Mke wangu hanisalimii, anasema salamu ni wajibu wa mwanaume kwa mke au familia yake

Mke wangu hanisalimii, anasema salamu ni wajibu wa mwanaume kwa mke au familia yake

Mambo ya ndoa yana mengi sana kaka. Kupoteza hisia kwa mwanamke wakati mwengine husababishwa na sisi wenyewe. Mtu daily unamchapa matukio wife unategemea hisia zinatoka wapi? Ni vyema pia kujiangalia personally kama uko sawa, inawezekana hana hata mtu lakini tu amechoshwa na reapeted actions zinamtoa mchezoni. Jichunguze mkuu kwanza kabla haujapoint fingers. Communication is key, ikishindikana involve watu wenye hekima wamueleweshe kuna kujisahau pia. Ndoa ni kuvumiliana na kujifunza everyday.
Siyo kweli hujawajua wanawake mkuu, anaweza akakuchoka kwa sababu zake binafsi au shinikizo la marafiki zake
Wanawake ni very complex creatures, cha msingi ni kuwa na demu wa pembeni akuliwaze ama sivyo anaweza kukupiga tukio ukajiua
 
Mwanamke anayekupenda anakupigia simu mara nyingi with no reason kama chiriku full stop.

Huyo mkeo mtafutie mwenzie huko unakokaa kupunguza msongo wa mawazo. Ili upunguze masononeko. Sometimes haya majamaa/ ke ni kuya-treat rough tu
 
Dawa atafute demu wa kumliwaza otherwise atakosa motivation kwenye maisha na anaweza kuharibu kazi yake na ndio itakuwa downfall yake huku kwa demu very possible ana jamaa mwingine anampa kiburi
Haya mambo ndio yanafanya wanaume wanakufa mapema

Tena hiyo anafanya kwa kumheshimu wengine wanatangaza Kabisa kuoa mke mwingine na Wala hawafanyi kificho
 
Mkuu hapo suala sio salamu, tatizo kubwa ni kuwa mkeo hana mawasiliano na wewe labda kama kuna shida tofaut na hapo mpaka uwaze wewe kupiga simu au kutuma sms.
Hiyo hali inatokea pale mtu anapomchoka mwenzake na kuazisha mahusiano mapya.
 
Aslaam,
Niko na mke takribani miaka 10 Sasa ya ndoa yetu.

Bahati mbaya mda mwingi hatulali na kuamka pamoja, kutokana na harakati za kutafuta maisha.

Huaga natumia siku 5 za wiki kwenda mahala pakazi yangu na siku 2 za mwisho wa wiki kushinda nyumbani na familia yangu, japo mara nyingine ikalazimu hata hizo siku za wiki naweza kuwa nyumbani.

Ila chakushangaza ni hii tabia ya mke kutonisalimia pale anapoamka au wakati flani wa siku.

Nisimpo mpgia mim kumtakia Hali yake na yawatoto ndo basi imeishia hiyo.

Nimejaribu kumuulizia mara nyingi kwanin hanijulii Hali mwenzie hasa pale ninapokuwa mbali na nyumbani?, jibu lake ni kwamba mwanaume ndiye mwenye wajibu wakusalimia familia yake.

Mwanamke na watoto haki yao nikupokea salamu na kujieleza kuhusu Hali zao zilivyo Kwa siku ile.

Nimejaribu mara nyingi kuamka na kukaa kimya bila kumpigia, aisee siku inakatika kabisa hanipigii.

Hili limenishangaza na linazidi kunishangaza kwakweli, yaan mim sina mtu wakunijulia Hali nimeamka naumwa au mzima ni juu yangu.

Kwa wale ambao wameoa au wanakaa na mke hili jambo nikwelii??

Huaga wajibu wakusalimia ni wa mwanaume tu? Hasa pale mnapokuwa mbali na familia zenu?
Ukiona hivyo kuna mwamba anapewa salamu ulizopaswa kupewa wewe.

Halafu cha ajabu ukute jamaa nae anapiga kimya hata akisalimiwa.

Maisha hayapo fair kabisa. Anaekitaka kitu hakipati na anaekipata hana haja nacho.
 
Kama wiki inaisha haulali nae basi yuko jamaa anajipigia , huyo wife wako anamtumia meseji nyingi za mapenzi huyo jamaa, alafu huyo jamaa huwa anachelewa kuzijibu meseji za mapenzi za mke wako na mke wako analalamika kuwa huyo jamaa hamjali kama wewe unavyolalamika
 
Kama wiki inaisha haulali nae basi yuko jamaa anajipigia , huyo wife wako anamtumia meseji nyingi za mapenzi huyo jamaa, alafu huyo jamaa huwa anachelewa kuzijibu meseji za mapenzi za mke wako na mke wako analalamika kuwa huyo jamaa hamjali kama wewe unavyolalamika
Na huo ndio uhalisia mchungu wa maisha
 
Sio sahihi lakini ingependeza lama na yeye angeletwa hapa tumsikilize, inawezekana ana sababu za msingi😀
Mawasiliano ni jambo la pande mbili, yakishaanza kuleta shida ujue ndio kwisha habari.

Hiyo comment uliyoniquote imenishtua, nilichanganya naedit
 
Mmeshachokana
FB_IMG_1741238748490.jpg
 
Mawasiliano ni jambo la pande mbili, yakishaanza kuleta shida ujue ndio kwisha habari.

Hiyo comment uliyoniquote imenishtua, nilichanganya naedit
Kutokuwa na mawasiliano kuna jambo limesababisha.

Labda atuambie je ipo hivyo tangu amemuoa au ni tabia ambayo ni mpya?
 
Back
Top Bottom