TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Pole sana kwa kufiwa na rafiki yako mkuu !!

Mwenyezi Mungu ampe makao mazuri huko alikoenda ,amen !!
 
Waliopata bahati ya kutoondolewa kwenye ile mgomo pale UDSM kipindi kile cha Rais Mwinyi. Wengine tulirudia mwaka wakatutangulia kuhitimu.
Alikuwa mwanachama mtiifu wa kijani
 
Alikuwa mwanachama mtiifu wa kijani
Inawezekana, kwa umri wake pamoja na nyadhifa na majukumu yake unaweza kuwa sahihii. Pia kumbuka kuna wengine ni wanachama wa ccm ila hawahusiki kwenye mambo ya chama ata kulipia kadi ya mwanachama anashangaa tu analipiwa.
Tumempoteza mtu wise sana na mtu anaeamini katika kusoma vitabu ili kuongeza maarifa.
Pumzika kwa amani Eng. Gissima, homeboy Maswi pole sana kwa kumpoteza rafiki.
 
Baadhi ya madereva serikali waonywe waendeshe magari kwa umakini,wana vurugu za kutosha barabarani na mwendo wa kutisha hawa jamaa watamaliza watu.Wiki iliyopita kuna mmoja alinisababishia ajali kwa kunichomekea,nashukuru Mungu ilikuwa ya kawaida.Hawa watu wapewe onyo wajue hayo ni majeneza ya tairi nne wasipofuata sheria.
 
Hayo machuma waliyogonga si yanayatoboa tu hata kabla collision haijaisha
Kwa ushauri wangu viongozi wasipende kukaa kiti cha mbele karibu na dereva kwenye hayo ma Prado

Wakae viti vya nyuma

Hizo air bags hazina msaada sanaa huko mbele

Wasikae kiti cha mbele cha kushoto kwa dereva ni risky sana

Collision nyingi zibsishia mara nyingi kuua waliokaa mbele kwenye hayo ma Prado
 
ulitaka achukue tahadhari zipi mkuu? Wangapi wanachukua tahadhari lakini wanakufa tu? Hata wakati ukitembea unaweza ukajikwaa ukafa kifo ni kifo tu mkuu,huenda mkurugenzi alizoea safari za namna hii,lakini kwa bahati mbaya leo amepata ajari amekufa`

Tuongelee no reform no election haya ya kifo tumwachie Yeye atoaye uhai.
 
dereva hana makosa, alikuwa anaambiwa na bosi wake kuwa anawahi musoma so achochee moto kadri awezavyo. Na asipotii amri ya mkuu wake anapoteza ajira yake. Wapumzike kwa amani.
 
Kama umenisoma vzr mimi nimesema ajali huwa zina kinga na kinga yake ni kuwa waangalifu na kufuata sheria na kanuni. Mkuu, mimi sio kama namlaumu yeye, ila ni kuwa waliohusika wote kwenye ajali wote wakichunguzwa ni lazima kuna mmoja ana uzembe. Unaweza kuwa kwenye gari unafuata sheria zote na mwendo mzuri lakini akaja kichaa na lori akakugunga na kusababisha kifo, lakini unaweza kuona kabisa kuwa hapo ajali imesababishwa kwa uzembe wa lori.
 
Wapumzike kwa amani! Hilo lori ndio limetikiswa hivyo na hiyo V8? Walikuwa mwendo mkali sana?
 
Uzembe hufanywa na madereva either wa lorry or whatever !
Na kisababishi kikuu ni spidi kubwa over 100 km per hour !
Mengine yote ni Abracadabra tu !
Vijana madereva wa sasa hawayajali maisha kabisa kabisa lakini cha ajabu ni kwamba ni waoga wa kufa 🤣 !
 
mimi nilijua ni huyu dah nilishaagiza k-vant kubwa hapa kwa shangwe
 
Mwendokasi, mwendokasi, mwendokasi,
MWENDOKASI!,
Lini viongozi wataelewa kuwa mwendokasi unaua!
RIP Eng Nyamohanga na RIP dereva Haule.
 
Kusafiri usiku siyo issue.
Yes dereva anatakiwa kuwa mwangalifu zaidi.
Mbona mabasi yanafanya overnight trips.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…