweli tishio la backlash ya mashabiki wa Yanga inaweza kuwafanya SportPesa kunywea hata kama kisheria wana madai yenye mashiko. Ila hizo ni mbinu za kihuni na siyo zinazotakiwa kufanywa na professional organisation.
Upo sahihi
 
Kipindi hiki wanatoa bonus kwa simba, je simba walivaa jezi za sportpesa?
 
Uuzwaji wa jezi atayeathirika ni GSM, na hii ni kama ana akiba ya jezi za zamani store, vinginevyo Sportpesa ataathirika endapo kama jezi ya zamani itapotea kabisa mtaani na kusababisha nembo yake isionekane popote.
Ni kwamba wapenzi wa yanga ni wale wale, anayenunua jezi mpya hawezi kuvaa ya zamani. Unajua demage yake kwa sportpesa inakuwaje mtaani?
 
Yaani unakaa unajiuliza hawa jamaa kichwani kuna kitu, yaani sportpesa aweke mkataba ambao hauwaruhusu kwenye mashindano ya CAF kwa sababu ya muingiliano wa kimasrahi na kampuni nyenzie. Najiuliza kwa mfano ikitokea mwakani 1X bet wakiondoka wakadhamini cocacola yanga watawazuia sportpesa kukaa kwenye kit yao?
 
Inaathiri kama mwaka jana na juzi, lakini ile visit tanzania ni mapendekezo ya sportpesa kama walivyopendekezewa yanga na kukaidi, visit tanzania haina masrahi kibiashara, sportpesa anaweza toa eneo lake kama zawadi kwa nchi sio kwa kampuni ya kibiashara. Suala la msingi ni kuwa ilo eneo ni la sportpesa hivyo wanahaki ya kulalamika kama hawajaridhika
 
Kipindi hiki wanatoa bonus kwa simba, je simba walivaa jezi za sportpesa? View attachment 2502942
Sijazungumzia kutovaliwa kwa jezi bali nimezungumzia sportpesa kuishia kutaja tu bonus kwa Yanga katika mashindano mawili tu ambayo ni Azam federation na NBC premier league pekee kwenye mkataba wa wao na Yanga. Kwanini hawakuweka na bonus watakayotoa kwa Yanga endapo watafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa?
 
Tusitete upuuzi wa viongozi Kama huu, tunamlalamikia fei kuheshimu mkataba vipi sisi timashindwa kuheshimu mkataba wa sportpesa?. Tusiww wapuuzi kiwango hiki haifai na ni ujinga kuona viongozi wanakiuka mikataba na kuwatetea.
Wamekiuka mkataba sehemu ipi? Ulete basi tuuone walipokiuka
 
Mwenzio kaandika kampuni gani na wewe unaandika kampuni gani? Unavoambiwa pikipiki boxer ni Mo unazani anazalisha yeye? Dealer wa boxer tz nzima ni Mo
Umedandia mada

Jamaa alieandika (Hair ni GSM ) na ndo nikamjibu hapo juu sasa hayo ya mo boxer yanahusiana vipi
 
Viongozi wa sasa wa Yanga SC wanapenda Kukurupuka na wanachokiwaza muda wote ni Kushindana na Simba SC ( hasa katika Masuala ya Nje ya Uwanja ) wakati Kiuhalisia huwa Wanaharibu na inawagharimu Kiuchumi na hata Kiufanisi. Sifa zitawaponza kama Klabu.
 
Sasa utavaaje visit Tanzania wakati utaishia kuburuza mkia?
We jamaa una akili mgando ndo maana Tz ni maskini wenye akili kama zako ni milion 60!
Yaani hata Yanga ichukue world cup bado utasema ni bahasha!
Hata tuwapige Makolo fc mara mia utasema ni hujma! Hivi hukuona Al Hilal walijiangusha dkk 80 Sasa utawafungaje na mpira Hawataki uchezwe? Hivi hukuona waarabu tuliwapiga kwao?
Hivi huoni possessing football ya Yanga Huwa unakuwa wapi?

Hii Yanga ingine boss unbeaten team! Amka!
 
Wewe ndio tahira kabisa,unaongelea Al hilal Kulala dk 80!!! wakati mechi ya kwanza mlikuwa mnarukaruka kama vyura uwanjani. Manara alishamaliza huko wenye akili wapo wawili na wewe haumo
 
Yani kisheria Club ilipaswa kumshirikisha main sponsor kwanza na sio kama ilivyofanya Club, kwamaana kwamba jezi mpya yaweza valiwa zaidi kuliko yenye main sponsor mwisho wa siku ikawa biashara kichaa kwa main sponsor. Hili jambo sio jepesi kama wengi mdhaniavyo, SP kaweka pesa nyingi halafu anashindwa kuheshimiwa. Yaan kwa mfano mdogo tu, upange chumba/fremu kwa miaka 5 kwaajili ya biashara ya pombe na ulipe kodi yote kwa muda huo wa miaka 5 na kukubali kama kutatokea ongezeko lolote utalipa, lakini baada ya mwaka mmoja mtaa huo wakapiga marufuku uuzaji wa pombe kwa muda wa mwaka mzima, ukaamua kuicha fremu yako wazi mpaka watakapo ruhusu ufanyikaji wa biashara yako, sasa katika hiko kipindi cha mwaka mzima biashara yako inakuaimesimama ukute mwenye fremu amempangisha mtu mwingine kwa muda huo wa mwaka mmoja bila kukushirikisha eti kwakua wewe haufanyi biashara kwa muda huo na ni zuio la kisiri kali eti siyo yeye mwenye fremu.
Kuna jambo pale klabuni pale halipo sawa hasa kitengo cha sheria.
 
Mkuu umenena vyema. Binafsi nahisi Kitengo cha Sheria katika Klabu ya Yanga kina walakini.
 
Mbona taarifa ya Sportpesa imeandika kabisa kua iliwataka watumie visit Tanzania?

Kwahiyo katika mfano wako hebu rekebisha Ili ulete maana nzuri.
 
Sportpesa hajalazmisha yawekwe maneno mengine ...lile eneo ni Mali ya sportpesa linatakiwa libaki plain..ikibidi wameshauri labda vitangazwe vivutio vya nchi sio kuweka biashara ya mtu mwingine ..
VISIT TANZANIA NI TANGAZO LA BIASHARA AISEE. NI TANGAZO LA KUVUTIA WATALII NA WAWEKEZAJI.

VISIT RWANDA KAFAME ANAILIOA ARSENAL MAPESA MENGI.

YANGA WASHAKUNJA 1.5B mengine yatapita tu!!
 
WIZARA WATAFUTE TIMU ZAO.. wanalipa mishahara au wanasajili???

Toa huu upuuzi.. Kwani mbona Royal tour walilipa.

Hakuna cha bure bhana,

Yanga wameshakunja 1.5 B ya Haier ukijumlisha na ile ya CAF ya makundi. Pesa ndefu

Mengine haya mbwembwe na yatapita.

Sportpesa wasuse na wavunje mkataba sisi tutaendelea. Yanga ni kubwa kuliko wanakamari hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…