Mlokole mwenzangu nisikilize! Usimwambie mtu, "kuwa na hofu ya Mungu"

Mlokole mwenzangu nisikilize! Usimwambie mtu, "kuwa na hofu ya Mungu"

Huwa nawashangaa sana mabinti wanaolewa kusema kuwa Wanataka mwanaume mwenye hofu ya Mungu😂.

Kunapahala kwenye bible imeandikwa Mashetani nayo yanahofu hadi yanatetemeka...
Screenshot_20260802_133913_ChatGPT.png
 
Mungu hahofiwi bali anapendwa, anatukuzwa, na anaheshimiwe.

Muda mfupi uliopita nilikuwa kanisani ambapo mtoto mmoja alimpokonya mwenzake pipi, yule aliyepokonywa akalia.

Mchungaji akamwambia yule mpokonyaji, "mungu anakuona", yule mtoto aliyeambiwa hivyo alizimia kwa hofu ya kuonwa na mungu.

Hivyo , nipende kukuambia wewe mlokole mwenzangu kamwe usimwambie mtu awe na hofu ya mungu, bali awe anampenda mungu.

Mbarikiwe nyote!

Seran.
Ni mbinu zao, uwe na hofu ili wazidi kukunyonya.
 
Mungu hahofiwi bali anapendwa, anatukuzwa, na anaheshimiwe.

Muda mfupi uliopita nilikuwa kanisani ambapo mtoto mmoja alimpokonya mwenzake pipi, yule aliyepokonywa akalia.

Mchungaji akamwambia yule mpokonyaji, "mungu anakuona", yule mtoto aliyeambiwa hivyo alizimia kwa hofu ya kuonwa na mungu.

Hivyo , nipende kukuambia wewe mlokole mwenzangu kamwe usimwambie mtu awe na hofu ya mungu, bali awe anampenda mungu.

Mbarikiwe nyote!

Seran.
Wapumbavu wa makanisani hadi mnadai kuwa mna MBARIKI MUNGU !! nini hofu ya Mungu 😁 kufuru kuu sana ....kusema kuwa wewe mwanadamu unambariki Mungu!
 
Wapumbavu wa makanisani hadi mnadai kuwa mna MBARIKI MUNGU !! nini hofu ya Mungu 😁 kufuru kuu sana ....kusema kuwa wewe mwanadamu unambariki Mungu!
Nalibariki jina la mungu😎.
 
Ibrahim akasema , kwa sababu naliona, Yamkini hapana HOFU YA MUNGU mahala hapa, nao wataniua kwasababu ya mke wangu” MWANZO 20:11.

Kumbukumbu la Torati 10:17 S
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa.

Zaburi 89:7
Wewe waogopwa katika baraza la watakatifu; wote wanaokuzunguka wanatiwa hofu kuu.

Malaki 1:14 inasema: "Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema Bwana wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa.

Waebrania 10:31
Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno

KUTOKUMUOGOPA MUNGU kutokuwa na hofu ya Mungu..na watu kutokujua sehemu ya UPANDE WA PILI WA MUNGU.
Kutokujua ghadhabu ya Mungu ,Hasira ya Mungu,ni Mungu mwenye wivu anawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.

kujua upande mmoja tu wa Mungu ule unaomtambua kama ni Mungu,wa REHEMA,NEEMA,si mwepesi wa hasira,anaghairi mabaya,anatuwazia mema,mwenye UPENDO,na msamaha...na mengine mengi..kumewafanya WANADAMU KUJISAHAU..na kumzoea Mungu..na hata kuishi maisha ya dhambi ama kutubu bila kuwa na malengo ya kuziacha huku wakitemtengeneza MUNGU MWENYE kuvumilia dhambi zao ambaye hatawawahukumu kwa vile atawavumilia na pia kuipungukia neema..

7
Rum 6:1-7
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

NA HILI NDIO TATIZO
Watu hawafundishwi upande wa pili wa Mungu kama Mungu mkali wanajua upande wa MUNGU mpole mwwnye huruma ,upendo na neema

wanafikiri Mungu amebadikika kuwa Mungu wa agano jipya sio makali kama yule wa aganano la kale.

Malaki 3:6: “Mimi Bwana sibadiliki”.

Yakobo 1:17: Mungu “habadiliki kama kivuli kinachobadilika”

.Hesabu 23:19: “Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu, abadili nia yake”.
 
Back
Top Bottom