Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa fidia kwa nchi masikini kwani viwanda vyao ndio vinatoa gas nyingi zinazoharibu ozone layer. Tena sio kwa kubembeleza ilibidi iwe ni lazima.
Kabisa unaamini Tanzaia inaweza kulazimisha hizo ncho zilizoendelea? Unaota?
We huoni mama Samia kila sentensi anaweka neno naomba
 
Nchi bila misaada haiendi ndio maana kina mwigulu walikuja na tozo za miamala mkaanza kulia lia, na ujue budget ya nchi 60% inategemea wahisani Sasa acheni kujilisha upepo serikali ikiongeza Kodi mtaanza kulia ka yatima jangwani.
Nchi kuendelea sio tozo Wala misaada Bali kutumia resources zake to the maximum
Tanzania ina kila aina ya rasilimali, itumie hizo kutoka hapa tulipo.
Kachukue mfano wa Singapore au China, alafu uje uone aibu tuliyonayo huku Africa.
 
Ndio ni aibu kuomba omba huku Nchini kwako umejaza Rasilimali Asili na Rasilimali watu za kutosha.
 
Nchi kuendelea sio tozo Wala misaada Bali kutumia resources zake to the maximum
Tanzania ina kila aina ya rasilimali, itumie hizo kutoka hapa tulipo.
Kachukue mfano wa Singapore au China, alafu uje uone aibu tuliyonayo huku Africa.
Na nchi zenye resources nyingi ni maskini maana hawana technology ya kuzitumia hzo resources kujitoa kwenye umaskini na hata Hali ya masoko inaamuliwa na wakubwa wa dunia unaweza kuzitumia hzo rasilimali ila kujitoa kwa umaskini ni ngumu maana unapangiwa Hadi bei ya kuuza bidhaa zako
 
Toa solution tufanyeje
 
Ninadhani kuhimiza wananchi kutumia majiko ya gesi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ingekua ni jambo la kujadili ndipo kuomba msaada wa kifedha.
Ni yale yale ya Maria Magdalena.Kama kuna uhaba wa mkate si wangekula keki?Kipato cha siku kwa watanzania wengi (majority wanaishi vijijini ni shillingi ngapi?)
Wana uwezo wa kutumia gesi.?Tuhimizane tusikate miti ovyo na tukikata mti tupande mti.
 
Kweli viazi mviringo ni vingi humu jukwaani.
 
Lini watanzania waliacha kujituma na kufanya kazi kwa bidii?!!!

Unaongea kana kwamba uko ndotoni vile......
Hivi unajua kuwa tanzania ndo nchi pekee ambayo wananchi wake wana muda wa kwenda kupoteza muda.[emoji57]
 
Nchi bila misaada haiendi ndio maana kina mwigulu walikuja na tozo za miamala mkaanza kulia lia, na ujue budget ya nchi 60% inategemea wahisani Sasa acheni kujilisha upepo serikali ikiongeza Kodi mtaanza kulia ka yatima jangwani.
Okay tozo bado zipo bakuli linatembea hadithi zilezile .
Lazima utambue maana ya umaskini kabla ya kupambana nao.
Kikwete hajui kwanini sisi ni masikini ndio maana ushauri wake ni kutembeza bakuli.
Wasomali wanakuja Tanzania kama wakimbizi lakini baada ya miaka kadhaa wanatajiriki formula ni ile ile geuzi rasilimali kuwa bidhaa ziinufaishe dunia uone kama hautikidhi mahitaji yako.
Hiyo ni kuanzia wewe binafsi hadi taifa sio kinyume chake
 
KAMA UNGELIKUWA WEWE NDIO RAISI UNGEFANYEJE?
 
Hatutaki Rais asiyekuwa na exposure, na muelewe wazi nchi hii haitatawaliwa tena na washamba.

Dosari za mama tunazijuwa tutadeal naye accordingly, lakini never again kukabidhi nchi kwa washamba.
HUU NDIO UKWELI
Ukitaka kuzuia uharibifu wa misitu ni lazima uweke mbadala wa matumizi ya cooking energy
Gesi inabidi iwe rahisi , na ili iwe rahisi utahitaji Ruzuku angalau kwa miaka 5 ya awali ili kuwapeleka watu kwenye kuzowea.
Vifaa vya Gesi viwe rahisi au vitoewe bure kwa angalau miaka 5 ya awali kwa wtu wa vijijini ambao ndio watumiaji wakubwa wa kuni na wa mijini watumiaji wa mikaa.
Mama anaomba Pesa za Kuliwezesha zoezi hili liweze kuharakisha uhufadhi wa Misitu yetu.
Bila ya hivyo sisi pekeyetu hatuwezi, utaidi usambaze Askari msituni kuzuia ukataji miti ambayo inahitajiwa kwa matumizi ya kila siku, hivyo haitawezekana mpaka upate mbadala.
Bakuli linahitajika lijae.
 
Rais kakumbushia utekelezaji wa Maazimio ya Paris. Mataifa makubwa yanayoongoza kuzalisha hewa ya ukaa, kinara akiwa China, US na Urusi na nyingine ziliji commit kutoa karibu Usd 100bilioni kukabilia mabadiliko ya Tabianchi.

Sasa kosa kukumbusha utekelezaji wa ahadi? Ina maana gani sasa kila mara viongozi wakutane halafu hakuna utekelezaji? Nilitegemea tumpongeze Rais wetu kawagonga wakubwa diplomatically...
 
Angetaja hata juhudi zilizo ndani ya uwezo wetu za upandaji miti basi ingetosha.

Wewe umeenda kwenye mkutano uwe sehemu ya suluhu halafu unaenda kutangaza njaaa1🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…