Mliokuwa mnauliza kazi ya Rostam Aziz kwenye ziara ya Rais Samia ya Marekani, hili ndio jibu lenu!

Mliokuwa mnauliza kazi ya Rostam Aziz kwenye ziara ya Rais Samia ya Marekani, hili ndio jibu lenu!

Kumbe nashea mambo makubwa na mtoto ndogo,kaulize kwani Lostam kwanini alijiuzuru ubunge kabla ya muhula wake kwisha,utajulishwa
Nakuuliza wewe useme lini Rostam alijiuzuru ubunge kwa sababu ya ku ya gamba

Statement ya Rostam kujiuzuru ilikuwa live akirekodiwa! Alisema alijiuzuru kwa sababu ya siasa za majitaka na alisema anaachana na siasa ili ajikite kwenye biashara zake! Amefanya hivyo

Wewe leta uthibitisho wako
 
Ngoja waje walinda legacy 😂😂😂
Intelejensia ya Dunia katika karne ya 21 imebadilika sana! Nchi nyingi duniani sasa zinafanya kazi kutengeneza nguvu na ushawishi kwenye uchumi!

Kupata nguvu na ushawishi kwenye Uchumi kunahusisha kutengeneza matajiri wakubwa wenye pesa wanaoweza kuwekeza, kushawishi uwekezaji, kuongeza ajira na mapato ya nchi kupitia ushawishi kwenye uwekezaji

Ukienda Misri kuna Nasser Sawaris anaemiliki viwanda vingi vya cement na shareholder wa kampuni kubwa zaidi ya vifaa vya michezo ulaya Adidas

Ukienda Afrika kusini Kuna Patrice Motsepe
anaemiliki shares nyingi kwenye makampuni mbalimbali ya madini

Ukienda Nigeria kuna Aliko Dangote mwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa cement , Sukari na mafuta na sasa anatengeneza refinery ya kwanza ya mafuta katika Bara la Africa

Tanzania tunae Rostam Aziz mmiliki wa kampuni ya Caspian, Taifa Gas, Tigo na Zantel! Huyu kuaminika kwake kunafanya kuwa mtu ambae Tanzania tunamtegemea sana kwenye kishawishi uwekezaji mkubwa unaotengeneza fursa za ajira na kukuza mapato na Uchumi wa nchi yetu

Urusi wanao wengi akiwemo Roman Abramovich aliyekuwa mmiliki wa club ya Chelsea

Marekani ndo usiseme wanao wengi na wanazidi kuzalisha wengi kila siku kama Jeff bezoz, Bill Gates, Warren Buffet, Elon Musk na wengineo wengi

Mfano wa kazi nzuri za Rostam Aziz kwa Tanzania ni huu! Katika ziara aliyoambatana na Rais Samia Marekani, ameweza kushawishi uwekezaji mkubwa katika kilimo hapa Tanzania kupitia Benki ya maendeleo Afrika.

Hongera Rais Samia, naiona akili kubwa sana kwako inayoenda kuiba dili haraka sana Tanzania kiuchumi

View attachment 2207616
 
Chuki zipi, mbona hatukuwahi kumsikia Mengi au Mo au Bacressa wakitajwa kwa ufisadi nchini,au wao sio matajiri?
Mengi hajawai kutajwa kwenye ufisadi? Una uhakika? Hujui alitajwa kuhusika na kufa kwa NBC? Nico?

Hujui Bakhresa anatajwa kuchukua kiwanda cha National Milling

Hujui Mo anatajwa kuchukua mashamba kwenda kukopea na hafanyi uwekezaji

Kama kutajwa nani hatajwi?
 
Sasa kuchukua shamba kwenda kukopa nao ni ufisadi?niambia Mengi alitajwa Nanani,wapi?Niko kuja kufirisika Mengi alikwisha jiuzuru ujumbe wa bodi,Niko imeliwa na Idi Simba
 
Bakhresa hakuchukua kiwanda cha National Milling bure bali alinunua kihalali toka PSRC. Hilo halina ubishi.
Wewe wasema hivyo ! Kuna wengine wanasema alifisadi kwa kuchukua kwa bei ya kutupa

All in all amefanya uwekezaji mkubwa, analipa kodi na anatengeneza ajira! Hakuna tatizo

Nilikuwa namjibu tu muuliza swali kuwa kama kutajwa kila mtu anatajwa
 
Sasa kuchukua shamba kwenda kukopa nao ni ufisadi?niambia Mengi alitajwa Nanani,wapi?Niko kuja kufirisika Mengi alikwisha jiuzuru ujumbe wa bodi,Niko imeliwa na Idi Simba
Hayo unasema wewe! Hoja yangu kama kutajwa kila mtu anatajwa
 
Lazima masikini tupige kelele kwani ndio tunaoumia mnapo tuhujumu wakati nyinyi mnajificha kwenye mahekalu ya wizi huko Msoga!
Unaumiaje kwa tajiri kuzidi kupata? Kwanza tajiri akizidi kupata hata wewe na wanao mnapata nafasi ya kupata ajira! Tajiri akifirisika wewe utapata kazi wapi?
 
Nilikuwa namjibu tu muuliza swali kuwa kama kutajwa kila mtu anatajwa

Sasa na wewe jibu ROSTAM alivifanya nini viwanda vya ngozi alivyotakiwa kuviendeleza kufuatana na mkataba wa kuuziwa na kama alimaliza lile deni la kununulia kule PSRC?
 
Sasa na wewe jibu ROSTAM alivifanya nini viwanda vya ngozi alivyotakiwa kuviendeleza kufuatana na mkataba wa kuuziwa na kama alimaliza lile deni la kununulia kule PSRC?
Weka uthibitisho kwanza wa Rostam kuhujumu hivyo viwanda
 
Unaumiaje kwa tajiri kuzidi kupata? Kwanza tajiri akizidi kupata hata wewe na wanao mnapata nafasi ya kupata ajira! Tajiri akifirisika wewe utapata kazi wapi?
Hapo ndipo unapoonesha upopoma wako!! Yaani wewe unakubali nchi iibiwe ili mradi Watu wanafanyishwa kazi kwa mshahara kiduchu na unaridhika? Wafanyakazi wa MO Dewji kila leo wanalalamika jinsi anavyowanyonya!!! Hawa sio wawekezaj ikama Bakhresa ni wezi wanaficha akiba zao DUBAI!!!
 
Back
Top Bottom