Mke wangu amesema kwasasa hayuko tayari kuzaa, kuna mambo yake anamalizia kwanza

Umesema Ukweli huyo atakua alitoa mimba nyingi sana kwahiyo ameamua kusogeza siku mbele ili asionekane anachelewa kubeba mimba, Vijana tunatakiwa tuoe Mabinti wadogo chini ya umri wa miaka 24.

Kuoa wanawake watafutaji/wanaosoma madegree ya juu hawawezi kukubali kuzaa hadi wagraduate
Nafikiri mtoa mada angetua mbia na upande wa ulimu/utafutaji...
 
True kabisa mie nasaka mrembo tuoane tuenjoy mie sitaki mtoto kabisa najijua nilivyo watoto watateseka tuu.
 

Mkuu pole sana kuna udhaifu unaonesha.

Nakushauri tafuta mke sahihi uoe, huyo ni mwanaume mwenzako (mwanamke aliyekuzidi akili). Inawezekana ameshakupima kwenye mambo mengi na umeonesha udhaifu. Makinika usije ukawa baba mlezi kwa huyo mkeo.

Lengo la kuoa ni kuanzisha familia, familia ni BABA, MAMA na WATOTO. Hukuhitaji kuanza kujieleza kwa mkeo kwamba unataka mtoto.

Shinikizo kutoka kwa wazazi😳, Yaani wazazi wako ndio wanakukumbusha umzalishe mkeo???

Unapata mawazo gani? Kwamba ndani ya hiyo miaka miwili umemuweka vizuri mkeo wako Kila mwezi na hajashika ujauzito??? Sasa unawaza au huwezi kuzalisha?

Au kinachokupa mawazo ni maneno ya wazazi wako??? Na kwanini maneno yao yakupe mawazo wakati wewe ndio unaepanga mipango ya familia Yako???
 
Kwanini asimalizie mambo yake kwanza kabla hajaolewa, ndani ya ndoa hakuna democras Mkuu, kwenye familia msemaji na muamuzi wa mwisho ni Baba pekee, usilete mambo ya majadiliano yasiyo na msingi, yaani mambo yake ni muhimu kuliko wewe?
 
Mkuu polee sana kwa kipindi unachopitia. Yawezekana kuna technical mistakes ulizifanya. Mwanamke yeyote usimuoneshee madhaifu mapema kiasi hicho saivi ashakusoma. Ebu simama kama mwanaume bhn bado hujachelewa. Inawezekana pia upo vizuri kakosa namna ya kukucontrol kakuanzishia vitimbi kama hivyo. Usikubali akupangie muda wa kuzaa naye otherwise utalea watoto wa wanaume wengine
 

Unajua kwa wenzetu walio endelea muda wa kuzaa, Idadi ya watoto nk huwa yanajadiliwa kabla ya kufunga ndoa. Pengine watazaa mtoto mmoja au wawili, watatu nk na wapatikane baada ya muda gani. Huku Afrika ndio tunafikiri ndoa maana yake ni kuzaa chap chap.
UKIAMUA KUOA MKE MSOMI UJUE INA GHARAMA ZAKE!
 
 
Hii inafanya kazi endapo wote hamko tayari kupata watoto! Ila endapo mwanaume anataka kupata mtoto ni haki yake kupewa! Sasa kwenye hii situation mwanamke anasema kuna mambo yake anamalizia hivyo haijakaa sawa kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…