Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Large heads small brains!
 
Mkuu najua una uwezo ila si mahitaji yote unaweza kuyatatua kwa kiasili chote Cha pesa ulichonacho

Kwa kua wewe unaona Jambo hili Ni jema na linafaa....

Ukipata muda umtume mkeo kwangu nimuongezee pesa ili muweze kukamilisha Mambo mengine mliyobakisha,

Usije ukajali sana kuhusu kuchelewa kwake Cha msingi pesa unayohitaji itakufikia yote
 
Na serikali ingepunguza gharama za umeme Ili watu wajikite kwenye kupikia na kupunguza kutumia mikaa na kuanzisha kampeni za upandaji miti kitaifa, maana makazi mengi yanaanzishwa bila kuhiniza upandaji miti
Hili la kupanda miti ni muhimu sana, angalau kila kaya ipande miti kumi kwa mwaka.
 
Ni yale yale ya Maria Magdalena.Kama kuna uhaba wa mkate si wangekula keki?Kipato cha siku kwa watanzania wengi (majority wanaishi vijijini ni shillingi ngapi?)
Wana uwezo wa kutumia gesi.?Tuhimizane tusikate miti ovyo na tukikata mti tupande mti.
Kama gesi tunayo kwanini kusiwe na jinsi ya kupata bei inayowezekana kila mtu kununua au wakulima waweze kubadilisha mazao kwa mtungi wa gesi.
 

Litaonekana wapi ?!!
Atapongezwaje nasi kwa diplomasia hiyo KUBWA?!!

Sisi tumeamua KUPINGA TU....
Sisi tunaitwa PINGA PINGA FC.....

Wengine wetu ni kutoka CHADEMA🤣
Wengine wetu ni wafuasi wa akina ndugu komredi Polepole......

KAZI YETU NI KUMPINGA MH.RAIS SAMIA NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA 6....

ASEME KUBWA ASEME DOGO sisi ni KUMPINGA TU 🤣🤣🤣

Siempre SSH
 
Hiyo Sasa ni dhihaka ya KITOTO...UTOTO MWINGI...

Ya mke yanahusiana vipi na diplomasia ya kimataifa Kati yetu na nchi zilizoendelea?!!!!

FYI: Ukikua utajua kuwa mke anaweza "kuuza haki ya mwenza" bila ya "kutumwa na mumewe" ama bila ya malipo yoyote....yaani huduma ikawa BUREEE BUREEE...bureee kabisaaaaa🤣

Siempre SSH💪
 
Kama gesi tunayo kwanini kusiwe na jinsi ya kupata bei inayowezekana kila mtu kununua au wakulima waweze kubadilisha mazao kwa mtungi wa gesi.
Unaishi Tanzania kweli?Hayo mawazo ya ujima.Wakitaka mahitaji mengine wabadilishe kwa kutoa mazao?Wananchi walio wengi hawana uwezo wa kupata hata mlo zaidi ya mmoja kwa siku.
Anayenunua mazao kwa kubadilishana na gesi ni nani?Serikali?Halafu hayo mazao wanapeleka wapi?
 
Hapa ndio mnapojjchanganya
Mama Samia alipokuwa bagamoyo alisema wameweka tozo ili nchi ijiendeshe iache kutegemea mikopo ambayo inakuja na mashrti magumu
Kama mnasema hao matajiri wana pesa za kuleta huku basi ondoeni tozo
Wananchi sasa ndo inabidi tusimame kidete ili tozo ziondoke!
Alafu fedha za climate finance na adaptation fund ni nyingi. Na si za mkopo kama za maendeleo chini ya WB au IMF!
Mwisho MIMI siko huo upande wa waweka tozo...
 
"....wananchi walio wengi hawawezi kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku"?!!

Ni hukohuko vijijini?!!!

Huku mijini inajulikana sababu ni zipi....ziko nyingi mno......
 
"....wananchi walio wengi hawawezi kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku"?!!

Ni hukohuko vijijini?!!!

Huku mijini inajulikana sababu ni zipi....ziko nyingi mno......
Mkuu tembea vijijini uone hali halisi. Walio wengi wanaishi kwa dhiki sana. Hawana maisha ya uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku.
 
Wanaopinga wawe na hoja na knowledge ya kile wanachokipinga basi. Ndiyo ukomavu katk mijadala. Sasa yaani vikao vikao...kuongea..kuongea tu kila mwaka bila utekelezaji? Rais kawagonga kidiplomasia jamaa watekeleze ya Paris kwanza. Tunasema katuangusha? Hapana sasa, si sahihi na hatuipi heshima nchi yetu.
 
Mkuu tembea vijijini uone hali halisi.Walio wengi wanaishi kwa dhiki sana.Hawana maisha ya uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku.
Mkuu wangu hebu twende taratibu....

Katika Jambo kubwa na sumbufu aliloumbiwa mwanadamu ni UPATIKANAJI WA CHAKULA....

Ni uzito KUPATA chakula Cha kushiba....ni uzito pia KUPANGA RATIBA YA KULA/CHAKULA....

Mkuu wangu hivi unajua ni kwanini WAYAHUDI wanapoamka asubuhi basi jambo la mwanzo ni KUMSHUKURU M/MWENYEZI kuwaumba walivyo na kutoacha kuwapa MKATE WAO WA KILA SIKU??!!

Waislam hupiga dua za kabla na baada ya kula?!!

Wakristo huomba na kusali kabla na baada ya kula?!!!

Mkuu mambo ya vyakula ndani ya kaya ni zaidi ya Sera za SERIKALI....

Karibu kahawa na kashata hapa kijiweni....mchana huu 🤣🤣
 
Reactions: Tui
😍
 
Kenya wanahitaji mazao yetu ya chakula, huu ni mfano mdogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…