Mliobahatika kuacha unywaji wa pombe mlitumia formular gani?

Formula yangu nilivyoanza kufuga dread zikawa Zinanicost kuliko kiwango nachotumia kwenye pombe Basi nikaona nichague moja na ofa nazikimbia..mwaka Sasa sijanywa na Sina habari
 
Kuacha ni ngumu ila unaweza kupumzika
 
Mi binafsi nataka kuacha maana naona natumia pesa nyingi kwenye pombe hadi nashindwa kufanya mambo ya maendeleo.Cha kushangza ata nikijaribu kuacha kunywa japo wiki mbili ,mirija yote ya kipato inakata(hakuna cha maana nafanya)[emoji57][emoji57]
 
Si kushauri uache jifunze tu kuimanage usiwe unakunywa kila siku tu
Umeshauri vzuri sana... Me mwenyew nashangaa watu wanaosema mtu aache pombe au anataka kuacha pombe... Pombe inatakiwa uweze kui control kiakili na kimwili...
Mimi nakunywa pombe ijumaa na jumamos pekee, jumapil naweza kunywa kama juma3 ni holiday, yaaan hapo nitakunywa kadri niwezavyo... Katkat ya wiki siwez kunywa pombe kwanza hata chupa 2 naona shida kumaliza...
 
Rahisi sana kuongea
 
Waambie watu wote wanaokuzunguka kuwa unataka kuacha pombe na wafanye kila namna usinywe.

Pressure na msukumo wao vitakufanya uache kabisa

Mfano ukitaka kunywa wao wanakuzuia, mkienda kwenye sherehe wa ahakikishe haugusi pombe hata kidogo, baada ya muda utaweza
 
Mimi nilikunywa wiki nzima bila kula, nikaumwa na kulazwa hospitali. Nilipotoka nikaacha moja kwa moja!
Ebu jaribu hii itakusaidia.
 
Mi binafsi nataka kuacha maana naona natumia pesa nyingi kwenye pombe hadi nashindwa kufanya mambo ya maendeleo.Cha kushangza ata nikijaribu kuacha kunywa japo wiki mbili ,mirija yote ya kipato inakata(hakuna cha maana nafanya)[emoji57][emoji57]
kabla hujafanya matumizi tenga pesa weka benki hata 20k ya malengo yako kama unalenga kufungua kiwanda bas jua hio ndo kazi ya hio pesa inayobaki bas ibajeti na nyingine itunze au oa
 
Cha kwanza kabisa ni kuichukia pombe kwa dhati ya moyo wako huu ndio msingi, epuka kampuni/makundi yako ya awali kuwa siku za kwanza hasa ile miezi miwili ya kwanza. Kunywa maji mengi kila siku kusafisha sumu ya pombe mwilini hadi lita 4.5 kwa siku kwa uzito unaozidi kg 89 kuendelea. Nilikuwa mlevi kupindukia! Nimefanikiwa kuacha kabisa! Mwezi wa 5 huu.
 
Mi siachi pombe labda nipate tatizo la kiafya na wanaonishauri wananijua vizuri majibu nayowapaga hawarudii tena .
 
Pombe sio chakula kwamba usipokunywa unakufa kwa njaa, ukilijua hilo tu unaacha kunywa pombe unabaki unakunywa maji tu
 
Wakuu heshima kwenu,

Nakuja hapa nikiwa na Tatizo moja kubwa sana la unywaji wa Pombe (Beer). Tatizo hili limekuwa kubwa sana kiasi kwamba ni kama nashindwa kuji-control hasa ninapokuwa na pesa mfukoni, Yaani nikiwa na pesa tu basi nitatafuta kiwanja nitapiga mitungi mpaka mida mibaya na kesho yake kuendelea tena hivyo hvyo angalau mpaka pesa ile iishe.

Pombe imeniletea matatizo makubwa hasa kifamilia, Nimegombana na Wife nimegombana na michepuko na nimegombana na ndugu pia. Kwa ufupi ni kama nimetengana na wife kwa namna fulani maana kila mtu anakaa kwake kwa sasa.

Pombe imenisababishia kupata ajali na kupoteza gari yangu nzuri kabisa.

Pombe inaniingiza kwenye hasara nyingi kwenye biashara na kazini, Kwani kuna wakati nakuwa na hela ya offisi ila mm naamua kuipasua pombe na kunywesha watu mpaka inaisha. Imagine naweza kuteketeza laki 8 ndani ya siku mbili au Tatu, Na nisijue imeenda wapi.

Pombe imeniingiza kwenye madeni mengi hasa kwenye Bar mbalimbali wanazoniamini maana wanajua mm ni mnywaji na mlipaji mzuri so huwa wananikopesha mpaka kiwango cha malaki kadhaa na mwisho wa siku najikuta nimeingia kwenye madeni kama hayo.

Pombe pia imeniingiza kwenye madeni na marafiki na ndugu mbalimbali ambao huwa wananikopesha na mimi kushindwa kurejesha maana kuliko nilipe deni ni bora nikakae kwanza ninywe beer mbili tatu nikiwa nafikiria kukulipa hilo deni lako ndugu mdeni.

Pombe inanifanya nashindwa kwenda kanisani Jumapili maana kila jumapili asubuhi nakuwa nipo hoi either kwa pombe za jana yake au kwa pombe nilizoanza kuzipasua jumapili hiyohiyo asubuhi.

Jamani ndugu zangu nafanyaje kuachana na huyu adui pombe, Hapa nilipo nasubiri saa 11 ifike nikapate kitimoto then nianze kushushia vitu.

Pombe inanifanya nasahau kununua nguo nzuri na viatu naona ni bora pesa nipeleke Bar , Yaani kuliko nikafanye shopping ya Laki mbili ni bora hiyo hela nikainywe beer za laki mbili.

Pombe inanifanya sasa nasahau au nashindwa kutuma mahitaji ya watoto kwanzia shule na nyumbani.

Mimi sio mtu wa wanawake sana ila kuna wakati pombe inanifanya pia najiingiza kwenye mambo ya Uzinzi japo ni mara mojamoja ila huwa najuta sana.

Jamani ndugu zangu nafanyaje mimi?

Huwa najaribu kuacha mara kadhaa lakini nikija kurudi ndio inakuwa balaa zaidi yaani inakuwa mara tatu ya ule unywaji kabla ya kuacha.

Kuna muda natamani hii inchi yetu ingekuwa kama zile nchi za waislamu ambazo hawaruhusu pombe , maana ingekuwa hivyo kweli ningeacha. Ila sasa ndio kila nikipita barabarani naona matangazo ya beer, Nikisikiliza redio naona beer yaani ni mtihani kwa kweli

Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disaster

Baada ya kusema hayo yote tafadhali naomba ushauri wenu kwa ambao mmefanikiwa kuachana na pombe mlifanyafanyaje , TAFADHAL SANA naomba ushauri wenu

MWISHO WA UZI

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…