Pre GE2025 Mnyika ampongeza Mbowe kwa kugharamia shughuli zote za Uchaguzi CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Licha ya mambo yanayoonekana kafanya Mbowe, alitaka kukipeleka chama sehemu mbaya sana na round hii deal lilishtukiwa mapema.

Watanzania inabidi watambue hakuna ugharamikiaji wa shughuri wenye thamani kuliko uhai wa wapigania demokrasia na haki wa kweli.

Kuna wadau wengi wamekuwa mstari wa mbele kuchangia hizo gharama lakini hawataki kujulikana.

Mbowe aliifanya Chadema kama saccoss yake, sasa hivi kutokuendelea kuonekana anachangia chama hakuna madhara yoyote yatakayoikwamisha Chadema kupigania demokrasia ya kweli.
 
Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika amempongeza Freeman Mbowe kwa kugharamia shughuli zote za Uchaguzi CHADEMA
Unaona? Hiki chama.CHADEMA kilikuwa mali yake ndo maana ya kauli hii! Chama kinatakiwa kiwe mali ya wanachama na kinatakiwa kiendeshwe kwa mapato ya chama kutoka LUZUKU + MICHANGO, HADA za chama
 

Matajiri walikuwa wakimpa pesa mbowe kimya kimya, kwa hakika Lissu atawaanika
 
Hongera Sana Mh Lissu Ila pia pole Sana Mh Mbowe .

Wanasiasa mjifunze kutoshindana na wakati.

Pesa haiwezi kukusaidia
 
Ni ujumbe Lissu anapewa hapo. Awe tayari tayari. Yaani akiwa kama kiongozi, ndio hatakiwi kutoa hela mfukoni ila Kuna point inahitajika milioni 500 ya chap, inabidi kama mwenyekiti utoe udai baadaye. Hapo ndio atakamatika.
 
Haya mambo ya mtu mmoja kugharamia taasisi ndio huwa nayakataa; why mtu mmoja awe na pesa zaidi ya chama?
 
Baraza Kuu CHADEMA lashindwa kuendelea na mikutano yake kutokana na team Lissu kushindwa kulipia ukumbi wa mlimani city, Wajumbe wameanza kumkumbuka Mbowe mapema sana.

Inasemekana wanatafuta Ukumbi wa bei rahisi kwa muda huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…