Cookie na Moderators Wengine wa JamiiForums
Paw,
YinYang,
Active,
Moderator na
JamiiForums nimeshawalalamikiemi mno kuhusu huyu Mtu ambaye leo niseme Kwenu kuwa mnamlea mno na huenda pia mkawa mnafurahia jinsi anavyopenda Kunidhihaki, Kunichokoza, Kunishambulia na hata Kunidhalilisha kwa kila Mada ambayo naianzisha hapa JamiiForums.
Najua anachokitaka ni Majibizano nami kisha nipandwe na Hasira ( Jazba ) na nianze Kumjibu hovyo kisha upesi sana Watu Wanaonichukia hapa Waniripoti Kwenu na mnipe BAN ya Wiki Mbili, Mwezi au Miezi Mitatu afurahie / Wafurahi.
Mimi mbona hata huwa sijishughulishi na Mada zake hapa JamiiForums? Hivi kama hanipendi GENTAMYCINE na havutiwi na Uwasilishaji wangu wa Masuala hapa JamiiForums kwanini haachani na Mimi na Kutwa amekuwa ni Mtu wa Kunifuatafuata tu?
Tafadhali kama huyu
LIKUD anatumika Kimkakati ili Kunichokoza Kimakusudi GENTAMYCINE ili nihamaki nijibizane nae na mnipige BAN nisiwepo hapa JamiiForums semeni tu Wazi Kwangu kuwa nanyi hamnitaki na sitakiwi ili niwaachieni Jamvi lenu hili kwa Amani sawa? Inakera.
Na mwambieni huyu Mtu kuwa hawezi / haiwezi kamwe Vita ya Maneno na Majibizano nami hapa JamiiForums kama nikiamua ila Najiheshimu, Nauheshimu huu Mtandao Wenu na nawaheshimu sana Followers wangu na hata wale Wanaonikubali hivyo sitaki Kuwakwaza.
Cc: JamiiForums Founder
Maxence Melo
Na naomba hii post isifutwe tafadhali.