TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

Ukifikiria kifo muda mwingine unajionea maisha hayana maana shenzi kabisa. Yaani unahangaika kutafuta mali halafu inafika siku unaziacha zote unakwenda kupumzika kaburini peke yako ukiwa mpweke, ndugu zako, mke na watoto wanakuacha ulale peke yako.

Ndio maana mimi kwa kila ninachotafuta kwa jasho lazima nitenge 5% mpaka 10% ya kwangu peke yangu nikale bata nipoze moyo. Iwe mshahara, posho, hela ya dili au faida ya kitu fulani hata kama nimeuza kitu.

Yaani nikifa, kila nitakachokiacha duniani ujue 10% yangu nilishafaidi peke yangu kisha wenzangu huku nyuma ndio wajue wanafanyaje.

Haiwezekani nitafute kwa jasho halafu niwaachie 100%! Haiwezekani haiwezekani.
Hata ule kufa ni kufa tu
 
Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo (zaidi ya abiria 70 walikufa) likitoka Tanga kwenda Dar mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff.
Ilitokea mto gani?
Hujachanganya na Msae?
 
Mto Msangazi, nilikuwepo pale that day. One of our staff made great efforts to swim and she saved some lives. It was a very sad moment! One of our RAAWU chairperson perished in the drown!
Yaani mwanamke ndiye aliyeokoa watu mtoni au mimi kimalkia changu ni butu? (One of our made great efgorts to swim and she saved some lives.)
 
Taarifa zilizotufikia leo asubuh ni kuwa mmiliki wa Kampuni za usafirishaji abiria ya Tashrif Hamoud Said amefariki Dunia

Innalillah wainna ilayhi raajiuun

=====

Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga ambae ni mmiliki wa mabasi ya Tashiriif, Hamoud Said Al Habsy amefariki dunia asubuhi ya leo Aprili 12, 2023 baada ya kudondoka ghafla wakati akitekeleza ibada ya swala ya Alfajir, mjukuu wa marehemu, Hamoud Salim Amri Said amethibitisha.

Mwili wa marehemu Hamoud ambae amezoeleka kwa jina la mzee Tashriif, unatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Alasir kwenye makaburi ya Mzalendo kata ya Mwanzange.

Azam news

View attachment 2585301
Kafa kifo kizuri na cha faida.. Hakuna gharama hakuna maumivu hakuna HARI ZA KIFO
 
Taarifa zilizotufikia leo asubuh ni kuwa mmiliki wa Kampuni za usafirishaji abiria ya Tashrif Hamoud Said amefariki Dunia

Innalillah wainna ilayhi raajiuun

=====

Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga ambae ni mmiliki wa mabasi ya Tashiriif, Hamoud Said Al Habsy amefariki dunia asubuhi ya leo Aprili 12, 2023 baada ya kudondoka ghafla wakati akitekeleza ibada ya swala ya Alfajir, mjukuu wa marehemu, Hamoud Salim Amri Said amethibitisha.

Mwili wa marehemu Hamoud ambae amezoeleka kwa jina la mzee Tashriif, unatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Alasir kwenye makaburi ya Mzalendo kata ya Mwanzange.

Azam news

View attachment 2585301
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
 
Baada ya hapo yakawa yanawaka moto sijui hitilafu ya umeme
 
Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo (zaidi ya abiria 70 walikufa) likitoka Tanga kwenda Dar mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff.
Mwaka gani?
 
Pole kwa wafiwa

Ngozi nyeupe hiyo huwa hawana shida kabisa akifa watoto wanaendesha biashara bila Shida

Angekufa mswahili saa hii hata maiti wangekuwa hawahangaiki nayo wanajadili mirathi na kutembezeana vipigo na kuficha mali kila.mtu akificha anachoweza

Hqpo bado ndugu waswahili nao utakuta mbio kuja kudandia mirathi
Weupe hawana Shida mzee ASAS wa ASAS group of Companies alifariki lakini cheki kampuni inakwenda bila shida

Watoto wanaiendesha vizuri

Afe mswahili watagombania mirathi hadi sufuria na vijiko na nguo zake hadi za ndani
Mfano St Mary's schools
 
Apumzike kwa Amani!
Nachelea kukihusisha kifo chake na mfungo. Mfungo uzingatie umri, hali ya kiafya n.k. Waislamu wengi hupoteza maisha kipindi cha mfungo, kwani wanafanya mabadiliko ya vile mwili ulivyozoea kwa ghafla (abruptly), na pia kwa kiwango cha juu (severely). Kama kuna mushkeli ya kiafya, inakuwa ni sawa na kujiua mwenyewe.
Umekosea sana sana ila ndo ubinaadam huna budi kusamehewa
 
Back
Top Bottom