Mke wangu kanipa wakati mgumu

Mke wangu kanipa wakati mgumu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, lakini nilihisi ana bwana wa pembeni, nikaanza kufanya uchunguzi, kweli nikafuma baadhi ya msg , ambaxo kwa tabia yake kwangu aliyonionesha kwa miaka hiyo tuliyoishi, niliona si kawaida.

Mbaya zaidi hizo msg alizokuwa anatuma kwa huyo bwana( siwezi kumwita hawara kwa sasa) ilikuwa ni kama yeye anataka mahusiano yaendelee, maana mwanaume alikuwa akimjibu kwa mkato tu.

Mke- kwema, kimya
Mume/ baada ya siku tano/- kwema nipo, sawa
Mke- mmm sawa hiyo vipi,
Mume/ safi
Mke — mvua tu

Baada ya wiki
Mume— mzima wewe
Mke—upo poa wewe
Kwema tu, hofu kwako,
Kimya jamani, naona umetupa jongoo na mti wake,
Jua kali tu ee utadhani limeshuka.

Mume, nipo , hujibu SMS zangu!
Mke— saa ngapi tena wewe ndio hujibu.
Mume—- hahahaa upo!

Mke— nipo kuzeeka tu ndio kumepamba moto.

Mume—- aaa baba ajambo

Mke—- yupo tu aliacha na kazi sasa hivi yupo tu nyumbani.,
Mume—/ poa

Mke tena baada ya wiki
Mke —Upo kaka, za uzima!

Mume— poa.

Baada ya kushindwa kuvumilia na kuepusha kuona maajabu zaidi, nimeamua kulileta hili hapa ili mnisaidie, mke wangu bado nampenda, lakini nataka nijue nini kinaendelea,

Swali je nimuulize au nivumilie kidogo.

Watoto tunao wanne na wana maisha yao.
Umeongea nae..??
Hamna mshenga..?
Hana wazazi..?
Kwa mtu mwenye watoto wanne kuleta mada kama hii humu ni kujionyesha ulivyo na mapungufu tu.
 
Lakini upendo utsendelea tena ndugu yangu kuishi na mtu wa namna hii,
Kumbuka nimeishi naye miaka yote hiyo kumbe slikuwa na mambo yske,

Nasikia uchungu sana kama ni kweli alikuwa ni malaya, nashindwa hata kuongea naye vizuri,

Kila akiongea naona ni tapeli fulani,

Lakini swali langu lipo palepale , je nimuulize?

Kama tumepita hapo, ushauri wangu, puuza tu Kaka, ila mweke vikao na Hakikisha amejuta sana.
 
Sasa mmeishi 30yrs, unatafuta nn kufukunyua ya sirini? Presha na stroke mnazitafuta wenyewe makusudi.

Em zeeka na huyo bibi plz [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miaka zaidi ya 30? Ina maana mna zaidi ya miaka 60? Tuseme mmeoana ukiwa kwenye 30's ina maana na uzee wote huo mnachepukana?
 
Back
Top Bottom