Mliambiwa lakini hamkusikia, sasa ni muda wa mavuno ya awali ya kile tulichopanda

Mliambiwa lakini hamkusikia, sasa ni muda wa mavuno ya awali ya kile tulichopanda

Awww couldn't have said it better; May God bless you. Na Mungu aendelee kuitofaitusha ndoa yako na za wengine. You shall enjoy your marriage and never endure it IJN.
Ubarikiwe na kwako pia Heaven Sent , ukweli ni kwamba nachokiamini siku zote furaha yako uegemea kwenye kuwa na mtazamo chanya mengine Mungu atayaweka sawa binadamu sio wakamilifu lakini tunafundishana ili tuishi pamoja na kuwa na common goal, tunaambiwa katika kitabu kitakatifu Ndoa iheshimike na watu wote lakini ajabu unasikia kataa ndoa, ndoa ni utapeli acha tutavuna tunayoyapanda ,
 
Kwema wakuu!

Hizi habari za kuchapiwa, kuchapiana Wake na Wachumba hizi ni Mvua tuu za rasharasha. Tunasema haya ni mavuno ya awali, bado mambo hayajachanganya. Mambo yakichanganya hapa Dunia itakuwa na tafrani.

1. Mliambiwa Mwanamke anatakiwa Aolewe akiwa Bikra, mkasema bikra haimfanyi Mwanamke kuwa mwaminifu. Mkajiona mnaakili kuwashinda Mababu zenu.
Sawasawa, huu ndio muda wa kuvuna mlichopanda.

2. Mliambiwa na Mababu zenu kuwa Mwanamke hapaswi kumiliki uchumi, kupewa nafasi za utawala.
Ninyi mkajiona mnaakili kuwashinda wazee wenu. Hizi ni Mvua za rasharasha tuu. Nafikiri kizazi kinachofuata ndio mavuno yatachanganya.

3. Mliambiwa na Wazee wenu kuwa Hakuna urafiki baina ya mwanaume na Mwanamke. Mkawaona wazee wenu ni hamnazo.
Ati MTU anaruhusu Mkewe ataniwe taniwe hovyo, simu ya Mkeo imejaa chatting akichat na wanaume, Kwa kisingizio ni marafiki zake, sijui wafanyakazi wenzake, sijui classmates gani Huko.
Mtavuna mlichokipanda.
Eleweni kuwa NI ngumu Sana Mwanamke kuchapwa ndani ya siku moja bila mazoea.

4. Mliambiwa mkapuuza, msioe Wanawake wenye watoto, hasa Kwa kijana ambaye ni mdogo. Mkajifanya mnayajua mapenzi kuliko waliowazaa.
Sasa yakiwakuteni mnaanza kupiga mayowe.
Vijana lazima mjue kuwa kuna tofauti ya mapenzi na Ndoa. Mapenzi ni hisia lakini ndoa au familia ni taasisi inayoongozwa Kwa sheria na kanuni. Wakati mapenzi hayana Kanuni wala sheria.
Sio kosa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na single mother, Ila ni kosa la kimkakati kuingia ndoani na Single mother.

Na hapa nazungumzia Kwa vijana wadogo wenye umri Chini ya miaka 40. Wazee mnaweza kuoa Mwanamke yeyote.

5. Mliambiwa msioe makabila tofauti. Mkajifanya mnaakili kuliko Babu zenu. ATI Kwa kudanganywa na maneno ya kisiasa. Ni kweli Sisi ni taifa moja lakini Sisi ni makabila tofauti yanayounda taifa moja.
Utofauti wa kimakuzi, desturi na Mila huchangia pakubwa kuvurugana ndani ya Familia.
Lakini hamtaki, kisa mnajifanya mmesoma, sijui mnashahada za uzamivu🤣🤣🤣 sasa mtavuna maumivu.

6. Mliambiwa Msiwe na huruma Sana na Wanawake na msiwaamini. Lakini Kwa ulofa wenu mmejichanganya.
Ni kweli wanasura za huruma, ni kweli wanatoaga machozi, ni kweli wanauwezo wa kuigiza ili waonewe huruma lakini kamwe usijichanganye.

Tumieni Akili, tumieni busara na hekima lakini msiongozwe na Huruma za kitoto na mihemko.
Oooh! Nimechepuka mara moja, nisamehe, ni Shetani, hakika Mimi ni Mwanadamu, huku anapiga magoti na kujiuliza. Upuuzi tuu! Sisi kama waafrika hakunaga kitu kinaitwa Msamaha Kwa kesi kama hizo.
Oooh! Huyu mtoto sio wako, Hana kosa lolote. Penda boga na Ua lake. Come on! Mmelogwa

Ooh! Taikon unachuki na Wanawake, hapana sina chuki. Hayo ni matunzo kila mwanaume lazima ayajue.
Vinginevyo vilio havikomi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kitokacho kwa Mungu,hulindwa na Mungu hayo mengine timiza wajibu wako acha woga ,amini katika mazuri na mema
 
Write your reply... Wanawake wa ckuiz wameshindikana kwa hiyo itabidi tuwaache tu Kama walivyo
 
Hujamfanyia vizuri Mkuu.
Hao wengi wao ndio wapo hivyo, Kwa kulijua Hilo usingemuongezea mzigo. Sio Poah ujue
Malengo hayakuwa hayo,nilitaka niishi nae kama mke lakini kadiri siku zilivozidi kwenda nikaona ni changamoto kubwa sana kuishi nae,na hata mzee wangu aliniambia kiutu uzima kuwa nilikua naishi na mtu mzima natakiwa nitafute binti mdogo
 
Daaah mwamba umenigusa sana, nimesafiri kikazi nipo mbali kimkoa nimezinguana na wife kwenye simu ananiambia majira ya jioni nisimtafute kwenye simu na Kama nitakuwa mbishi nitajuta nitakachokisikia(anamaanisha anaenda kuliwa), Nina machungu hayana mfano, mafunzo niliyojia huku hata hayanogi kabisa, nipo nawaza atakavyovuliwa chupi(sjui atavaa shanga au cheni, vyote nimenunulia Mimi) ...aaarrgh!!!

Kwa kweli nikiacha huyu mwanamke, sitakuja kuoa tena maisha yangu yote
Hivi mwanamke wa kukuambia maneno kama hayo,ulipewa Bure au ulitoa mahali, na ulimpata mkoa Gani ? daaaaah nimeumia sana mkuu
 
Hivi mwanamke wa kukuambia maneno kama hayo,ulipewa Bure au ulitoa mahali, na ulimpata mkoa Gani ? daaaaah nimeumia sana mkuu
Itakuwa pale Singapore maana wale wanakuwaga na majibu machafu sana. Singida Girl Mungu anawaona 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom