Greetings Wana JF!
Kwenye baraza hili la mawaziri, viongozi watano wametoka katika mkoa wa Pwani peke yake. Nimekuwa nikijiuliza ina maana mkoa wa Pwani una mchango mkubwa sana kwenye nchi hii, na ni "wachapakazi" sana au ina "viongozi wenye akili nyingi sana" mpaka wateuliwe kwa wingi hivi kwenye baraza la mawaziri?
Mawaziri na manaibu mawaziri walioteliwa kwenye baraza la mawaziri katika mkeka uliotoka hivi karibuni wanaotokea mkoa wa Pwani ni;
1. Selemani Said Jaffo - Mbunge wa Kisarawe ( Waziri wa Ofisi ya makamu wa Rais - mazingira)
2. Mohamed Omary Mchengerwa - Mbunge wa Rufiji (Waziri wa Utamaduni na michezo)
3. Abdallah Hamis Ulega - mbunge wa Mkuranga ( Naibu waziri mifugo)
4. Ridhwan Jakaya Kikwete - mbunge wa Chalinze ( Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi)
5. Omary Kipanga - mbunge wa Mafia ( Naibu waziri wa Elimu)
Kitu ninachojiuliza inakuaje kamkoa kadogo kama Pwani kanatoa mawaziri na manaibu mawaziri wengi kiasi hicho? Wakati kuna mikoa mingine mikubwa tu na yenye mchango mkubwa sana kwenye taifa hili haijatoa kabisa, na kama imetoa kiongozi ni mmoja tu? Kitu ninachokiona sasa hivi ni kuwa uongozi wa nchi hii unaegemea zaidi mikoa ya Pwani na Zanzibar. Ukihesabu viongozi wote waliopo kwenye baraza la mawaziri nusu wanatokea mikoa ya pwani ( Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Zanzibar)
Hii kitu haipendezi kabisa na haina afya kwa umoja wa kitaifa. Na inaonyesha kuwa Kuna kakikundi kadogo cha wanafamilia (Makamba, Kikwete, Mwinyi na Nnauye) na wapambe wao wa mikoa ya pwani ndo wanatawala nchi hii sasaiv na wanagawana madaraka wanavyotaka bila aibu.
#Acha ukweli usemwe
Nawasilisha