Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

- Mke sio ndugu yako.

- Life partiner ni mtu mnaesaidiana katika maisha, yaani shida zako azione kama zake na zake uzione kama zako.

- Mke asiyeelewa shida zako tayari amesha jiondolea kigezo cha kua life partiner wako.

- Hakuna reward kwa mtu mbinafsi, na kama ukimruhusu mke apite iyo njia basi madhara yake yatakuathiri wewe mwenyewe au hata watoto wako pia.
 
Ukichangia mwanamke aondoke wewe ndo unaenda kuishi kwenye familia ya jamaa yako upike na utimize majukumu yote? Yaani mwanamke aondoke aache wanae kisa huyo mtoto?

Ndiyo kwa maelezo inaonekana mwanamke ana roho mbaya ila sisi hatujamskiliza upande wake! Usijifanye mwema mwambie rafiki yako arufishe mtoto kwao. Au mtoto aletwe kwako tuone kama mke wako hatokulaza kwenye banda la kuku.
 
So amfukuze mke wake nyie mtaenda kulea wanae? Mnajifanya wema amfukuze mke wake nyinyi mko na wake zenu mmewakumbatia yeye aanze kulala bar.

Usitowe hukumu bila kusikiliza upande wa pili.
Mimi sina roho mbaya sitoweza kuwa na shida na ndugu wa mme ila ndugu zangu hawawezi kuja kuishi kwangu, niko tiyari kumsaidua akiwa huko huko ila sio kuja kwangu kuishi spendi maneno ya ndugu.

Mwanaume akipenda alete ukoo mzima kwake waishi ila ndugu zangu nooooo waje watembee warudi nyumbani.
 
Mimi nilishajiwekea utaratibu.. nitawasaidia ndugu wakiwa huko huko walipo biashara ya kujaza ndugu/watoto wa ndugu nyumbani kwangu ndio mwanzo wa kuharibiana michongo kila mtu akae kwake.. dunia ishakuwa mbaya nyakati hizi.
 
Ila ifikie wakati mtu kusaidiwa iwe huko aliko na si kumleta nyumbani kwako. Labda itokee wazazi wote wamefariki. Kuna shule za boarding unaweza kumpeleka mtoto na kugharamia kila kitu na likizo anaenda kwa wazazi au mzazi aliyopo.

Hii inaleta changamoto sana kwenye familia maana tunaishi kwa mipango sasa mmepanga kuwa na watoto wawili au watatu mnaletewa wengine tena.

Mimi binafsi natoa sana msaada ila huku huko uliko

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Huyu ndio wa kwanza kuishi nae ila anadai aliwahi kuishi na mtoto wa ndugu wa mke sasa hivi yuko chuo. Kuhusu tabia za mtoto hakuna malalamiko hayo
Huyo mtoto arudishwe kwa wazazi wake na huyo mwanamke siku ndugu zake wakikanyaga kwake awa timue mara moja bila kupepesa macho.
 
Ila baadhi ya wanawake wana roho mbaya sana kwa ndugu wa mume daah. Hapo soon atakuja mtoto wa ndugu yake na ataona ni halali kuishi nae hapo



Sana yani [emoji24]

Halafu atashangaa mtoto wake au wanae watakavyomsumbua mpaka ajute!

Choyo tu hapo hana lolote [emoji57][emoji19]
 
Wengi mnafurahisha sana! Hii kitu ni ngumu sana. Sijaona familia iliyosaidia ndugu akaondoka (baada ya mission completed) kwa kuishukuru. Mwisho wa yote huwa ni lawama tu.

Mtoto umejizalia mwenyewe akikua anakuita mchawi. Anakuua refer case za rombo, moshi mjini na hii ya kwimba ya juzi juzi.

Hivi humu ndani mnajua maana ya ndoa nyie? Unadhani ndoa ni mbususu? Ndoa unatafuta Rafiki wa ukweli, msaidizi wakati wa shida; mtu wa kukufichia madhaifu yako, mtu wa kukufariji etc,

Ndo maana Mie namchumbia To yeye ili Watoto awapeleke kwa Depal ili gharama ziwe kwa Demi na Antonnia awe Mchepuko
 
Mkuu amua kama mwanaume kama kweli huyo mke yupo tayari kuachana na wewe sababu ya huyo mtoto mwambie mtoto lazima muishi naye kama anaondoka aondoke


Kabisa, ningekuwa ni mimi ndie huyo mume wa familia ningekaza kama noma na iwe noma [emoji123]

Aondoke kama anaondoka huyo mwanamke.

Eti sababu ya choyo ?! [emoji848]

Halafu ukute anajifanya kusali kama ni kanisani yuko mbele mbele kumbe moyoni amejaa makorokosho ya choyo na chuki.
 
Mkuu uwezi kujua kapitia manyanyaso gani hapo alipokuwa ana lelewa
 
Ataamua yeye sio mimi, kwangu naishi na watoto wawili wa ndugu zangu na mmoja wa mke wangu, mimi binafsi siwezi kukataa kusaidia ndugu sababu mke wangu hataki.

Niliwahi kuwa na mtoto kabla ya ndoa mwanamke alikuja kunitupia nyumbani nikiwa likizo baada ya kusikia nataka kuoa, huyo mtoto alitunzwa na mama yangu mdogo hadi nilipooa ndio nimemchukua.

Mnaposema mtoto aondoke asaidiwe akiwa huko, je kama msaada wenyewe ni malazi?!
 
Mimi binafsi niliwahi kuishi kwa ndugu sababu ya umasikini wa baba yangu na si kwa matakwa yangu nilikuwa mdogo lakini nakumbuka mengi siwezi kuruhusu mtoto wangu akaishi kwa ndugu kamwe ila tu kwa kulazimishwa na hali ikiwemo kifo.
Mkuu sababu ulizozitaja kukusababisha wewe kuishi kwa ndugu, ndiyo hizo hizo hufanya watoto wengine kulelewa na ndugu.

Katika kulea kijana, kina mama wengi ni katili sana katika malezi hadi unashangaa.

Muda wa kumlea kijana huwa ni mfupi sana, maana akimaliza shule tayari mnaachana naye.

Lakini unakuta anafanyiwa matukio mpaka mtu unajiuliza faida yake ni nini!
 
Msaidie umpeleke kwako maana una familiya ndogo.atalala hata seblen.
 
angekuwa anamsomesha sijui ingekuwaje
 
sahihi kabisa mkuu, maranyingi hawa watoto hawapendi kukaa kwa watu ila hali huwasukuma na maranyingi wanawake ndio huwa vikwazo angalia hata kwa wadada wa kazi.
 
Huyo jamaa itakuwa ni yeye, eti ufukuze mke kisa unaforce ukae na ndugu ambaye wazazi wake wapo.
Sent using Jamii Forums mobile app


Hapana nazani tafsiri ya hicho alichofanya huyo mwanamke kina mapana na kina kwa mwerevu ndio maana maamuzi ya kukubali aondoke kama mwenyewe alivyoanza kutaka iwapo mtoto hataondolewa.

Hiyo ni indication tu lakini hiyo mwanamke si mtu mzuri.

Anaweza mzuru hata huyo mumewe.

Sasa Kwanini ikawe na mtu wa mashaka ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…