white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,566
- 13,770
upo sahihi mkuu,tena vile vindege vidogo vidogo,mlango wa abiria huwa unafungwa/kufunguliwa na mtu aliyeko nje.Inategemea na aina ya ndege.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
upo sahihi mkuu,tena vile vindege vidogo vidogo,mlango wa abiria huwa unafungwa/kufunguliwa na mtu aliyeko nje.Inategemea na aina ya ndege.
Kuna abiria mmoja alitepona alikuwa anasema kuwa,kuna mfanyakazi wa kwenye ndege ndiye aliyekuja kuufungua mlango na wao waliokuwa nyuma ndipo wakaanza kutoka.Mlango wa dharura una funguliwa kwa ndani nii manually,ila unahitaji nguvu kubwa kuufungua,hivyo hata kama ndege imezimika bado unaweza kufunguka ,Nimejiuliza sana bila majibu. Nadhani wahudumu wa ndege walifanya jitihada za kufungua mlango ndipo shujaa Majaliwa akasaidia kuunasua ama kuuvuta kwa nje maana kwa jinsi ile ndege ilivyokuwa mlango usingefunguka vizuri wao wakiwa ndani.
Mnahaha kweli kumshusha Majaliwa wa watuNaomba kuuliza kwa wenye uelewa. Hivi mlango wa ndege unaweza kufunguliwa kwa nje? Wajuzi wa mambo ya ndege tafadhali.
Na ukumbuke kwamba kama hakuna oxygen ya kutosha ndani milango inakuwa ngumu kufunguka.Kuna manusura alisema mudumu ndie aliyefungua mlango, hapa inawezekana mhudumu alifungua kitasa na aliyekua nje alifungua mlango, kwa aliyekua ndani ni dhahiri mlango ulikua mzito kutokana na presha ya maji, na muda huo pia akili za waliokua ndani ni tofauti na waliokua nje.
you are right majaliwa alifungua ule wa kushusha chini huku muhudumu akiangaika na huu mlango wa bafu huku [emoji52]Najua milango ya dharula kwenye ndege, inakua pia nyuma karibu na mkia, Kwa majibu wa muhanga mmoja, andai, watu wa mbele, walifunikwa na maji ila pia alimuona mhudumu akihangaika kuufungua mlango wa dharula.
Ila hajui kama alifanikiwa.
Hili lipo wazi mnoMimi suala la dogo kuwa kafungua mlango haliniingii akilini maana ni ngumu kwa nje kufungua
Ha ha ha dogo kawaokota watu mnoKwanza vumbi tu la udongo na maji yale ya Ziwani aliwezaje kuonana na Pilot? Ukizingatia tukio limetokea punde...
Ha ha ha dogo kapiga sound Taifa mpaka mkuu wa NchiAKA YA Majaliwa anakuambia mtaani anajulikana kama "Maja Mnyama." Dogo sound nyingi alafu hizo pesa anazopewa ingekuwa vizur angewapa na marafiki zake waliokuwa wote kwenye pirika za uokozi.
Majaliwa kachukuliwa kama mpango mkakati wa kutuliza tukio na kuficha uozo wa sirikali...SI Kuna wali Wahudumu wa Ndege Wasichana Wawili ambao Mwanzo tuliambiwa ndio Walisaidia kwenye kuongoza Abiria kutoka kwende...lakini Sasa Wameshauriwa Kabisa kama vile hawakuwepo! Mambo yote ni Bwana Mdogo Majaliwa TU.
Au Walinywa wake kimwa?
Walistahili nao Kuitwa Bungeni....!!
Mlango unafunguka kwa nje, kuna sehemu unapress. Labda majaliwa alipiga kwenye ile sehemu ya kupush ukafubguka kirahisiPunguzeni ujuaji. Dogo anasema baada ya kuupiga ule mlango kwa kasia ukafunguka, akaokoa baadhi ya watu then akazama majini akaenda kwa rubani. Rubani akampa maelekezo ya ulipo mlango wa dharura ambao ndio waloufunga kamba inayovutika.
Na ikumbukwe haikuwa emergency landing, ilikuwa inatua kawaida na si abiria au wahudumu walikuwa wametayarishwa kwa emergency landing. Na kukiwa na pressure kubwa ndani ya ndege sio rahisi kuufungua ule mlango kwa ndani kama hakuna matayarisho yoyoteMlango unafunguka kwa nje, kuna sehemu unapress. Labda majaliwa alipiga kwenye ile sehemu ya kupush ukafubguka kirahisi
Kasikilize tena, wale manusura walitoka nje na hakukuwa na msaada wowote mpaka ukapita muda kidogo ndio ukatokea mtumbwi. Hoja yako sio sahihi na hujasikiliza bali umesimuliwa, nenda kaisikilize tena.Kwa Kadri nilivyowasikia majaaliwa na wenzake na pia manusura wa ajali ni kwamba walipokuwa wanagonga mlango kwa kasia walioko ndani walisikia kwamba kumbe huko nje kuna msaada tayari, hivyo aidha mhudumu au baadhi ya abiria wakaenda kwenye mlango na kuufungua lock yake kwa ndani na mlango ukafunguka. Kuna clip ya jamaa mmoja aliyekuwa anaenda kikazi Tabora ila ikabidi wapande hiyo ndege yenye ruti ya Mwanza lakini kupitia bukoba. Huyu jamaa anasema baada ya ku recover from the shock of the accident na kuona maji yameingia ndani ya ndege na yamemfika kiunoni akasikia mhudumu akiomba life jacket ili aende kufungua mlango (nadhani ndiyo huo mlango akina Majaliwa walikuwa wanagonga na kasia). Basi jamaa naye akaamua kwenda hapo mlangoni maana ilikuwa jirani, na ndiyo wakawa wa kwanza kutoka na kuokolewa.
Kama alikuwa na mtumbwi basi yy hakufungua huo mlango, kwa maana walionusurika wamesema walifungua mlango na walipotoka hakukuwa na mtu wala mtumbwi wowote wa kuwapa msaada.Alikuwa na mtumbwi ambao alikuwa na wenzake 2 na yeye 3
Hawezi kwa maana kuna namna unakuwa LockedKwa hiyo akitokea chizi anaweza kuufungua ndege ikiwa angani?
Mm nimevua sana, Jahazi zetu zilikiwa zinaenda Mafia, Msumbiji, Kilwa nk. Nimeishi Mtwara na najua kasia ni nini na huundwaje, hakuna kasia la Chuma kwa mitumbwi hii yote ya kienyeji. Nimesafiri na meli za utafiti wa mafuta kule mtwara mara kibao.Umewahi kupanda mtumbwi? Unajua kasia lilivyo lakini?