Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanaweza kuwa wazalendo zaidi ya wanaojiita wazawa
Hujui Africa kuna silaha wanapewa majambazi na kwenda kufanyia uharamia?
Wanaokula Rushwa maofisini ni kina nani?
Wanaobambikia kesi watu ni nani?

Kuna watu wanaiba hela za miradi mabilioni ila huoni wamefungua makampuni je umejiuliza hao wazawa wanazipeleka wapi hizo hela ?

Kama wana nia mbaya nazo unajuaje?

Leo mnabaguana mpaka mnawataja walioshika wadhifa tena kwa upendo wao kuingia siasa

Ni mmoja katika milioni ya wasomali ndio utaona kwenye siasa au General mwenye asili ya Rwanda au Zambia lakini babu zao walikuja miaka 100 iliyopita
Sasa kuna watu humu wengi sana asili zao sio hapa ila kwa kuwa ni wabantu hawajisemi kwa woga

Ila wenzetu mbona wanasema asili zao kama Biden ambae ni Irish?
Ila wabongo waoga kwanini
Kwani ukisema asili yangu Zimbabwe nani atakurudisha kwenu
Marekani na Uingereza si ni walewale tu lao moja kiutawala Dunia.Sasa sisi na Wanyarwanda na Warundi tuna malengo sawa?
Watutsi wa Kagame wao wanajiona ni superior race na kwamba wao waliumbwa kuwatawala wenzao(Tafuta Uzi wa Bahima Empire)
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024


CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."


Zis is serias!
Wanyarwanda na warundi bado wamo jeshini na usalama?
Nchi hii hatuko serious na usalama wa nchi!
 
Marekani na Uingereza si ni walewale tu lao moja kiutawala Dunia.Sasa sisi na Wanyarwanda na Warundi tuna malengo sawa?
Watutsi wa Kagame wao wanajiona ni superior race na kwamba wao waliumbwa kuwatawala wenzao(Tafuta Uzi wa Bahima Empire)
Hao nawajua sana na tamaa ya utawala, na migogoro yote tunajua, inawezekana CDF anajua ana maanisha nini ila kazuga tu na watu wamekurupuka na kuanza kumtaja Bashe ambae hata Somalia haijui
Wanaoongelewewa na kulengwa ni Bahima Empire ndio maana kuna uzi niliandika nikasema tunahitaji bajeti kubwa kwenye Ulinzi kwa sasa badala ya madege ya abiria tungenunua za kivita
Sasa tunajionyesha mbele ya hao hao kwa kuruka kutoka kwenye helicopter na kamba mambo ya kizamani na kubeba Manati what a joke 🤣
 
Uzur ni kwamba na wao wanafahamu hilo. Nilifikiria ni sisi tu hapa jukwaan tunapigizanaga kelele bure bila msingi. Kumbe inasaidoa na wao wanafuatilia
Kati ya vyombo vyote, naliamini JWTZ kwa uzalendo toka moyoni. Vyobo vingine kwamuda mrefu vimetumika kisiasa.
Namuunga mkono CDF, kwa kulisema hili hadharani.
 

Hii CDF kaiweka wazi ili baadhi ya watu kwenye utumishi wa umma waone aibu na waache kupenda rushwa!

Baadhi ya watumishi wa umma hawana uchungu na nchi, wanawaza rushwa tu. Haya ya watu wasio watanzania kupata nafasi kubwa kama hizo ni matokeo ya rushwa tu.
 
Yaani,haya ndio maoni ya CDF! Anasema kuna watu wanapata uraia, bila serikali kujua!? Kuna ubaya gani, MTU kutoka Rwanda, Burundi, Congo, kuomba uraia? Au kwa vile ni weusi? Mbona wa Asia, wazungu,wapo kibao tu,? Kama jeshi, na taasisi zake za, intelijensia, hawana, tskwimu, na wala hawajuhi hao watu, basi, huyu jamaa, ni kilaza kweli kweli, yaani na jwtz na wao wanalalamika! Kuhusu, wakimbizi haramu! Ingekuwa jeshi lenye weredi, angesema, wamekamata watu 3000+walioingia kinyemera! Fucking stupid
Punguza mhemko. hajasema hawajulikani. Amesema wapo nchini kama waomba hifadhi na wakimbizi. bado utaratibu wa kupata uraia kamili haujafanyika au hata hawajaomba lakini wameingia katika ajira na wengine wamepenya hadi nafasi za maamuzi. Lakini pia mkimbizi au muomba hifadhi kupata uraia siyo haramu. Nchi hii ina wakimbizi wa tangu miaka ya 1970's, wananishi nchini na hawajapewa uraia rasmi. Kimsingi haowatu ni watanzania, hawawezi kuitwa wakimbizi maana wamezaa na wana wajukuu waliozaliwa ndani ya nchi.
 
Tumeandika sana tangu Jambo Forum (2006) mpaka hii leo Jamii Forum (2024), kuwa kuna raia wa nnje wamepatiwa pasi za Tanzania na wana vyeo huko serikalini,mashirika ya umma na taasisi za umma,lakini vyombo vya dola vimeweka pamba masikioni.

Kuna miaka ya 2010 hivi RSO wa mkoa fulani alipelekewa "dossier" ya mtu fulani mkubwa,akasema atafanyia kqzi,lakini mpaka leo huyo mtu yupo na nafasi kubwa tuu.

Hii inchi ni kama nyeti za kuku upepo uvumapo.
Ipo siku tutalia.
Pesa mwanaharamu
Mtu anaingia leo kesho ana kiwanda na anaajiri na ana ardhi anajenga
Lakini wengi wanapambana tu na maisha lakini wanapata vyote hivyo kutoka kwa wazawa waliokabidhiwa dhamana ya nchi kwa thamani ndogo

Wangekamata waliotoa vibali na passport na sio kinyume
 
Kati ya vyombo vyote, naliamini JWTZ kwa uzalendo toka moyoni. Vyobo vingine kwamuda mrefu vimetumika kisiasa.
Namuunga mkono CDF, kwa kulisema hili hadharani.
Na inawezekana they mean biznes kulisema hadharan maana wangeweza kuli communicate internally tu.. sasa kuliweka public inaweza ikawa ni message intended to be delivered kwa wahusika..either humu ndani au huko nje
 
Wamechukua hatua gani hadi sasa baada ya kugundua serikali ya ccm inawapata nafasi wakimbizi serikalini 🤔🤔
 
Back
Top Bottom