TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Sio madereva tu, Hata hao viongozi ni stupid vilevile.

Utakubalije kukimbizwa kama gazeti na wewe umekaa tu ume relax?

Au hao viongozi hawana mdomo wa kusema punguza mwendo?
 
Hakuna
Sidhani kama mnatenda haki mkisema hivyo. Watu wasio wakurugenzi ndiyo wenye haki ya kusafiri kwa magari na kupata ajali? Jambo la msingi ni kudai barabara zetu zijengwe kwa viwango na madereva na magari yawe ya viwango.
Hakuna Cha kujengwa Kwa viwango, barabara zipo vizuri ni kiburi tuu Cha madereva wa magari ya serkali pamoja na maboss zao, wanajionaga wakiwa barabarani kama vile ni Mali ya baba au mama zao kiburi Cha mavyeo Yao tuu,

Huwa wanakimbiza na kuendesha Kwa rafu sana, mfano ni misafara ya viongozi wakiwa wanapita mabarabarani gari zinakimbizwa as if Kuna mashindano, kiasi kwamba ikipata ajali gari moja zote zinakuwa chapati.

Haya ni mafunzo Kwa wengine, waache viburi na kujiskia, waheshim Sheria za barabarani wasione nchi hii kama ya baba au mama yao, wakumbuke Kuna kifo.
 
Sio madereva tu, Hata hao viongozi ni stupid vilevile.

Utakubalije kukimbizwa kama gazeti na wewe umekaa tu ume relax?

Au hao viongozi hawana mdomo wa kusema punguza mwendo?
Viburu vya tumbo kushiba na uwezo wa kurefusha kamba
 
Kifo ni kifo tu alisikika mheshima mmoja baada ya Ally.Kibao kufariki. Mungu uwaangazie mwanga wa milele na uwape stahiki dhao kwa matendo yao
 
R.I.P Home boy.
 
Mchina akiongea kiswahili na kukosea ni sawa kwa sababu hana option pale anapokuwa Tz. Sasa huyu ndugu yetu ana ulazima gani wa kutumia lugha inayompiga chenga wakati kuna kiswahili?
Atasema steshen zote za redio na television nchini zina majina mengi ya vipindi kwa lugha hiyo
 
Latra hawarusu basi la masafa marefu kusafiri kama halina madereva wawili.
Sheria ndivyo inavyosema. Je utekelezaji wake ukoje?? Usanii mtupu. Ukisafiri toka point A kwenda B na ukafika salama mshukuru sana Muumba wako.
 
Sikatai kuwa Tanzania uendeshaji ni mbovu sana na tena siyo kwa magari ya serikali tu bali ni asilimia kubwa ya madereva. Lakini kama unasema barabara zetu zina viwango vya kutosha, well, pengine siyo kosa lako kwani inawezekana hujaona barabara kuu za nchi zilizoendelea. Hata mimi nilipokuwa mdogo kijijini kwetu huko, nilikuwa nadhani wali kwa kuku ndicho chakula cha kifahari na ghali duniani kote.
 
Useless explanation! Kama umewahi kusoma kitabu cha Kusadikika cha Shaaban Robert basi utakuwa ulikutakana na watu wanaoitwa wasadikika ambao waliishi miaka mingi iliyopita, na walikuwa na mawazo kama yako. Kama hujui siku ya kufa ndiyo usichukuwe tahadhari na kufuata kanuni za maisha salama? Mbona ukiugua unakimbilia hospital?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…