Mnawezaje kuishi na Wageni wanaochagua sana vyakula?

Mnawezaje kuishi na Wageni wanaochagua sana vyakula?

Noma Sana ,nakumbuka miaka ya 90 hiv mgeni akiwa anataka kuja, mama alikua anaremba nyumba na toilet paper, chakula tunachinja kuku kinawekwa kwenye hotpot ,kinafunikiwa na kitambaa cha kutarizi spesheli kwa mgeni / wageni.
Ni utamaduni mzuri kumkirimu mgeni..
 
Huku mtimua?
Maana wanatumbi wengi tuna hang hang kwenye vyakula hivo?
Nilimrudisha mkuu nilikaa nae miezi miwili tu nikanyoosha mikono juu, na nilimtoa ngara huko nauli nilitoa 150k iliniumaaa.
 
Sasa madhara si hicho kichefuchefu ? Bora mboga yangu iwe maharage kila siku kuliko dagaa , toka nilitafunia kokwa la konokono hazipandi kabisa ,dagaa nitawapa kuku wakue halafu niwachinje hizi dagaa nizile zikiwa ndani ya kuku.
Navyopenda ugali na dagaa naona kama unakosa utamu 😂
 
Navyopenda ugali na dagaa naona kama unakosa utamu 😂
Mimi napenda ndizi za maharage na mboga za majani, au maziwa , ila dagaa ugali makande hapana kabisa 👐
 
Mimi napenda ndizi za maharage na mboga za majani, au maziwa , ila dagaa ugali makande hapana kabisa 👐
hahaha mimi nakula almost kila kitu kipikwe tu vizuri..
Nilishawahi kwenda sehemu walikua wanachinja ng’ombe na nnavopenda nyama niliona sifiki, sasa hiyo nyama ilivokua imepikwa!
Sitasahau hadi nakufa niliondoka na njaa yangu 😂
 
Na uzuri mmoja Africa karibu yote ukitoa Daslamu jogoo mkubwa huwa ni wa mgeni😋
Huwa ni heshima ya kipekee...

umepika wali, kuku, mboga za majani, viazi na matunda katika hivyo lazima tu mgeni kuna anachotumia, kuliko kuuliza watu 'una njaa, utakula nini?'

Kwenye vinywaji ni sawa kuuliza mtu 'coffee?, soda?, beer ,juice ?' hata maji usiweke maana hachelewi kusema 'nipe maji tu' kumbe anataka beer.. 😂
 
hahaha mimi nakula almost kila kitu kipikwe tu vizuri..
Nilishawahi kwenda sehemu walikua wanachinja ng’ombe na nnavopenda nyama niliona sifiki, sasa hiyo nyama ilivokua imepikwa!
Sitasahau hadi nakufa niliondoka na njaa yangu 😂
Waliipikaje hio nyama?
 
Huwa ni heshima ya kipekee...

umepika wali, kuku, mboga za majani, viazi na matunda katika hivyo lazima tu mgeni kuna anachotumia, kuliko kuuliza watu 'una njaa, utakula nini?'

Kwenye vinywaji ni sawa kuuliza mtu 'coffee?, soda?, beer ,juice ?' hata maji usiweke maana hachelewi kusema 'nipe maji tu' kumbe anataka beer.. 😂
Mambo ya kuambiwa karibu ukisikie upo nyumbani hayo , kumbe ni utapeli tu bwashee , huwa wageni tunaelewa hizo code ndio maana tunachukua maji tu😁
 
Back
Top Bottom