Umemaliza kila kitu!
Najiuliza, kwani ndege ilitua uwanjani au iliingia kwenye maji kwa kishindo?
Kama iliingia kwa kishindo, kuna uwezekano vyuma vyuma vikawa vimelegea na dogo aliweza kufungua mlango kwa nje!
Yote kwa yote jamani, dogo ni jasiri. Kitendo cha kuisogelea ndege iliyopata ajali ni ujasiri. Nani hajui ndege ikipata ajali inaweza kulipuka. Jiulize, ungekuwa ni wewe ungeisogelea kirahisi hiyo ndege na ungeweza kufanya hizo harakati alizofanya Majaliwa?
Majaliwa alienda hadi kwa rubani ili amuokoe ila ikashindikana. Huo ni ujasiri pia.
Dogo alipigwa na kamba kichwani akazimia, huu ni ujasiri pia.
Jiulizeni, wataalamu wangapi wa uokoaji waliwahi eneo la tukio na kuisogolea ndege?
Halafu inaonekana kuna kampeni inayofanywa na vyombo vya ulinzi kumshusha dogo kwa sababu wao walikuwa wazembe!